Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Boris Johnson: Nina huzuni kuacha kazi bora zaidi duniani

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amejiuzulu wadhifa wake. Akitoa hotuba yake alisema:''Ninasikitika kuacha kazi nzuri zaidi duniani lakini ndiyo hali halisi''

Moja kwa moja

  1. Mtoto wa mbuzi mwenye masikio marefu apata umaarufu duniani

    Kila mtu amesikia kuhusu Dumbo: kikaragosi cha tembo ambaye kutokana na masikio makubwa sana alidhihakiwa na wenzake na kulazimishwa sarakasi kali.

    Dumbo sio mnyama pekee ambaye amepata umaarufu kwa kucheza michezo wa kuvuta vitu virefu.

    Kutana na Simba - mtoto wa mbuzi kutoka Karachi, Pakistani ambaye masikio yake mawili yana urefu wa 54cm (21in) kila moja.

    Na muda unavozidi kwenda. Badala ya kudhihakiwa, sasa amekuwa nyota ulimwengu: ameshinda mashindano ya urembo na maisha ya kupendeza.

    Mfugaji wa mbuzi huyu ‘Simba’, Mohammad Hasan Narejo, aliliambia shirika la habari la AFP kwamba hata anakaribia kufika katika rekodi za dunia za Guinness.

    Kwa sasa hakuna kipengele cha "mbuzi mwenye masikio marefu zaidi," kwa hivyo haijulikani ikiwa ni kweli masikio ya Simba yanavunja rekodi.

    Iwe ni maskio mrefu zaidi duniani au la, mbuzi huyo tayari amekuwa mnyama mashuhuri kwenye mitandao ya kijamii nchini Pakistani baada ya picha za masikio yake ya kuvutia kuanza kusambaa.

    Lakini pamoja na kuipandisha nyota ya mbuzi huyo, kuzaliwa na sifa hizo ndefu kunaleta changamoto za kipekee.

    Kwa mfano, ukweli kwamba wao ni hatari kwa safari. Ili kuzuia ajali, Bw Narejo ameamua kukunja masikio ya Simba mgongoni mwake na pia amebuni uzi wa kuvaa unaofanya kazi hiyo hiyo.

    Hofu nyingine ni wafugaji wanaoshindana, ambao umakini wao usiohitajika unamtia wasiwasi Bw Narejo. Amegeukia sala na desturi za kitamaduni ili kuzuia nia mbaya inayoweza kutokea kutoka kwa wengine.

    "Tunamkariri aya za Kurani na kumpulizia ili kutupilia mbali jicho baya," aliiambia AFP.

    Hatimaye, hata hivyo, mipango yake ni kabambe zaidi. Anataka kumkuza mbuzi huyu ili kutangaza taswira ya Pakistan kuwa kinara wa ufugaji wa mbuzi duniani.

    • Je mbuzi anaweza kuendesha baiskeli ?
    • Jinsi wanyama wanavyogundua majanga hata kabla yatokee
    • Sababu inayochangia ndege wanaohama hufurika mijini
  2. Rais wa zamani aliyepatikana na hatia arejea Burkina Faso

    Rais wa zamani wa Burkina Faso, Blaise Compaoré, amerejea nchini mwake baada ya kukaa uhamishoni kwa miaka saba.

    Serikali inasema iko tayari kufanya mazungumzo na jeshi kama sehemu ya juhudi za upatanisho.

    Mwandishi mmoja wa habari amekuwa akiweka picha zake kwenye mtandao wa Twitter:

    Mwezi Aprili mwaka huu Compaoré alihukumiwa kifungo cha maisha bila kuwepo mahakamani kwa jukumu lake katika mauaji ya kiongozi aliyechaguliwa wakati wa uhuru, Thomas Sankara, kupitia mapinduzi yaliyomuingiza madarakani miaka 35 iliyopita.

    Haijabainika kama Compaoré atakabiliwa na mchakato wa mahakama kwa kuwa amerejea Burkina Faso.

    Mawakili wanaowakilisha familia ya Bw Sankara wametaka akamatwe.

  3. Uturuki yaachilia meli ya Urusi iliyo na nafaka zilizoibiwa za Ukraine - Wizara ya Mambo ya Nje

    Uturuki haikupakua, lakini iliachilia meli ya Urusi iliyokuwa na nafaka za Ukraine zilizoibiwa, Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Ukraine iliripoti.

    ‘’Shukrani kwa kuingilia kati kwa mamlaka husika ya Ukraine, meli hii haikuweza kupakuliwa bidhaa zilizoibiwa na iliwekwa kizuizini. Ombi lilitumwa kwa upande wa Uturuki kukamata meli na mizigo. Wakati huo huo, kupuuza rufaa ya upande wa Ukraine, Meli hiyo iliachiliwa jioni ya Julai 6,’’ Wizara ya Mambo ya Nje iliripoti.

    Kuhusiana na hali hiyo, balozi wa Uturuki mjini Kyiv aliitwa kwa Wizara ya Mambo ya Nje.

    Mnamo Julai 1, meli ya Zhibek Zholy iliingia kwenye bandari ya Uturuki ya Karasu, ikisafirisha nafaka kinyume cha sheria kutoka Berdyansk iliyokaliwa.

    Soma zaidi:

  4. Mtangazaji wa Marekani azua mjadala kuhusu wanawake wajawazito wa Kenya

    Mtangazaji wa Fox News Emily Compagno amezua mjadala kwenye mtandao wa Twitter baada ya kutoa maoni kwamba "Wanawake wajawazito wa Kenya hawawezi kutoka majumbani kwa hivyo hawana haki ya kupiga kura".

    Maneno hayo a,eyasema wakati akitoa maoni yake kuhusu haki za kupiga kura za wanawake nchini Marekani na akalinganisha na Kenya na Oman.

    Sheria ya Kenya inatoa haki sawa ya kupiga kura kwa watu wazima wote na wanawake wajawazito wanapewa kipaumbele katika foleni za kupiga kura.

    Wanasiasa wanawake na watumiaji wa Twitter nchini wamekosoa maoni ya Compagno.

    Gavana wa kaunti ya Kitui, Charity Ngilu, alimtaka mtangazaji huyo "kuanza kwa kuitafuta Kenya kwenye ramani kwanza labda".

    Esther Passaris, Mwakilishi wa Mwanamke wa mji mkuu, Nairobi, alimtaka mtangazaji wa Fox News kubatilisha kauli yake.

    "Wanawake wajawazito nchini Kenya wanaruhusiwa kutoka nyumbani. Wanawake wajawazito nchini Kenya wanaweza kupiga kura. Wanawake wajawazito wanapewa kipaumbele kwenye mistari ya kupiga kura," aliandika katika mtandao wa twitter.

    Mwandishi maarufu Yvonne Owuor alikosoa kwa kuandika "hoja za Kimarekani".

    "Ungebarikiwa kuishi katika Kenya yetu nzuri. Sasa, tafadhali wape dada zetu, mama zetu, wake zetu msamaha wanaostahili."

    • Viongozi wanawake Kenya wamekuwa na mchango gani katika siasa za nchi hiyo?
    • Uchaguzi wa Kenya 2022: Kwanini kura za Wakikuyu zinapiganiwa katika uchaguzi?
    • Uchaguzi Kenya 2022: Mfahamu mgombea mwenza wa Raila Odinga Martha Karua
  5. Mume wa Nicki Minaj Kenneth Petty ahukumiwa kifungo cha nyumbani cha mwaka mmoja

    Mume wa Nicki Minaj amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja nyumbani kwa kushindwa kujiandikisha kama mhalifu wa ngono.

    Kenneth Petty alitakiwa kufahamisha mamlaka alipohama kwa sababu ya jaribio la ubakaji kutoka mwaka 1995.

    Lakini kijana huyo mwenye umri wa miaka 44 alikiri kushindwa kufanya hivyo alipohamia California pamoja na Nicki Minaj mwaka wa 2019.

    Sasa amehukumiwa na kutozwa faini ya $55,000 (£46,000), kulingana na Ofisi ya Mwanasheria wa Marekani.

    Chini ya sheria za Marekani, wakosaji wa ngono waliosajiliwa wana siku tano za kutoa maelezo yao ikiwa makazi yao yatabadilika.

    Petty hapo awali alikana kosa hilo katika kesi yake ya mahakama mwaka 2020, lakini alibadilisha ombi lake Septemba iliyopita.

  6. Marekani ipo tayari kuishauri Tanzania kuhusu usalama wa mpaka wake na Msumbiji

    Serikali ya Marekani ipo tayari kutoa ujuzi na ushauri kwa Tanzania katika masuala ya kiusalama ili kuimarisha ulinzi kwenye mpaka wake na nchi ya Msumbiji.

    Katika mahojiano maalumu na BBC Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright alieleza namna ambavyo Marekani inavyoguswa na tishio la usalama katika baadhi ya mipaka ya Tanzania ikiwemo eneo la mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.

    Aidha ameelezea athari ya mabadiliko ya tabia nchi lakini pia hatua iliyopigwa na serikali ya Tanzania katika kukuza demokrasia.

    Balozi Wright alisema, “Kimsingi Marekani inaguswa na masuala ya kiusalama ya dunia nzima, na hata ukiangalia masuala ya kiusalama katika mipaka ya kusini mwa Tanzania. Kama Balozi natambua na kuweka suala hilo kuwa kipaumbele cha ubalozi wangu…

    …tunafikiri kwamba masuala haya yasipoangaliwa kwa umakini yanaweza kuleta madhara, hivyo tumekuwa tukijielekeza katika masuala haya, na tunafurahi kuona Rais Samia Suluhu ameushirikisha umoja wa nchi za kusini mwa SADC ili ziweze kutoa suluhisho na sisi tupo tayari kutoa ushirikiano wetu wa kimawazo pale utakapo hitajika.”

    Hali ya Demokrasia Tanzania

    Balozi amepongeza jitihada za serikali ya Tanzania ya sasa kutokana na mazungumzo ambayo yamekuwa yakiendelea kati ya serikali, chama tawala na vyama wa upinzani.

    Balozi huyo alisema,Rais Samia ameonyesha jitihada kubwa katika suala zima la maridhiano ya kisiasa amekuwa na mikutano kadha kukutama na viongozi wa upinzani ili kupata mariadhiano ya kisiasa na kupata maoni yao hivyo sisi Marekani tunasimama na serikali na kwamba tunaunga mkono kufikiwa kwa maridhiano hayo.

    Athari za mabadiliko ya tabia nchi

    Hata hivyo Balozi Donald amezungumzia nia ya Marekani kuisadia Tanzania katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

    Alisema, “Naomba niseme kwamba suala la mabadiliko ya tabia nchi ni janga linazoathiri mataifa mbali mbali duniani, hivyo mabadiliko ya tabia nchi ni eneo muhimu ambalo tunaliangazia pia,na ambalo limekuwa likisababisha ukame,katika ukanda wote wa nchi za jangwa la Sahara,ilikuwa ni mwaka mmoja tu uliopita Kenya ilikumbwa na janga nzige waliodhoofisha uzalishaji katika mashamba ya mawese…

    “…kwa hiyo kutaendelea kuwepo na majanga kama hayo hivyo tunataka kushirikiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha tunatoa msaada,” alisema Balozi huyo.

    • Mgogoro wa ugaidi Msumbiji: Watu wanaotekeleza vitendo vya kigaidi ni nani, wanataka nini Msumbiji?
    • Shambulizi la Palma Msumbiji: Kwanini kujihusisha kwa kundi la IS kunatiliwa chumvi
  7. Johnson: Nina huzuni kuacha kazi bora zaidi duniani

    Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amejiuzulu wadhifa wake. Akitoa hotuba yake alisema:

    ''Ninasikitika kuacha kazi nzuri zaidi duniani lakini ndiyo hali halisi''

    ‘’Ninataka ujue jinsi ninavyohuzunishwa na kuacha kazi bora zaidi duniani,’’ waziri mkuu anasema.

    "Nimekubaliana na Sir Graham Brady, mwenyekiti wa wabunge wetu wa viti maalum, kwamba mchakato wa kumchagua kiongozi mpya uanze sasa na ratiba itatangazwa wiki ijayo. Na leo nimeteua Baraza la Mawaziri kuhudumu, pia nitaendelea kuongoza hadi kiongozi mpya atakapochaguliwa.’’

    ''Inatia uchungu kutoona miradi yangu ikikamilika''

    Johnson anasema ni upuuzi kubadilisha serikali – na kukataa wazo la uchaguzi mkuu - wakati ‘’tunatimiza majukumu mengi na makubwa hali ya kiuchumi ikiwa ngumu sana ndani na kimataifa’’.

    ‘’Najuta kutofanikiwa katika majadiliano na inatia uchungu kutoona mawazo na miradi mingi ikitimia.’’

    Bwana Johnson ameshukuru umma kwa ‘’mapendeleo makubwa’’

    ‘’Zaidi ya yote, ninataka kuwashukuru nyinyi, umma wa Uingereza, kwa mapendeleo makubwa mliyonipa,’’ amesema.

    Anasema umma utahudumiwa kuanzia sasa hadi waziri mkuu mpya atakapochukua wadhifa huo.

    Mustakabali wetu pamoja ni uliong’aa - Johnson

    Waziri mkuu amemaliza kauli yake kwa kusema kwamba hadi pale atakapopatikana mbadala wake, maslahi ya umma yatatekelezwa.

    ‘’Kuwa waziri mkuu ni elimu ya kivyake - nimesafiri kila sehemu ya Uingereza na nimekutana na watu wengi wenye asili ya Uingereza isiyo na kikomo na wako tayari kushughulikia matatizo ya zamani kwa njia mpya.

    ‘’Hata kama mambo yanaweza wakati mwinginekuonekana kuwa giza nene, mustakabali wetu pamoja ni mzuri, uliong’aa,’’ Johnson anasema huku akipigiwa makofi anapoondoka.

    Soma zaidi:

  8. Rais wa Sri Lanka amuomba Vladimir Putin wa Urusi msaada wa kununua mafuta

    Rais wa Sri Lanka amesema amemwomba Vladimir Putin wa Urusi kulisaidia taifa lake lenye matatizo ya fedha kuagiza mafuta wakati huu ambao nchi yake inakabiliwa na mzozo mkubwa zaidi wa kiuchumi tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka 1948.

    Gotabaya Rajapaksa alisema "alikuwa na mazungumzo yenye tija" na Putin.

    "Niliomba msaada wa mkopo kuagiza mafuta," Bw Rajapaksa alitweet akimaanisha mazungumzo yake na kiongozi huyo wa Urusi.

    Hii inakuja baada ya waziri wa nishati wa Sri Lanka kuonya mwishoni mwa juma kwamba nchi hiyo huenda ikakosa petroli hivi karibuni.

    Rajapaksa pia alisema "ameomba kwa unyenyekevu" safari za ndege kati ya Moscow na Colombo kuanza tena baada ya shirika la kubeba bendera la Urusi Aeroflot kusimamisha huduma mwezi uliopita.

    Siku ya Jumatano, mamia ya watu waliandamana kwenye mitaa ya mji mkuu Colombo kupinga serikali.

    • Mamia wakamatwa maandamano ya kupinga serikali Urusi
    • Mkutano wa Jumuiya ya madola Sri Lanka
  9. Jamila Kizondo: Nyota wa Tik tok anayekikuza kiswahili ughaibuni,

    Wakati dunia inapoadhimisha Siku ya Kiswahili Duniani hii leo ikiwa ni mara ya kwanza tangu kutambuliwa na Umoja wa Mataifa.

    Roncliffe Odit amezungumza na Jamila Kizondo, mzaliwa wa Mombasa, Kenya anayeishi Atlanta, Georgia Marekani, lakini anayekiendeleza Kiswahili kupitia video zake katika mitandao ya kijamii

  10. Kenya yafungia akaunti za benki za kampuni ya teknolojia ya Nigeria

    Mahakama nchini Kenya imefungia akaunti za benki zinazoendeshwa na kampuni ya malipo ya mtandaoni ya Nigeria huku kukiwa na madai kwamba zinahusishwa na ulaghai na utakatishaji fedha.

    Shirika la Urejeshaji Mali ya Kenya (ARA) lilisema na lilipewa maagizo ya kufungia jumla ya shilingi 6.2bn ($52.5m; £43.9m) katika akaunti 62 za benki za Flutterwave na makampuni mengine sita.

    Flutterwave ni kampuni ya Nigeria ambayo inaruhusu biashara za Kiafrika na wateja wao kufanya malipo ya mtandaoni.

    Mwaka jana ilikua kampuni inayoongozwa na mwafrika kukua kasi zaidi na kufikisha thamani ya mabilioni ya dola.

    Mamlaka ya Kenya inasema hakukuwa na maelezo au nyaraka za kuunga mkono shughuli za kifedha za Flutterwave katika akaunti 29 ambazo zilisambazwa katika benki tatu.

    Akaunti hizo zilikuwa na shilingi za Kenya, dola za Kimarekani, euro na pouni ya Uingereza.

    Flutterwave pia inashutumiwa kwa kutokuwa na kibali kutoka kwa Benki Kuu ya Kenya kutoa huduma za malipo.

    "Uchunguzi zaidi ulibaini kuwa kuna sababu za msingi za kuamini kuwa fedha hizo ni mapato ya uhalifu yaliyopatikana kutoka kwa vyanzo visivyo halali na mlalamikiwa ambayo yanahitaji kuhifadhiwa hadi kuwasilishwa na kusikilizwa kwa ombi la kutaifisha lililokusudiwa," wakala huyo alinukuliwa akiwasilisha.

    mahakama. Mtendaji mkuu wa Flutterwave Gbenga Agboola ameripotiwa kukanusha madai hayo, na kuliambia jarida la Peoples Gazette la Nigeria kwamba mashtaka hayo yanaweza kuwa ya kisiasa.

    “Kwa nini kampuni za Nigeria nchini Kenya zinalengwa na Kenya ARA? Haya yanajiri karibu na wakati wao wa uchaguzi,” alinukuliwa akisema.

    Hakuna benki yoyote iliyotoa maoni juu ya suala hilo.

  11. Habari za hivi punde, Boris Johnson atajiuzulu kama kiongozi wa Conservative leo

    Boris Johnson atajiuzulu kama kiongozi wa Conservative leo - ataendelea kuhudumu kama Waziri Mkuu hadi msimu wa vuli.

    Kinyang'anyiro cha uongozi wa Conservative kitafanyika msimu huu wa kiangazi na Waziri Mkuu mpya atakuwa tayari kwa mkutano wa chama cha Tory mnamo Oktoba.

  12. Waziri Mkuu wa Ethiopia kuhutubia bunge kuhusu mauaji ya halaiki

    Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed anatarajiwa kulihutubia bunge la nchi hiyo leo Alhamisi huku shinikizo likiongezeka kwa serikali yake kuhusu mauaji ya mamia ya makabila madogo katika mashambulizi mawili tofauti katika wiki za hivi karibuni.

    Ghasia za mwezi uliopita katika vijiji vya wakulima katika eneo la Oromia, magharibi mwa nchi hiyo, zilisababisha vifo vya zaidi ya watu 300.

    Wengine waliuawa katika shambulio jingine wiki mbili baadaye.Hii itakuwa mara ya pili kwa Bw Abiy kufika mbele ya wabunge katika kipindi cha chini ya mwezi mmoja.

    Wakati mamlaka zimekimbilia kulaumu kundi la waasi kwa mashambulizi ya Oromia, hasira ya umma imeelekezwa kwa serikali na baadhi ya maafisa na kuwashutumu kwa kushiriki.Maandamano yalifanyika katika maeneo mengi katika wiki za hivi karibuni.

    Na huku ghasia zikiendelea kushuhudiwa katika maeneo kadhaa ya nchi, maswali yanaibuliwa kuhusu uwezo wa serikali kukabiliana na ukosefu wa usalama.

    Kumekuwa na utulivu katika mapigano katika vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe kaskazini mwa Ethiopia baada ya kutangazwa kwa mapatano ya kibinadamu mwezi Machi.

    Lakini mizozo iliyoenea katika maeneo mengine inaonyesha kuwa nchi bado inapambana na ghasia.

    • Ethiopia: Mzozo wa Tigray ulivyogeuka vita vya wenyewe kwa wenyewe
    • Vita vya Ethiopia mwaka mmoja baadaye: Jinsi ya kumaliza mahangaiko
  13. Kundi la M23 lasema halitaondoka kutoka sehemu ilizochukua nchini DRC

    Waasi wa M23 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanasema mazungumzo katika mji mkuu wa Angola kati ya Rais wa Rwanda Paul Kagame na Rais wa Kongo Félix Tshisekedi hayatasimamisha mapigano mashariki mwa nchi hiyo.

    Mazungumzo ya Jumatano mjini Luanda - chini ya upatanishi wa Rais João Lourenço - yalikubali kusitishwa kwa mgogoro kati ya Rwanda na DR Congo, ofisi ya rais wa Kongo ilisema kwenye Twitter.

    Viongozi hao pia walitoa wito wa "kusitishwa mara moja kwa uhasama na kujiondoa mara moja na bila masharti kwa M23 kutoka sehemu walizoshikilia nchini DRC".

    Lakini msemaji wa M23 Meja Willy Ngoma aliambia BBC kuwa kundi hilo halijiondoi kwenye sehemu hizo

    "Kujiondoa ili twende wapi?" Meja Ngoma aliuliza. “Sisi ni Wakongo. Unataka tuishi bila nchi?" Alisema hili ni tatizo la kisiasa la Kongo linalopaswa kutatuliwa miongoni mwa Wakongo.

    Kundi hilo lenye silaha linasema linapigania "lengo zuri’ na kutetea haki za Wakongo wanaozungumza Kinyarwanda - wale ambao inasema wametengwa, lakini serikali ya Kongo inaishutumu kwa kuungwa mkono na Rwanda.

    Uhusiano kati ya Rwanda na DR Congo umekuwa wa wasiwasi tangu M23 kuanza tena mashambulizi katika jimbo la Kivu Kaskazini mwishoni mwa mwezi Machi baada ya takriban muongo mmoja bila mashambulizi makubwa.

    Kila upande unalaumu upande mwingine kwa kuanzisha mapigano hayo, ambayo yamewakosesha makazi zaidi ya watu 170,000, kulingana na Umoja wa Mataifa.

    Hivi majuzi waasi hao waliuteka mji wa Bunagana kwenye mpaka na Uganda.

    DR Congo inaishutumu Rwanda kwa kuunga mkono kundi la M23, ambalo Kigali na M23 wamekuwa wakikanusha mara kwa mara.

  14. Rocco Morabito: Mlanguzi mtoro "mfalme wa kokeni wa Milan’ akabidhiwa kwa Italia

    Mmoja wa watu wanaosakwa sana nchini Italia, Rocco Morabito, amewasili Roma baada ya kusafirishwa kutoka Brazil, alikokuwa amejificha.

    Anajulikana kama "mfalme wa cocaine wa Milan", Morabito alikamatwa Mei mwaka jana katika operesheni ya pamoja ya polisi wa Brazil na Italia.

    Morabito mwenye umri wa miaka 55 atatumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa ulanguzi wa dawa za kulevya.

    Bosi huyo wa mafia alitumia miongo kadhaa kukimbia akitumia kitambulisho ghushi huko Amerika Kusini.

    Hatimaye polisi walimtafuta mwaka jana hadi João Pessoa, mji wa bandari kaskazini-mashariki mwa Brazili, ambako alikamatwa pamoja na mwanachama mwingine wa kundi la 'Ndrangheta mafia, Vincenzo Pasquino. Pasquino amehukumiwa kifungo cha miaka 17 jela kwa ulanguzi wa dawa za kulevya.

    Kuwasili kwa Rocco Morabito huko Roma kunamaliza msako wa miongo kadhaa.

    Mzaliwa wa mji wa Calabrian wa Africo na akiwa na uhusiano wa kifamilia na bosi wa mafia Giuseppe Morabito, Rocco Morabito alikuwa mtu muhimu katika 'Ndrangheta, mtandao unaoenea wa uhalifu ambao unadhibiti ulanguzi mkubwa wa kokeini nchini Italia na kwingineko.

    Akiwa kijana, Morabito hivi karibuni alijipatia umaarufu kama mlanguzi wa dawa za kulevya huko Milan, akianzisha njia kuu za magendo ya kokeini kutoka Amerika Kusini hadi Italia.

    Alirekodiwa akijaribu kuagiza zaidi ya tani moja ya kokeini kutoka Amerika Kusini lakini alitoweka muda mfupi baadaye.

    Polisi wanadhani alikimbilia Brazil, ambako aliishi chini ya jina la Francisco Capeletto.

    Kutoka hapo, alihamia nchi jirani ya Uruguay, ambako aliishi katika mapumziko ya Punta del Este kwa angalau miaka 13.

  15. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya moja kwa moja leo