Hakuna kizuri au matumaini katika mazungumzo ya amani-Urusi

"Kilicho chanya ni kwamba upande wa Ukraine angalau umeanza kutunga na kuweka kwenye karatasi kile inachopendekeza. Hadi sasa tulikuwa hatujaweza kufikia hilo,"

Moja kwa moja

  1. Mpaka hapa tumefika mwisho wa matangazo haya, tukutane tena hapo kesho.Asante

  2. Urusi yadai kuwaajiri wapiganaji 16,000 wa Mashariki ya Kati

    m

    Chanzo cha picha, Reuters

    Hapo awali tulikuletea habari kwamba wanajeshi wa Syria walikuwa wakipewa hadi £5,000 kwa mwezi kupigana katika mstari wa mbele kwa ajili ya Urusi nchini Ukraine - sasa tuna habari zaidi kutoka kwa mwandishi wa BBC Arabic Emir Nader.

    Urusi inasema imewasajili takribani wanajeshi 16,000 kutoka Mashariki ya Kati, huku katika mitandao ya kijamii nchini Syria ikijaa maombi ya watu kujiunga na wanajeshi wa Urusi.

    Mmoja wa waajiri aliiambia BBC: "Kuajiri watu kwa Ukraine ni sawa na jinsi tulivyoajiri Libya; kuna wawakilishi katika maeneo mbalimbali. "Una haki ya kubadilisha uamuzi wako baada ya kutuma maombi. Hakuna mtu atakulazimisha kwenda."

    Uchumi wa Syria, ambao tayari umeharibiwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, sasa unakabiliwa na kupanda kwa bei kwa bidhaa muhimu kama ngano, ambazo nyingi hutoka Ukraine na Urusi - na kufanya ofa ya Urusi kuonekana ya kuvutia zaidi.

    Urusi imeunga mkono utawala wa Syria wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo na taarifa za habari za serikali ya Urusi zinadai kuwa wanajeshi wa Syria wanataka kurudisha fadhila hiyo.

  3. Rais Samia arejesha tozo ya mafuta iliyoondolewa mwezi huu

    M

    Rais Samia Suluhu ametangaza kurudisha tozo ya Sh100 iliyokuwa ikitozwa katika mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa nchini Tanzania.

    Wizara ya Nishati iliondoa tozo hiyo Februari 28, 2022 ikisema uamuzi huo umetokana na kuendelea kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia kunakosababishwa na vita kati ya Urusi na Ukraine.

    Wakati anapokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Rais Samia ametangaza kuirejesha tozo hiyo.

    Amesema suala la upandaji wa bei za mafuta yamekuwa yakipanda tangu katikati ya mwaka jana na kwamba walichukua hatua yakupunguza tozo kwa mara ya kwanza ili kushusha bei ya mafuta kwa wananchi.

    Ruka X ujumbe, 1
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 1

    Mwezi mmoja uliopita, Wizara ya nishati nchini Tanzania ilisema ilifikia uamuzi wa kuondoa tozo ya shilingi 100 kwa kila lita ya Dizeli, Petroli na mafuta ya taa ambayo ilipaswa kulipwa na watumiaji wa mafuta nchini humo kuanzia mwezi Machi mpaka Mei , mwaka huu huku taifa hilo likiendelea kutathmini mwenendo wa soko la dunia katika mafuta.

    Hatua hii ilikadiriwa kupunguza mapato ya serikali ya shilingi bilioni 30 za Tanzania kwa kila mwezi.

    Ruka X ujumbe, 2
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 2

    Taarifa ya wizara ya nishati ilisema pia kuwa uamuzi huo uliaenda sambamba na maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa ya kupunguzwa kwa tozo zinazotozwa na taasisi mbalimbali katika bidhaa za mafuta hapa nchini zenye thamani ya Sh102 bilioni kwa mwaka, kwa lengo la kupunguza bei za mafuta na kuwapa unafuu wananchi.

    Taasisi zilizoguswa na maelekezo hayo ya Rais Samia zilikuwa ni, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (tozo ya udhibiti), Mamlaka ya Bandari (tozo ya miundombinu), Mamala ya Mapato Tanzania (tozo ya kuchakata taarifa), Shirika la Viwango Tanzania (tozo ya kupima ubora wa mafuta kwenye meli na gharama ya uwekaji wa vinasaba kwenye mafuta).

    Hata hivyo bei mpya ya mafuta iliyoanza kutumika Machi 02, 2022 zikizingatia marekebisho ya kanuni alizoweka waziri wa nishati, January Makamba , imefutwa na rais ingawa hawajasema lini inaanza wala kuisha.

  4. Kwa nini ushirikiano wa Marekani na Urusi unaendelea kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu?

    th

    Chanzo cha picha, Roscosmos

    Licha ya mvutano mkubwa kati ya Urusi na nchi za Magharibi kuhusu Ukraine, mwanaanga wa Marekani na wanaanga wawili wa Urusi wametua salama Kazakhstan wakiwa kwenye chombo kimoja wakisafiri kutoka Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu.

    Kurudi kwa Mwamerika Mark Vande Hei Duniani akiwa katika chombo maalum cha Soyuz cha Urusi pamoja na Warusi hao wawili kunaonyesha kwamba inapofika Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu, ni shughuli kama kawaida.

    Wakati Urusi na Magharibi zimejiondoa katika maeneo mengi ya ushirikiano wa anga - katika misheni ya sayansi ya kinadharia na katika shughuli za usambazaji viwandani - hawana chaguo ila kuendelea kufanya kazi pamoja kwenye ISS.

    Jukwaa la obiti linajumuisha moduli na vipengele kutoka nchi nyingi tofauti, na zote zinategemeana.

    Lakini nguvu nyingi hutoka kwa sehemu ya Marekani, na hakuna kitu kinachofanya kazi bila umeme. Kwa hivyo kila mtu kwenye ISS ameunganishwa na mwingine kwa karibu sana .

  5. BBC yaruhusiwa kuanza tena matangazo nchini Burundi

    th

    Chanzo cha picha, Getty Images

    BBC imeruhusiwa kuendelea na shughuli zake nchini Burundi, miaka mitatu baada ya kupigwa marufuku huko.

    Mamlaka ya Vyombo vya Habari nchini Burundi au Conseil National de la Communication (CNC) imetangaza kwamba wameondoa marufuku ya shughuli za BBC nchini Burundi.

    Tangazo hilo lilitolewa katika mkutano na waandishi wa habari baada ya kikao cha baraza hilo katika mji wa kibiashara wa Burundi Bujumbura.

    BBC ilipigwa marufuku kufanya shughuli zozote nchini Burundi tarehe 29 Machi 2019 na hakuna ripota aliyeruhusiwa kufanya kazi au kushirikiana na vyombo vya habari nchini humo kwa namna yoyote ile.

  6. Daktari wa soka Zambia afariki dunia baada ya mchezo wa Nigeria na Ghana

    Dk. Joseph Kabungo

    Chanzo cha picha, Nkweto Tembwe

    Maelezo ya picha, Dk. Joseph Kabungo alijulikana nchini Zambia kama anayekuwepo wa kudumu kwenye mechi za soka

    Mmoja wa madaktari bingwa wa Zambia amefariki dunia baada ya mchezo wa Nigeria dhidi ya Ghana wa kufuzu Kombe la Dunia Jumanne usiku, wakati mashabiki wa Nigeria walipoanza kuwashambulia wachezaji na wafanyakazi wa Ghana uwanjani na kusababisha tafrani au mkanyagano.

    Haijabainika jinsi Dk. Joseph Kabungo alivyofariki - kuna baadhi ya ripoti kwamba alipatwa na mshtuko wa moyo.

    Alikuwa mmoja wa madaktari wa mechi hiyo mjini Abuja wakati Nigeria ilipotoka sare na wapinzani wao 1-1, na kupelekea Ghana kufuzu kulingana na sheria ya bao la ugenini.

    Matukio mabaya yalifuata baada ya mashabiki wa Super Eagles waliokuwa na hasira kushambulia timu pinzani kwa chupa za maji zilizorushwa kutoka jukwaani walipokuwa wakiondoka uwanjani, huku polisi wakiripotiwa kutumia vitoa machozi kuwatawanya umati huo.

    Mamlaka ya Nigeria bado haijasema lolote hadharani kuhusu tukio hilo.

    Daktari huyo alikuwa mchezaji wa kudumu katika mechi kuu za soka, ikiwa ni pamoja na Kombe la hivi karibuni la Fifa Arab Cup nchini Qatar na Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Cameroon.

    Kifo chake ambacho hakikutarajiwa kimewaacha wadau wa soka wa Zambia katika huzuni.

    “Tunatuma rambirambi zetu za dhati kwa familia ya Dk. Kabungo na familia ya soka kwa ujumla,” rais wa FA wa Zambia Andrew Kamanga alisema katika taarifa yake kuthibitisha kifo hicho.

    Gwiji wa soka wa Zambia Kalusha Bwalya, ambaye alikuwa marafiki wa karibu na Bw Kabungo alishtuka, akiambia BBC kuwa haamini habari hizo.

    Dk. Kabungo alikuwa daktari wa timu ya taifa wakati nchi hiyo ya kusini mwa Afrika iliponyanyua taji lao la kihistoria la Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2012.

    Pia alikuwa sehemu ya kamati ya matibabu ya Fifa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) wakati wa kifo chake.

  7. Kupotea kwa lazima na mauaji nchini Kenya yafichuliwa na Ripoti ya Amnesty International

    th

    Watu 33 walitoweka na wengine 167 waliuawa kinyume cha sheria wakiwemo wale waliokamatwa kwa kukiuka sheria za Covid19 nchini Kenya.

    Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Amnesty International ya mwaka 2021-2022.

    Shirika hilo la haki za binadamu linadai kuwa polisi walitumia na katika visa fulani nguvu kuua katika kuvunja maandamano katika kipindi hicho.

  8. Tanzania:Deni la serikali laongezeka kwa asilimia 13.7 hadi Shilingi trilioni 64.52

    th

    Chanzo cha picha, Ikulu/Tanzania

    Deni la Serikali Tanzania limeongezeka kutoka Sh56.76 trilioni mwaka uliopita hadi kufikia Sh64.52 trilioni kufikia Juni 30, 2021.

    Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere ameyasema hayo leo wakati akiwasilisha ripoti ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2021 kwa Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu Chamwino.

    Kichere amesema ongezeko hilo la Sh7.76 trilioni ni sawa na asilimia 13.7.

    Hata hivyo, amesema kipimo cha deni la Serikali kinachotumia pato la Taifa, kinaonyesha deni hili bado ni himilivu.

  9. Mke bado yupo gizani miezi baada ya mumewe kutekwa nyara Kenya

    Milen Mezgebo
    Maelezo ya picha, Milen Mezgebo anasema polisi hawajamjulisha kuhusu uchunguzi huo

    Miezi minne baada ya kutekwa nyara katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, mfanyabiashara tajiri Samson Teklemichae, familia yake bado inasubiri majibu kuhusu kile kilichompata.

    Novemba mwaka jana, video zilizosambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii, zilionekana kuonyesha raia huyo wa Ethiopia akitekwa nyara mchana kweupe.

    Katikati ya barabara, nje kidogo ya mji wa kibiashara wa Nairobi, anaonekana akitolewa nje ya gari lake na kuwekwa kwenye gari lingine ambalo linaondoka kwa kasi ya ajabu.

    Bado hakuna anayejua Bwana Samson yuko wapi

    Mkewe, Milen Mezgebo, amechanganyikiwa.

    Anasema tukio hilo liliishangaza familia na watoto wake wanaoendelea kuuliza maswali ambayo hawezi kuyajibu.

    “Watoto wangu wanateswa kila siku ... wameona video,” aliambia BBC.

    Anasema kuwa muda pekee ambao amezungumza na polisi ni pale alipokwenda kutoa taarifa kuhusu kutoweka kwa mumewe.

    Tangu wakati huo hajasikia chochote kutoka kwa mamlaka.

    Bw. Samson, anayetoka eneo la kaskazini mwa Ethiopia la Tigray, alipata pesa zake kwa kuendesha biashara ya mafuta ya kimiminikaya petroli.

    Ameishi Kenya na familia yake kwa miaka 17 iliyopita.

    Serikali ya Ethiopia imetoa wito kwa Kenya kuharakisha uchunguzi kuhusu aliko.Balozi wake nchini Kenya, Meles Alem, anasema serikali ya Kenya imewaambia polisi wanafanya uchunguzi lakini haikutoa maelezo yoyote.

    Serikali ya Kenya haijajibu ombi la BBC la kutaka maoni yake.

    Samson Teklemichael amekuwa akiishi nchini Kenya kwa miaka 17

    Chanzo cha picha, Family of Samson Teklemichael

    Maelezo ya picha, Samson Teklemichael amekuwa akiishi nchini Kenya kwa miaka 17

    Chanzo cha utekaji nyara huo bado ni kitendawili.

    Ikizingatiwa kuwa Bw. Samson anatoka Tigray, baadhi walidhani kwamba huenda chimbuko la hayo yote ni vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

    Wengine wameelekeza polisi wa Kenya, ambayo imekuwa ikilaumiwa kwa makumi ya watu kupotea katika miaka ya hivi karibuni.

    Lakini msemaji wa polisi Bruno Shioso anapuuza uvumi huu.

    “Tupo kulinda maisha ya watu, ya raia, na watu wengine wowote ambao wanaweza kuwa ndani ya eneo letu,” aliambia BBC.

    “Tuna wahalifu ambao wanafanya kazi sana, wana mbinu, kwa hivyo sio polisi, na haipaswi kuwa polisi.”

    Afisa wa polisi wa trafiki anaweza kuonekana kwenye video ya Bw. Samson akichukuliwa.

    Bw. Shioso anakiri kwamba alikuwa polisi lakini anasema alikuwa nje ya kazi rasmi na alisimama tu “ili kuuliza ghasia hizo zilihusu nini.”

    Anasema afisa wa polisi “hakuwa katika eneo la tukio kusaidia au kukamata”.

  10. Crimea ni sehemu ya Urusi na hakuna majadiliano kuhusu hilo- Kremlin

    th

    Msemaji wa Moscow Dmitry Peskov anasema Urusi iko makini kutoa maoni yake kuhusu mazungumzo ya hapo jana kwani "tunaamini kwamba mazungumzo yanapaswa kufanyika kimyakimya" lakini anasema mpatanishi mkuu wa Urusi atazungumza baadaye.

    Anaongeza kuwa Crimea, eneo lililotwaliwa na Urusi mwaka 2014, ni "sehemu ya Urusi" na katiba ya Urusi ilizuia kujadili hatima ya eneo lolote la Urusi na mtu mwingine yeyote.

    Mazungumzo ya amani hayakutoa mafanikio yoyote - Urusi

    Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amekuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu mazungumzo hayo yaliyofanyika na Ukraine nchini Uturuki hapo jana, na kupunguza matumaini yoyote ya kufanikiwa.

    Hapo jana, Urusi ilisema inakusudia kupunguza shughuli zake za kijeshi huko Kyiv na Chernihiv, na Ukraine ikasema itazingatia kuwa taifa lisiloegemea upande wowote.

    "Kilicho chanya ni kwamba upande wa Ukraine angalau umeanza kutunga na kuweka kwenye karatasi kile inachopendekeza. Hadi sasa tulikuwa hatujaweza kufikia hilo," Peskov alisema.

    "Kuhusu mengine, hatuwezi, kuiweka hivi kwamba kwa sasa kumekuwa na mafanikio yoyote, " alisema, katika matamshi yaliyoripotiwa na shirika la habari la Interfax.

  11. Watu kumi na wawili wamefariki katika shambulio: Gavana wa Mykolaiv

    Waokoaji wanafanya kazi kwenye eneo la jengo la utawala wa kikanda lililopigwa makombora na Urusi huko Mykolaiv

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Waokoaji wanafanya kazi kwenye eneo la jengo la utawala wa kikanda lililopigwa makombora na Urusi huko Mykolaiv

    Shambulio la Urusi dhidi ya jengo la serikali katika mji wa bandari wa Mykolaiv kusini mwa Ukraine jana limesababisha vifo vya watu 12 na kuwajeruhi karibu wengine 30, maafisa wa Ukraine wamesema.

    Meya wa Mykolaiv, Oleksandr Senkevych aliiambia BBC hakukuwa na wanajeshi katika jengo hilo, "kulikuwa na walinzi tu ... watu wengine wote walikuwa wafanyikazi wa ofisi tu".

    Senkevych anafikiri kwamba vikosi vya Urusi huenda vilikuwa vinajaribu kumlenga gavana wa eneo Vitaliy Kim, ambaye hakuwepo wakati huo.

    Anasema: "Shughuli zake za vyombo vya habari, kwa hakika, [hazisaidii Warusi katika malengo ya wanajeshi wao kwa hivyo nadhani kulikuwa na shambulio kwake."

    Soma zaidi:

  12. Kupunguza mashambulizi dhidi ya Kyiv ni ujanja wa 'kujipanga upya', asema mshauri wa zamani wa usalama wa Ukraine

    th

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Oleksander Danylyuk, mshauri wa zamani wa usalama wa taifa rais wa Ukraine Rais Volodymyr Zelensky, anasema haamini ahadi ya Urusi ya kupunguza operesheni za kijeshi karibu na Kyiv na Chernihiv.

    Anasema sauti ya makombora asubuhi ya leo imethibitisha hofu yake.

    Wakati hakuna ongezeko na baadhi ya askari wamehama kutoka Kyiv, "huku ni kujipanga upya", anasema.

    Urusi tayari imeelekeza upya kampeni yake katika maeneo ya mashariki mwa Ukraine baada ya kukumbwa na msururu wa vikwazo kaskazini mwa mji mkuu.

    Danylyuk anaamini Urusi itaweka juhudi zake zote katika kuchukua Donetsk na Luhansk, mashariki, kwani Vladimir Putin anahitaji kuonyesha ushindi.

    Lakini anasema Urusi "haitapunguza unyakuzi wao" kwa Kyiv na Chernihiv - "haya ni maneno tu".

    Anasema Urusi imependekeza kupunguzwa kwa maeneo hayo lakini anasema hapa ndipo wanajeshi wa Ukraine walikuwa tayari wanasonga mbele kuyachukua tena maeneo hayo.

    "Kwa hivyo sasa ikiwa tutaendelea tu kuikomboa miji iliyo karibu na Kyiv, Urusi itatushtaki kwa kufanya kazi dhidi ya kushuka kwa kasi," anasema.

    "Kama kawaida kuna michezo ya kijeshi na kidiplomasia ya KGB yote kwa pamoja, huu ni mchezo mmoja," anaongeza.

    Mengi zaidi

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
    • SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine
  13. 'Mwanajeshi wa Urusi alinifyatulia risasi kutoka kwa bunduki yake ya kumimina risasi'

    Natalia alipata majeraha yaliyobadilisha maisha baada ya kupigwa risasi mara kadhaa
    Maelezo ya picha, Natalia alipata majeraha yaliyobadilisha maisha baada ya kupigwa risasi mara kadhaa

    Urusi inasema hailengi raia - majengo wanamoishi na kufanya kazi, au watu wenyewe.

    Akiwa amelazwa katika kitanda cha hospitali katika mji wa kusini mwa Ukraine wa Zaporizhzhia, Natalia Mykolaivna anadhihaki kukanusha huko kwa Warusi.

    Kilichomtokea Natalia mwenye umri wa miaka 45 kilikuwa cha makusudi, kilicholengwa na bila uhalali.

    Ni muujiza kwamba bado yuko hai.

    Akiwa ameshika mkono unaomfariji wa mwanawe, Nikolai, alisimulia yaliyotukia katika mji wa kwao wa Polohy siku ambayo majeshi ya Urusi yalipowasili.

    “Nilitoka nyumbani kwangu, nilikuwa na wasiwasi na mama yangu mzazi, hivyo nikaenda kumuona,” alisema Natalia, ambaye alieleza jinsi alivyoruhusiwa kupita kwenye kizuizi cha jeshi la Urusi.

    “Kisha nilitembea kuelekea nyumbani kwa mama yangu, nikainua mikono yangu juu hewani - nikisema tayari nimeambiwa naweza kupita - lakini mwanajeshi huyo alifyatua risasi kutoka kwa bunduki yake ya kumimina risasi, ikanipiga miguuni, kila mahali kutoka kiunoni kwenda chini.”

    Natalia alihamishwa na majirani na familia yake hadi hospitali iliyo karibu na Zaporizhzhia na tangu wakati huo ameambiwa na madaktari kwamba alinusurika ‘kifo kwa milimita moja.’

  14. Mamake Will Smith: 'Hiyo ndiyo mara yangu ya kwanza kumwona akiwa na hasira hivyo'

    Will Smith akiwa na mkewe

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Will Smith akiwa na mkewe

    Carolyn Smith, mamake Will Smith, amesema walikuwa wamekusanyika pamoja na familia nyumbani kwake viungani mwa Philadelphia Jumapili usiku, akifurahi kumtazama mwanawe kwenye tuzo za Academy.

    Alikuwa na furaha kupindukia baada ya mwanawe mwigizaji kupata tuzo yake ya kwanza ya Oscar lakini alishtushka baada ya kumuona Will Smith akimpiga mchekeshaji Chris Rock.

    "Yeye ni mtu mwenye anayependa usawa," alisema.

    "Ndiyo mara ya kwanza nimewahi kumuona akiwa na hasira kiasi hiki. Mara ya kwanza katika maisha yake."

    Nyota huyo aligonga mwamba baada ya kufanya mzaha kuhusu mke wa Smith, Jada Pinkett Smith aliyenyolewa kichwa.

    Ellen Smith, dadake Will Smith, alizungumza na kituo hicho kuhusu shinikizo analopitia kaka yake kama mtu mashuhuri.

    "Kila mtu ameonewa au kunyanyaswa kwa namna fulani," alisema. Ninaelewa kabisa."

    Carolyn Smith alisema ushindi wa mwanawe siku ya Jumapili ulikuwa kilele cha miaka ya matumaini na bidii ya mwigizaji huyo.

    "Nimekuwa nikingoja na kusubiri na kusubiri, alisema. Niliposikia jina, nilikuwa tu nasema, Ndiyo!"

    Soma zaidi:

  15. Milio ya makambora yasikika kwenye ukingo wa Kyiv

    Vikosi vya Ukraine (juu) na waasi wanaoiunga mkono Urusi wameanza kuvuta vifaru vyao

    Chanzo cha picha, AP

    Milipuko imesikika karibu na Kyiv tena asubuhi ya leo.

    Mwandishi wetu mkuu wa kimataifa Lyse Doucet alisema siku ilianza kwa vilio vya vingora vya mashambulizi ya anga, na kufuatiwa na mirindimo mikubwa kutoka nje ya jiji ambayo angeweza kuhisi katikati mwa mji mkuu.

    Na Jeremy Bowen, ambaye pia yuko Kyiv, alituma ujumbe kwenye Twitter kwamba "sauti nyingi za mizinga zilikuwa zikivuma kutoka ukingo wa jiji hadi katikati".

    Haijulikani ikiwa milipuko hiyo ni ya Urusi au ya Ukraine au zote mbili, alisema.

    Jana, kufuatia mazungumzo, Urusi ilisema inakusudia kupunguza shughuli karibu na mji mkuu - ahadi ambayo viongozi wengi wa magharibi walisema inapaswa kushughulikiwa kwa tahadhari.

    Soma zaidi:

  16. Kura ya kutokuwa na imani na Baraza za Mawaziri Afrika Kusini kupigwa

    Kura ya kwanza ya kutokuwa na imani dhidi ya Baraza la Mawaziri la rais wa Afrika Kusini Ramaphosa itafanyika leo mchana bungeni.

    Chama cha upinzani, Democratic Alliance (DA), kilitoa wito wa kura ya kutokuwa na imani dhidi ya baraza lake la mawaziri.

    Chama cha African Transformation Movement (ATM) kilipendekeza kupigiwa kura ya kutokuwa na imani na Ramaphosa mwenyewe.

    Ombi lao awali lilikuwa lipigiwe kura ya siri, Spika wa Bunge aliridhia kwa sharti kwamba lifanyike kwa utaratibu wa majina ya Wabunge (ambapo majina ya wabunge yanasomwa na kutamka "ndiyo" au "hapana").

  17. Urusi yaendeleza 'vitendo haramu' dhidi ya wenyeji - Ukraine

    Rais wa Urusi Vladimir Putin

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Rais wa Urusi Vladimir Putin

    Vikosi vya jeshi la Ukraine vimesema katika matukio ya kila siku kwamba wanajeshi wa Urusi wanaendelea "kufanya vitendo visivyo halali" dhidi ya wakaazi wa eneo la Zaporizhzhia kusini-mashariki mwa Ukraine, na Kherson kusini.

    BBC haijaweza kuthibitisha madai hayo lakini vikosi vya Ukraine vilisema kuwa:

    • Urusi inaendelea kupeleka wanajeshi Ukraine

    • Vikosi vya Urusi vinaendelea kuvamia nyumba za wakaazi wa eneo hilo, kuwaweka kizuizini wanaharakati wanaounga mkono Ukrainian na maafisa wa serikali

    Taarifa hiyo inawadia kufuatia ya ahadi ya Urusi katika mazungumzo ya amani mjini Istanbul siku ya Jumanne "kupunguza kwa kiasi kikubwa" operesheni za kijeshi karibu na Kyiv.

    Soma zaidi:

  18. DR Congo: Waasi wa M23 wakanusha kuidungua helikopta ya Umoja wa Mataifa

    Umusirikare wa Republika Iharanira Demokrasi ya Kongo, mu gihe c'imirwano n'abarwanyi b'umugwi ADF Nalu mu kwezi kwa mbere 2018

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Waasi wa M23 wakanusha kudungua helikopta ya walinda amani wa UN

    Waasi wa M23 wamekanusha madai kwamba wamedungua helikopta ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa ambayo ilitoweka katika eneo la vita kati yao na majeshi ya DR Congo,FARDC.

    “Ndege hiyo iligongwa na silaha za FARDC.” Msemaji wa M23 Meja Jenerali Willy Ngoma ameambia BBC Great Lakes.

    Katika taarifa Jumanne usiku, waasi hao wanaongeza kuwa wakati jeshi la kifalme lilipokuwa likishambulia eneo lao kombora iliigonga ndege ya walinda amani iliyokuwa na watu wanane.

    Vikosi vya jeshi la Pakistan viliomboleza kifo cha walinda amani wake sita waliokuwa kwenye mpaka. Katika Twitter, waziri wake wa habari Fawad Hussain aliwaita wanajeshi walioaga dunia "mioyo ya ujasiri".

    Mapigano ya waasi na jeshi la kifalme yaliyozuka alfajiri ya Jumatatu yamesababisha zaidi ya raia 6,000 kukimbia makazi yao katika eneo la Rutshuru mkoani Kivu Kaskazini, shirika la Msalaba Mwekundu limesema.

  19. Jada Pinkett Smith avunja ukimya juu ya kibao cha Oscar

    Will Smith na Jada Pinkett Smith katika sherehe ya Vanity Fair Oscars siku ya Jumapili

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Jada Pinkett Smith amevunja ukimya baada ya mumewe kukosolewa kwa kumpiga kibao mchekeshaji Chris Rock kwa kufanya mzaha juu yake.

    Katika chapisho fupi kwa Instagram, mwigizaji huyo aliandika juu ya "msimu wa uponyaji" akimaanisha tukio la Oscars.

    Mume wake, Will Smith, alilaaniwa na waandaji wa tuzo hizo kwa kumzaka kofi Rock.

    Aliomba msamaha siku ya Jumatatu, akitaja tukio hilo kuwa vurugu "sumu na uharibifu".

    Tukio hilo la Jumapili usiku lilitokea kabla tu ya Smith kushinda tuzo ya Oscar ya Muigizaji Bora, wakati mchekeshaji Rock alipokuwa jukwaani kutoa tuzo ya Makala Bora.

    Alifanya mzaha kuhusu kichwa kilichonyolewa cha Pinkett Smith, iliyotokana na ya hali ya upotezaji wa nywele alopecia.

    Pinkett Smith hakutoa maoni yake huku kukiwa na mzozo mkali na mjadala wa hadharani uliofuata kuhusu utani wa Rock na vitendo vya Smith hadi Jumanne, akichapisha kwenye Instagram: "Huu ni msimu wa uponyaji na niko hapa kwa ajili yake".

    Rock bado hajatoa maoni yake hadharani juu ya kile kilichotokea kwenye tuzo za Oscar au msamaha wa Smith.

    Hata hivyo, tikiti za maonyesho yake yajayo ya vichekesho zimeripotiwa kupanda kufuatia tukio la Jumapili.

  20. Wanajeshi wanane wa kulinda amani wa UN wathibitishwa kupoteza maisha DRC

    Wanajeshi wa kulinda amani

    Chanzo cha picha, AFP

    Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo limesema waasi wameiangusha helikopta ya Umoja wa Mataifa mashariki mwa nchi hiyo.

    Takriban watu wanane walikuwa kwenye ndege hiyo iliyodunguliwa wilayani Rutshuru katika jimbo la Kivu Kaskazini.

    Sita kati ya waliofariki walikuwa wanajeshi kutoka Pakistan. Jeshi la Congo limesema helikopta hiyo ilidunguliwa na wasi.

    Ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa umesema helikopta yake moja ilitoweka katika eneo la Chanzu, ambalo lilishambuliwa na wapiganaji wa kundi la M23 Jumapili usiku.

    Shirika la Msalaba Mwekundu linasema takriban watu elfu sita wamekimbilia nchi jirani ya Uganda ambapo wanapelekwa kwenye kambi ya wakimbizi.

    Idara ya Operesheni za Amani ya Umoja wa Mataifa ilithibitisha kupoteza kwa askari wanane wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, kufuatia ajali ya helikopta yao Jumanne hii, katika Mkoa wa Kivu Kaskazini.

    Miongoni mwa waliofariki waliokuwa ndani ya ndege hiyo, wafanyakazi sita kutoka Pakistani na wafanyakazi wawili wa kijeshi, mtawalia kutoka Urusi na Serbia.

    Mapema leo, Vikosi vya Wanajeshi vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vilishutumu kundi la waasi kwa kuiangusha helikopta ya Umoja wa Mataifa.

    Jenerali Sylvain Ekenge, Msemaji wa serikali ya Kivu Kaskazini aliviambia vyombo vya habari kwamba waasi wa M23 waliiangusha helikopta ya MONUSCO ilipokuwa ikiruka juu ya maeneo yanayodhibitiwa na M23, kwa misheni isiyo na hatia iliyolenga kuwasaidia waathiriwa wa mashambulio ya hivi majuzi.

    Katika taarifa yake, leo, msemaji wa M23, Meja Willy Ngoma amelilaumu jeshi la DRC kwa kufanya mashambulizi dhidi ya nafasi zao, akisema walijibu ili kujilinda. Mapigano yalizuka kati ya jeshi la kawaida la DRC na M23 tangu mapema Jumatatu.

    Unaweza kusoma zaidi;