Rais wa Urusi asema nchi yake inalenga kuwa yenye ‘’nguvu zaidi duniani'' katika masuala ya baharini
Amezungumza hayo katika sherehe za ‘Siku ya Jeshi la Wanamaji la Urusi, na kutia saini sera mpya ya majini ya Shirikisho la Urusi linalofanyika mara moja kwa mwaka.
Moja kwa moja
Rais wa Urusi asema nchi yake inalenga kuwa yenye ‘’nguvu zaidi duniani'' katika masuala ya baharini

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Rais wa Urusi Vladimir Putin Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema nchi yake inalenga kuwa yenye ‘’nguvu kubwa baharini,’’ akishindana na Marekani kwa ushawishi.
Amezungumza hayo katika sherehe za ‘Siku ya Jeshi la Wanamaji la Urusi, na kutia saini sera mpya ya majini ya Shirikisho la Urusi linalofanyika mara moja kwa mwaka.
Alionya kuwa kile alichokiita ‘’tamaa ya Marekani kutawala bahari’’ inawakilisha moja ya vitisho vikubwa kwa Urusi, pamoja na upanuzi wa NATO.
Urusi imeahidi kwamba hivi karibuni itamiliki kombora la Zircon hypersonic, ambalo limeundwa kujibu ukiukaji wowote wa utaifa na uhuru wa Urusi.
Kulingana na shirika la Interfax, sera ya Urusi imebainisha kuwa nchi hiyo inaweza kutumia nguvu za kijeshi kutetea maslahi yake katika Bahari ya Dunia ikiwa uwezekano wa kidiplomasia utashindikana.
Pia inabainisha ‘’maendeleo ya mahusiano na mataifa ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini na maeneo ya karibu na bahari, ikiwa ni pamoja na Bahari ya Mediterania na Bahari Nyekundu.’’
Hata hivyo, nyaraka hiyo kuhusu masuala yake ya baharini iliyoidhinishwa Juni 2015, inatambuliwa kuwa batili.
Soma zaidi:
Mzozo wa mpaka kati ya Afghanistan na Iran: Taliban yasema mtu mmoja aliuawa

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Taliban katika siku za nyuma walipigana na vikosi vya Irani kwenye mpaka (picha kutoka maktaba Februari 2022) Vikosi vya Taliban vya Afghanistan vimepambana na walinzi wa mpaka wa Iran kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili.
Serikali ya Afghanistan inasema afisa wake mmoja aliuawa katika mapigano ya Jumapili, yaliyotokea katika eneo la mpaka kati ya jimbo la Nimroz nchini Afghanistan na eneo la Hirmand la Iran.
Kila nchi ililaumu nyingine kwa tukio hilo.
Kumekuwa na mapigano kadhaa katika mpaka tangu wanamgambo wa Taliban wachukue udhibiti wa Afghanistan mwaka mmoja uliopita.
Iran haijaitambua serikali ya Taliban mjini Kabul.
Hali halisi ya mapigano ya hivi punde haijulikani.
‘’Tuna mmoja aliyeuawa na mmoja amejeruhiwa,’’ msemaji wa polisi wa Nimroz Bahram Haqmal aliambia shirika la habari la Reuters.
Katika mkoa wa Sistan va Baluchestan nchini Iran, afisa wa Hirmand Maysam Barazandeh alinukuliwa na shirika la habari la Fars akisema hakujawa na majeruhi kwa upande wa Iran.
Shirika la habari la Iran la Tasnim lilisema mapigano yalianza baada ya vikosi vya Taliban kujaribu kuinua bendera yao ‘’katika eneo ambalo si la Afghanistan’’, na kusababisha kurushiana risasi kwa ‘’dakika kadhaa’’.
‘’Vikosi vyetu vilijibu tukio hilo ilivyohitajika,’’ Bw Barazandeh alisema.
Mwezi uliopita wizara ya mambo ya nje ya Iran iliripoti kifo cha mlinzi wa mpaka wa Iran kufuatia tukio jingine katika eneo hilo hilo.
Oleksiy Vadatursky: Tajiri wa nafaka wa Ukraine auawa katika shambulio la Urusi

Chanzo cha picha, NIBULON
Maelezo ya picha, Oleksiy Vadatursky alikuwa na thamani ya $450m (£369m), kulingana na makadirio ya 2020 na Forbes. Mfanyabiashara mmoja tajiri zaidi nchini Ukraine ameuawa akiwa na mkewe katika shambulizi ‘’kubwa’’ la Urusi katika mji wa kusini wa Mykolaiv.
Oleksiy Vadatursky, 74, na mkewe Raisa walikufa wakati kombora lilipopiga nyumba yao usiku kucha, maafisa wa eneo hilo walisema.
Bw Vadatursky alimiliki Nibulon, kampuni inayohusika na mauzo ya nafaka nje ya nchi.
Pia alikuwa amepokea tuzo ya ‘’shujaa wa Ukraine’’.
Meya wa Mykolaiv Oleksandr Senkevych alisema huenda ni mashambulizi makubwa zaidi ya Warusi katika jiji hilo kufikia sasa.
Kulikuwa na uharibifu wa hoteli, uwanja wa michezo, shule mbili na kituo cha huduma, pamoja na nyumba.
Mykolaiv iko kwenye njia kuu kuelekea Odesa, bandari kubwa zaidi ya Ukraine kwenye Bahari Nyeusi, na imepigwa mara kwa mara tangu Urusi ilipoanzisha uvamizi wake tarehe 24 Februari.
Soma zaidi:
Uhuru amkabili naibu wake Ruto kwa madai kwamba anawindwa kuuawa

Maelezo ya picha, Uhuru amkabili naibu wake William Ruto Rais Uhuru Kenyatta amemjibu Naibu wake William Ruto akisema hana nia ya kumdhuru yeye, familia yake au washirika wake kufuatia madai ya Naibu Rais kwamba maisha yao yako hatarini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Barabara ya Nairobi Expressway katika kituo cha JKIA, Rais Kenyatta alimwambia naibu wake azingatia kutangaza manifesto yake na kuepuka kueneza uwongo.
“Baada ya wiki moja tutakuwa tunatimiza haki yetu ya kikatiba ya kuchagua utawala unaofuata. Ninataka kuwahimiza Wakenya kudumisha amani katika kipindi kilichosalia cha kampeni. Na baada ya siku ya uchaguzi. Hakuna haja ya kuitana majina. Kila mtu, ikiwa ni pamoja na mimi binafsi, ana uhuru wa kumpigia kura mgombea anayempendelea,” alisema.
“Uamuzi uko kwa Wakenya. Hakuna haja ya kusema uwongo.
Si umenitukana miaka mitatu? Je, si nimekuwa mmiliki wa ofisi hii kwa miaka hiyo mitatu? Nilikuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Sasa, ninapojitayarisha kukabidhi mamlaka, na kuwa na uwezo mdogo, unafikiri nina wakati wa kukutafuta? Tafadhali zingatia kampeni zako na uuze manifesto yako. Ninamalizia kazi yangu. Niacheni,” alisema rais.
“Iwapo Wakenya wataamua kukupigia kura, ni sawa. Wakiamua vinginevyo, tutarudi nyumbani pamoja, na maisha yataendelea,” alisema.
Aidha amewataka Wakenya kuwa watulivu, na kufanya mambo yanayofaa, na kuwataka wanasiasa kuwafahamisha Wakenya kuhusu mipango yao ya kubadilisha maisha.
Mnamo Ijumaa, Julai 29, Naibu Rais William Ruto alimtaka mkuu wa nchi akome kutoa vitisho na kuwaacha watu wake akidai kuwa kuna njama ya kumdhuru pamoja na familia yake na washirika wake.
“Nataka nikuombe rais uache kutishia watu. Kazi yako ni kuhakikisha kuna amani ya nchi, acha kutuambia tutakujua wewe ni rais, acha kututia ugaidi hatuwezi kutishiwa. ‘Mradi hutaua watoto wangu, nitakabiliana na wewe lakini tafadhali tuheshimiane,” Ruto aliteta.
Naibu rais pia alitoa wito kwa mkuu wake kuonyesha shukrani kwa msaada aliopata wakati akitafuta kura za kushinda mihula yake miwili.
Soma zaidi:
Leicester inaadhimisha miaka 50 tangu kuhama kwa raia wa Kiganda

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Jamii za Wahindi na Wapakistani ziliamriwa kuondoka Uganda ndani ya siku 90 mnamo tarehe 4 Agosti 1972 Michezo mitatu ya kuigiza inachezwa mjini Leicester kuadhimisha miaka 50 tangu kuhamishwa kwa Waganda wa Asia.
Zaidi ya Waasia 27,000 walifurushwa na dikteta wa Uganda Idi Amin mwaka 1972 na maelfu wakaweka makazi Leicester.
Sasa, kila mmoja ameandika hadithi kuhusu familia zao kuhusu kilichotokea wakati wa kutoroka Uganda, ambazo zinasimuliwa kupitia maonyesho.
Jumba la maonyesho lilisema kuwa tamthilia hizo zilikuwa ‘’kitu kizuri’’ kilichohusisha ‘’hadithi za kipekee’’ za miaka 50 iliyopita.
Soma zaidi:
Habari za hivi punde, Urusi inashambulia vikali eneo la kusini mwa Ukraine

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Wiki kadhaa za makombora ya Urusi yamesababisha uharibifu mkubwa huko Mykolaiv, kama picha hii ya Alhamisi inavyoonyesha Ukraine inasema mji wa kusini wa Mykolaiv umekumbwa na mashambulizi ‘’mkubwa’’ ya Urusi kufanya mashambulizi usiku kucha.
Mmoja wa watu tajiri zaidi wa Ukraine, Oleksiy Vadatursky, na mkewe Raisa waliuawa, gavana alisema.
Bw Vadatursky, 74, anamiliki Nibulon, kampuni kubwa ya kilimo.
Meya wa jiji aliita ufyatuaji wa makombora ‘’bila shaka kuwa ndio mkali zaidi kuliko mwingine wowote’’.
Kulikuwa na uharibifu wa hoteli, uwanja wa michezo, shule mbili na kituo cha huduma, pamoja na nyumba.
Mykolaiv iko kwenye njia kuu ya kuelekea Odesa, bandari kuu ya Ukraine, na imekuwa ikigongwa mara kwa mara.
Wakati huo huo, Urusi imeahirisha sherehe za Siku ya Wanamaji katika eneo la Crimea inayolikalia.
Sababu iliyotolewa na Gavana wa Sevastopol Mikhail Razvozhayev ilikuwa shambulio la ndege zisizo na rubani za Ukraine kwenye makao makuu ya Fleet ya Bahari Nyeusi.
Kwa muda mrefu, ya kivita imekuwa ikiwa katika eneo la Sevastopol.
Lakini afisa mkuu wa Ukraine, Serhiy Bratchuk, alipuuzilia mbali ripoti hiyo ya Urusi na kusema ni ‘’uchokozi’’.
‘’Ukombozi wa Crimea yetu utafanyika kwa njia tofauti na kwa ufanisi zaidi,’’ alisema.
Vikosi vya Urusi vilitwaa eneo la Crimea mwaka wa 2014. Hilo lilishutumiwa kimataifa kuwa haramu na lilisababisha vikwazo dhidi ya Urusi.
Soma zaidi:
Brazil: Mama afungiwa ndani ya nyumba na kuteswa kwa miaka 17

Chanzo cha picha, RIO DE JANEIRO MILITARY POLICE/EPA
Maelezo ya picha, Jiko kuukuu ndani ya chumba ambacho mama na watoto wawili walifungiwa kwa miaka 17 Mwanamke wa Brazil amezungumzia masaibu yake ya kufungiwa - pamoja na watoto wake wawili - na mumewe kwa miaka 17, vyombo vya habari vya ndani vinaripoti.
Familia hiyo iliokolewa kutoka kwa nyumba hiyo katika kitongoji cha Guaratiba, magharibi mwa Rio de Janeiro siku ya Alhamisi, polisi walisema.
Mume aliyefungia familia yake kwa miaka yote hiyo amekamatwa.
Katika maoni kwa mamlaka yaliyonukuliwa na tovuti ya habari ya Brazil G1, mwanamke huyo alidai kuwa mumewe alisema angetoka nje ya nyumba hiyo tu atakapofariki dunia.
Kulingana na polisi, mwanamume huyo - aliyetajwa kama Luiz Antonio Santos Silva - na mkewe walikuwa wameoana kwa miaka 23.
Baada ya kuokolewa, inasemekana mama huyo aliambia mamlaka kwamba kuna wakati walikaa bila chakula kwa kwa siku tatu, na mara nyingi walinyanyaswa kimwili na kisaikolojia.
Nyumba walimofungwa pia ilikuwa mbovu, yenye mwanga mdogo na mazingira ya ndani ni machafu, picha zilizotolewa na polisi zinaonyesha.
Watoto hao wawili waliokomaa walikuwa wamefungwa kamba, ni wanyonge na wenye njaa walipopatikana, kulingana na polisi.
Wana umri wa miaka 19 na 22, ripoti ya vyombo vya habari vya ndani.
Kapteni William Oliveira wa kikosi cha kijeshi alisema katika maoni yaliyonukuliwa na gazeti la O Dia la Brazil kwamba awali alifikiri wawili hao walikuwa watoto kwa sababu ya kiwango chao cha utapiamlo.
‘’Tulipoona hali ya watoto hao wawili, tulidhani hawangenusurika kifo kwa wiki nyingine,’’ mkazi mmoja wa eneo hilo alisema.
Baada ya kuokolewa watatu hao walipelekwa hospitalini mara moja kutibiwa kutokana na upungufu mkubwa wa maji mwilini na utapiamlo, vyombo vya habari vya nchini vinaripoti.
Soma zaidi:
Italia: Kilio juu ya mauaji ya wahamiaji wa Kiafrika mitaani

Chanzo cha picha, POLIZIA DI STATO/QUESTURA DI MACERATA
Maelezo ya picha, Polisi wa eneo hilo walitoa picha ya eneo kufuatia shambulio hilo Kifo cha mhamiaji aliyeshambuliwa mchana kweupe katikati mwa Italia kimezua hasira.
Shambulio dhidi ya mfanyabiashara huyo raia wa Nigeria lililotekelezwa mtaani na mwanamume mwingine katika kituo cha mji wa Civitanova Marche lilinaswa kwenye video siku ya Ijumaa.
Video hiyo, iliyochukuliwa na watazamaji bila jaribio lolote la kuingilia kati, inaonyesha mwathirika akiwa ameshikiliwa chini na raia mmoja mzungu.
Muitaliano mwenye umri wa miaka 32 amekamatwa kwa tuhuma za mauaji na wizi.
Video ya shambulio hilo - ambayo imesambazwa sana kwenye tovuti za habari za Italia na mitandao ya kijamii - imeshtua jamii, huku wengi wakionyesha ‘’kutojali’’ kwa mashahidi.
Mazingira ya tukio hilo hayaeleweki.
Wito wa haki ikipatikane
Mwathiriwa ametajwa kuwa Alika Ogorchukwu, baba aliyeoa na mwenye watoto wawili.
Mke wake, aliyetajwa kwa jina la Charity Oriachi, alishindwa kuzuia machozi yake alipokuwa akiambia vyombo vya habari jinsi alivyoonyeshwa mwili wa mumewe ukiwa umelala chini.
Siku ya Jumamosi mamia ya watu kutoka jamii ya eneo la Nigeria waliingia katika mitaa ya Civitanova Marche, katika mkoa wa Marche, kudai haki.
Shambulio hilo pia limelaaniwa na wanasiasa wa Italia.
Enrico Letta, kiongozi wa chama cha mrengo wa kushoto cha Democratic Party, alisema kilichotokea ni cha ‘’kusikitisha’’.
‘’Kutosikika kwa ukatili. Kuenea kwa kutojali. Hakuwezi kuwa na uhalali,’’ aliandika kwenye ujumbe wa Twitter.
Kiongozi wa mrengo wa kulia Matteo Salvini pia alionyesha kukerwa na kifo hicho, akisema ‘’usalama hauna rangi’’ na ‘’kuna haji ya kurejeshwa kuwa haki.’’
Soma zaidi:
Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja
