Wanajeshi 15,000 wa Urusi wameuawa vitani Ukraine: Mkurugenzi wa CIA
"Makadirio ya hivi punde kutoka kwa jumuiya ya kijasusi ya Marekani yangekuwa kitu karibu na 15,000 [majeshi ya Urusi] waliouawa
Moja kwa moja
Watakaouza Unga wa ugali Ksh.200 kukamatwa Kenya
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Rais Uhuru Kenyatta
Serikali ya Kenya imesema itawakamata na kuwafungulia mashitaka watakaopatikana wakiuza unga wa ugali wa kilo mbili kwa zaidi ya shilinghi mia moja.
Katika hotuba kwa taifa hapo jana, Rais Uhuru Kenyatta aliagiza kuwa bei ya unga kote nchini ishukishwe kutoka shilingi mia mbili na tano kwa pakiti ya kilo mbili hadi shilingi mia moja.
Msemaji wa Serikali Kanali mstaafu Cyrus Oguna ameiambia BBC kuwa mfumo wa kuwafidia wauzaji wa bidhaa hiyo walioinunua kwa bei ya juu kabla ya tangazo la jana ulifikiwa na watafahamishwa vilivyo namna gani utakavyofanya kazi.
Kumekuwa na maswali jinsi bei hiyo mpya ya unga itakavyoshughulia na fidia itakuwaje au jinsi gani serikali itakavyowafikia wafanyabishara wa rejareja kote nchini katika mpango huo wa fidia.
Baadhi ya wenye maduka hawajaanza kuuza unga wa mahindi kwa bei hiyo mpya kwa kuhofia kuingia hasara.
Habari za hivi punde, Rais wa Marekani Joe Biden apatikana na Virusi vya Corona
Rais wa Marekani Joe Biden amepimwa na kukutwa na virusi vya Covid-19. Ikulu imesema kiongozi huyo ameonekana kuwa na "dalili zote kali".
Mzee huyo mwenye umri wa miaka 79, ambaye amepata chanjo kamili ya Corona, atajitenga katika Ikulu ya White House na kuendelea kutekeleza majukumu yake yote, taarifa ilisema.
Maelezo zaidi kuhusu habari hii yataendelea kukujia, endelea kufuatilia BBC Swahili.
Ulaya yaongeza riba kwa mara ya kwanza katika miaka 11
Chanzo cha picha, Getty Images
Benki Kuu ya Ulaya (ECB) imepandisha viwango vya riba kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka 11 inapojaribu kudhibiti mfumuko wa bei wa katika kanda hiyo ya Ulaya.
ECB imepandisha kiwango chake cha riba kutoka asilimia 0.5 hadi 0.0% siku ya Alhamisi, kukiwa na mpango wa kuongezeka zaidi baadaye mwaka huu. Kiwango hicho kimekuwa hasi tangu 2014 ili kuhimiza benki kukopesha badala ya kuweka pesa benki.
Bei za watumiaji zilipanda kwa kiwango cha rekodi cha 8.6% katika miezi 12 hadi kufikia Juni mwaka huu. Bei hiyo ni ya juu kupita kiwango cha benki cha asilimia 2%.
Benki kuu duniani kote, ikiwa ni pamoja na Benki ya Uingereza na Hifadhi ya Shirikisho la Amerika, zimekuwa zikipandisha viwango vya bei zinapoongezeka.
Kupanda kwa gharama za nishati, mafuta na chakula kunaongeza gharama ya maisha, na kuweka shinikizo kwa kaya.
Meta yaondoa maudhui hatari ya Kenya kabla ya uchaguzi
Chanzo cha picha, Getty Images
Kampuni kubwa ya teknolojia ya Meta imeondoa maelfu ya machapisho yanayowalenga watumiaji wa Kenya kwenye mtandao wake wa kijamii wa Facebook kwa kukiuka sera zake kabla ya uchaguzi wa Agosti.
Miaka minne iliyopita, wakuu wa kampuni ya ushauri ya Cambridge Analytica inaonekana walinaswa kwenye kamera wakijivunia udhibiti walioutumia katika uchaguzi wa urais wa Kenya uliozozaniwa mwaka 2017, na kampuni yao ilishutumiwa kwa kuchimba data za binafsi za Wakenya kwenye Facebook kumsaidia Rais Uhuru Kenyatta kushinda.
Facebook sasa inasema katika ripoti mpya kwamba imeondoa machapisho zaidi 37,000 ya kueneza matamshi ya chuki na 42,000 kwa kukiuka sera zake dhidi ya uchochezi, katika muda wa miezi sita kabla ya tarehe 30 Aprili.
Kampuni hiyo pia inasema imekataa matangazo 36,000 ya kisiasa kwa kutofuata sheria zake za uwazi.
Facebook inasema kuwa imeshirikiana na wakaguzi huru wa nchini Kenya kukanusha habari potofu kabla ya uchaguzi wa Agosti.
Mkurugenzi wake wa sera za umma Mashariki na Pembe ya Afrika, Mercy Ndegwa, anasema wameimarisha udhibiti kwenye majukwaa yao ambayo yatarahisisha kutambua na kuondoa maudhui ambayo yanaweza kusababisha ghasia zinazohusiana na uchaguzi.
Makombora ya ‘’Uturuki’’ yalipigwa na Iraqi na kusababisha vifo na majeruhi
Raia tisa , wakiwemo watoto
wawili, wameuawa na wengine 33 kujeruhiwa katika shambulio la kombora la
Uturuki katika jimbo la Dohuk kaskazini mwa Iraq,
kwa mujibu wa maafisa.
Televisheni ya Iraqi iliripoti
kuwa "shambulio zito" lilipiga
hoteli ya kifahari katika mji wa Zakho, ambao uko kwenye mpaka wa Kurdistan
baina ya nchi hiyo na Uturuki.
Shirika la habari la
Iraq limesema kuwa watu wote waliokufa walikuwa ni watalii.
Maafisa wa Iraqi
wameishutumu Uturuki kwa shambulio hilo, lakini serikali mjini Ankara imekana
kuhusika na tukio hilo.
Mkuu wa jimbo la Zakho
, Mushir Bashir, alisema kuwa wengi wa waliokufa walikuwa ni "watalii wa
kiarabu kutoka Iraqi, wengi wao kutoka maeneo ya kati na kusini mwa nchi ".
"uturuki ilikipiga
kijiji mabomu mara mbili kwa siku",alinukuliwa
akiliambia shirika la habari la AFP.
Habari za hivi punde, Mkurugenzi wa CIA: Wanajeshi wa Urusi wanaokadiriwa kuwa 15,000 waliuawa
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mkurugenzi wa CIA William Burns
Mkurugenzi
washirika la ujasusi la Marekani (CIA )William
Burns amesema kuwa: "Makadirio ya hivi karibuni kutoka
ujasusi wa marekani ni kwamba Urusi imewapoteza watu 15,000 katika vita vya Ukraine na mara tatu ya idadi
hiyo walijeruhiwa ."
Taarifa hiyo
imechapishwa katika jukwaa la usalamala Aspen , na vyombo vya habari vya Reuters na CBS.
"Na
Ukraine pia labda iliumiwa -kidogo, lakini bado , unafahamu, vifo hivi ni muhimu," aliongeza Mkurugenzi wa CIA.
Kulingana na ujumbe wa
Twitter, mwandishi wa wa CBS, Mkurugenzi wa CIA alipoulizwa kuhusu hali ya
Putin alisema: "Kuna uvumi mwingi kuhsu hali ya afya ya Putin, lakini tunavyojua , afya yake ni nzuri zaidi ,"
Alisema Burns.
Urusi na Ukraine: Mengi zaidi
MOJA KWA MOJA:Biden amuonya Putin: ''Madikteta watagharamika
YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Uongozi wa Conservative : Sunak na Truss waanza kinyang’anyiro cha kumrithi Boris Johnson
Chanzo cha picha, PA MEDIA
Wagombea wawili katika kinyang’anyiro cha uongozi wa chama cha Conservative leadership wamewasilisha mipango yao kwa wajumbe wa chama ambao watamchagua mrithi wa Boris Johnson.
Rishi Sunak na Liz Truss walipata kura nyingi zaidi katika uchaguzi wa mwisho wa wabunge Jumatano.
Akiandika katika gazeti la Daily Telegraph, Bw Sunak alisema atapanga "mageuzi makubwa kama yale ambayo Margaret Thatcher aliyafanya katika miaka ya 1980".
Katika Daily Mail, Bi Truss aliahidi "kukata kodi, kuboresha biashara, na kuweka sera rafiki za biashara za Conservative".
Wawili hao waliibuka kuwa wagombea wakuu baada ya Bi Truss kubadilisha ushindi mdogo wa Waziri wa biashara Penny Mordaunt, ambaye wakati mmoja alipendelewa, kwa kupata uungaji mkono wa Waconsertvative 113 dhidi ya Bi Mordauntaliyepata 105.
Kansela wa zamani Bw Sunak,ambaye aliendelea kuongoza miongoni mwa wabunge, alishinda kwa kura 137.
Kura za maoni zinaonyesha kuwa ni mtu ambaye ana umaarufu wa kiwango cha chini zaidi miongoni mwa wajumbe wa chama cha Conservative ambao watapiga kura kwa mgombea ajaye mwezi ujao.
Unaweza pia kusoma:
Kujiuzulu kwa Boris Johnson: Kipi kinafanyika sasa?
Boris Johnson: Sakata nne zinazomtia matatani Waziri Mkuu wa Uingereza
Chama cha upinzani cha DP nchini Uganda chatia saini makubaliano ya kushirikiana na Museveni
Chanzo cha picha, AFP
Kiongozi wa upinzani nchini
Uganda na mgombeaji mara mbili wa urais,
Nobert Mao ametia saini makubaliano ya ushirikiano na chama tawala cha National
Resistance Movement kufuatia mkutano na Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni
katika Ikulu ya Entebbe siku ya Jumatano.
Museveni alituma video fupi
ya kutiwa saini kwa makubaliano hayo kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Aliwasifu viongozi wa Chama
cha Democratic kwa kile alichotaja kuwa ni ishara ya ukomavu, mtazamo wa mbele
na siasa za kujenga.
Mao amekuwa rais wa chama cha
Democratic tangu 2010 na alianza kuonekana katika siasa za kitaifa mwaka 1996
alipochaguliwa kuwa mbunge ambapo alihudumu kwa mihula miwili.
Alijitokeza kwa ufasaha wake
na msimamo wake wa kupinga.
Chama chake kimekumbwa na
migawanyiko ya ndani kwa miaka kadhaa.
Kabla ya uchaguzi wa 2021,
alipoteza viongozi kadhaa katika chama chake na kujiunga na National
Unity Platform cha Bobi Wine.
Wafuasi wa Mao wataona
maendeleo haya kama ushirikiano mzuri wa vyama viwili lakini wale wanaompinga
watahisi kuwa anatoa lawama kwa shutuma zao za awali alizotoa kwa Museveni.
Wakati huo huo Rais wa Uganda
Yoweri Museveni ametetea uamuzi wa serikali yake wa kutotoa ruzuku au kupunguza
ushuru akisema pesa hizo zingetumika kutatua shida zinazoikabili nchi.
Alikuwa akihutubia taifa
katika hotuba iliyorushwa kwenye televisheni Jumatano usiku huku kukiwa na
ongezeko kubwa la kupanda kwa gharama za maisha kutokana na kupanda kwa bei ya
mafuta na uhaba wa chakula katika baadhi ya maeneo nchini.
Rais Museveni alisema ruzuku inawapotosha watu kufikiri
kwamba kuna mengi na wanashindwa kujipanga kiuchumi kwa kile walichonacho na
hatimaye kumaliza akiba ya kigeni ya nchi.
Alisema kupunguzwa kwa ushuru
pia kutasababisha kukwama kwa miradi ya miundombinu.
Rais Museveni alituma video ya kusaini makubaliano na Democratic Party kwenye Twitter:
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Hakuna thibitisho la kijasusi kwamba Putin ni mgonjwa-Mkuu wa CIA
Chanzo cha picha, EPA
Hakuna
taarifa za kijasusi kwamba Vladimir Putin hana utulivu au afya mbaya,
mkurugenzi wa CIA amesema.
Kumekuwa
na uvumi unaoongezeka wa vyombo vya habari ambao haujathibitishwa kwamba Bw
Putin, ambaye anatimiza miaka 70 mwaka huu, anaweza kuwa anaugua, labda
saratani.
Lakini
William Burns alisema hakuna ushahidi wa kupendekeza hili, akitania kwamba
alionekana "mwenye afya njema".
Maoni
yake yalikuja huku Marekani ikitangaza kuwa itaipatia Ukraine silaha zaidi za
masafa marefu.
Hapo
awali Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov alisema mwelekeo wa kijeshi
wa Urusi nchini Ukraine hautasalia ‘mashariki
pekee’ na alisema mkakati wa Moscow umebadilika baada ya nchi za Magharibi
kuipatia Ukraine silaha hizo.
"Kuna
uvumi mwingi kuhusu afya ya Rais Putin na kwa kadiri tunavyoweza kusema yu
mzima sana," Bw Burns alisema katika Jukwaa la Usalama la Aspen huko Colorado.
Akijibu baada ya jibu lake kuzua kicheko kwa waliokuwa
wakimzikiliza aliongeza kuwa hii haikuwa
tathmini rasmi ya kijasusi.
Bw
Burns, ambaye aliwahi kuwa balozi wa Moscow, alisema amekuwa akimtazama na
kushughulika na kiongozi huyo wa Urusi kwa zaidi ya miongo miwili.
Bw Putin
ni "muumini mkubwa wa udhibiti, vitisho na kulipiza kisasi" na tabia
hizi zimezidi kuwa ngumu katika muongo mmoja uliopita huku mzunguko wa washauri
wake ukipungua , mkuu wa CIA alisema.
"Ana
hakika kwamba hatima yake kama kiongozi wa Urusi ni kuirejesha Urusi kama
mamlaka kuu. Anaamini kuwa jambo la msingi katika kufanya hivyo ni kuunda upya
nyanja ya ushawishi katika nchi jirani na Urusi na hawezi kufanya hivyo bila kuidhibiti
Ukraine."
Wanajeshi 15,000 wa Urusi wameuawa vitani Ukraine: mkurugenzi wa CIA
Chanzo cha picha, SERGEI ILNITSKY/EPA
Marekani inakadiria kuwa wanajeshi wa Urusi waliofariki vitani nchini Ukraine
kufikia sasa wamefikia takriban 15,000 na pengine 45,000 waliojeruhiwa, mkurugenzi wa
CIA amesema, akionya kwamba Kyiv imepata hasara kubwa pia.
"Makadirio ya hivi punde kutoka kwa jumuiya ya kijasusi
ya Marekani yangekuwa kitu karibu na 15,000 [majeshi ya Urusi] waliouawa na
labda mara tatu ya waliojeruhiwa. Kwa hivyo ni kiwango kikubwa cha hasara,
"William Burns alisema katika Jukwaa la Usalama la Aspen huko Colorado.
"Na, Waukraine wameteseka pia - labda kidogo kuliko
hiyo. Lakini, unajua, maafa ya watu
wengi’