Kiongozi wa upinzani nchini
Uganda na mgombeaji mara mbili wa urais,
Nobert Mao ametia saini makubaliano ya ushirikiano na chama tawala cha National
Resistance Movement kufuatia mkutano na Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni
katika Ikulu ya Entebbe siku ya Jumatano.
Museveni alituma video fupi
ya kutiwa saini kwa makubaliano hayo kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Aliwasifu viongozi wa Chama
cha Democratic kwa kile alichotaja kuwa ni ishara ya ukomavu, mtazamo wa mbele
na siasa za kujenga.
Mao amekuwa rais wa chama cha
Democratic tangu 2010 na alianza kuonekana katika siasa za kitaifa mwaka 1996
alipochaguliwa kuwa mbunge ambapo alihudumu kwa mihula miwili.
Alijitokeza kwa ufasaha wake
na msimamo wake wa kupinga.
Chama chake kimekumbwa na
migawanyiko ya ndani kwa miaka kadhaa.
Kabla ya uchaguzi wa 2021,
alipoteza viongozi kadhaa katika chama chake na kujiunga na National
Unity Platform cha Bobi Wine.
Wafuasi wa Mao wataona
maendeleo haya kama ushirikiano mzuri wa vyama viwili lakini wale wanaompinga
watahisi kuwa anatoa lawama kwa shutuma zao za awali alizotoa kwa Museveni.
Wakati huo huo Rais wa Uganda
Yoweri Museveni ametetea uamuzi wa serikali yake wa kutotoa ruzuku au kupunguza
ushuru akisema pesa hizo zingetumika kutatua shida zinazoikabili nchi.
Alikuwa akihutubia taifa
katika hotuba iliyorushwa kwenye televisheni Jumatano usiku huku kukiwa na
ongezeko kubwa la kupanda kwa gharama za maisha kutokana na kupanda kwa bei ya
mafuta na uhaba wa chakula katika baadhi ya maeneo nchini.
Rais Museveni alisema ruzuku inawapotosha watu kufikiri
kwamba kuna mengi na wanashindwa kujipanga kiuchumi kwa kile walichonacho na
hatimaye kumaliza akiba ya kigeni ya nchi.
Alisema kupunguzwa kwa ushuru
pia kutasababisha kukwama kwa miradi ya miundombinu.
Rais Museveni alituma video ya kusaini makubaliano na Democratic Party kwenye Twitter: