Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Milipuko Uganda: Sita wauawa wakiwemo washambuliaji watatu
Mmoja ulitokea karibu na kituo kikuu cha polisi ambacho pia kiko karibu na bunge.
Moja kwa moja
Ambia Hirsi
Habari za hivi punde, Kenya yawekwa katika hali ya tahadhari kufuatia milipuko Uganda
Kenya imewekwa katika hali ya tahadhari kufuatia milipuko miwili iliopiga mji wa Kampalanchini Uganda mapema siku ya Jumanne.
Shirika la huduma ya kitaifa ya maafisa wa polisi nchini Kenya NPS limesema kwamba usalama umeimarishwa katika maeneo yotena mijini nchini pamoja na mipakani .
Raia wametakiwa kuwa chonjo na kuripoti vitendo vyovyote visivyo vya kawaidakatika vituo vilivyopo karibu vya polisi ama kwa kutumia nambari ya dharura ya 999/112.
‘’Huduma ya polisi ya NPSinawahakikishia raia kuhusu usalama wao kufuatia matukio ya ugaidi katika taifa jirani mapema asubuhi. Huruma zetu ziwafakie waathiriwa na familia ambazo ziliathiriwa na tukio hilo la kikatili’’, NPS ilichapisha ujumbe wao wa Twitter.
Milipuko hiyo ilitokea katika tofauti ya dakika chache, huku mmoja ukipiga katika kituo cha polisi mwendo wa saa nne na nusu na kuwaua watu wawili na kujeruhi watu wengine 17 alisema msemaji wa polisi Fred Enanga .
Mlipuko wa pili ambao ulimuua mtu mmoja na kuwajeruhi 16 ulitokea karibu ma majengoi ya bunge mwendo wa saa nne na dakika sita .
Tanzania na Uingereza zajadili namna ya kushirikiana kibiashara,
Serikali ya Uingereza imesema kuna kila sababu ya kuhakikisha kuwa uwekezaji unafanyika nchini Tanzania ili kunufaisha mataifa yote mawili.
Mwakilishi wa Waziri Mkuu wa Uingereza aliyeongoza ujumbe wa Wafanyabiashara wa taifa hilo, Lord Walney ameyasema hayo leo wakati akihutubia kwenye mkutano wa biashara kati ya Tanzania na Uingereza uliofanyika katika Mji wa Kibiashara wa Dar es Salaam.
Walney amesema kuwa kuna kila sababu ya Tanzania na Uingereza kujadili namna ya kukubaliana kwenye mustakabali wa ushirikiano kwenye masuala mbalimbali ikiwemo kilimo, miundombinu, madini na uchumi wa blu.
Amesema, “Kuna utajiri mkubwa Tanzania, Leo mataifa yetu yamekutana kujadiliana kuhusu biashara na fursa mbalimbali zilizopo kwenye mataifa yetu. “ Vile vile kuna fursa nyingi na za kuvutia kwenye kilimo, miundombinu, madini na uchumi wa blu,” alieleza Walney.
Waziri Mkuu nchini Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zipo tayari kuwapokea, kuwasikiliza na kushirikiana na wawekezaji kutoka Uingereza ili kuimarisha shughuli za uwekezaji na biashara nchini Tanzania.
Majaliwa amesema Uingereza imeendelea kuwa mshirika wa asili, wa kihistoria na wa muda mrefu wa kibiashara wa Tanzania na kwamba uhusiano huu unajipambanua na uwepo wa fursa nyingi za biashara na uwekezaji ambazo hazijaweza kutumika ipasavyo.
Misri: Kaburi la binti wa Farao lapatikana
Kaburi lililopatikana nchini Misri linasemekana kuwa lilimzika binti wa Farao, miaka 3,700 hivi iliyopita, na inaaminika kwamba mabaki hayo yalikuwa ya binti ya Farao.
Mabaki hayo yalipatikana katika piramidi za Misri..
Wizara ya masuala ya kale nchini Misri imesema mabaki hayo yalikuwa katika piramidi za kale za Dahshur , walikuta sanduku la mbao lenye maandishi mbalimbali.
Ndani ya sanduku hilo kulikuwa na chombo kidogo kilichojaa nyama za binadamu, ikiaminika kuwa ni mwili wa mwanamke anayedhaniwa kuwa ni binti wa mfalme mmoja wa farao wa Misri, Emnikamaw.
Mtaalamu mmoja wa historia walipata tovuti ambayo iliandika maana ya jina hilo la Emnikamaw.
- Misri ya Kale: Mafarao walizikwa pamoja na wahudumu wao wakiwa hai kama kafara ya maisha ya baadaye
Wanawake wawili wamshtumu baba yake Waziri Mkuu wa Uingereza kuwagusa vibaya bila ridhaa yao
Wanawake wawili akiwemo mbunge wa chama cha Conservative wamemshutumu baba yake waziri mkuu wa Uingereza, Stanley Johnson kwa kuwagusa isivyostahili.
Caroline Nokes ameiambia Sky News kuwa bwana Johnson alimshika kwa nyuma kwa nguvu wakati wa mkutano wa chama cha Tory mwaka 2003.
Na mwandishi wa siasa Ailbhe Rea anamshutumu bwana Johnson kwa kumpapasa bila ridhaa yake katika mkutano wa chama cha Conservative mwaka 2019.
Bwana Johnson ameiambia Sky kuwa hakumbuki kufanya jambo kama hilo kwa bi. Nokes.
Bi Nokes, Mbunge wa Romsey na Southampton North tangu mwaka 2010, alikuwa mgombea wa chama cha Conservative wakati tukio hilo lilipotokea katika mkutano wa mwaka 2003 huko Blackpool.
Milipuko Uganda: Polisi wanasema nini juu ya milipuko hiyo
Polisi nchini Uganda wamekuwa wakitoa maelezo juu ya mashambulio la asubuhi jijini Kampala:
- Watu sita waliuawa kwa jumla wakiwemo washambuliaji watatu wa kujitoa mhanga
- Mshambulizi wa nne alikamatwa
- Watu 33 wanatibiwa hospitalini huku watano wakiwa katika hali mbaya
- Mlipuko mmoja ulitokea karibu na kituo kikuu cha polisi, mwingine karibu na bunge
- Shambulio hilo karibu na kituo cha polisi lilitekelezwa na mlipuaji wa kujitoa mhanga akiwa peke yake. Mlipuko huo pia uliua watu wengine wawili
- Washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga wakiwa kwenye pikipiki walifanya shambulio la pili ambalo lilimuua mtu mwingine mmoja
- Polisi wanasema kundi la wanamgambo wa Uganda la Allied Democratic Forces ndilo lililohusika na mashambulizi hayo.
Milipuko Uganda: Vitisho vya mabomu bado vinaendelea - polisi
Msemaji wa polisi nchini Uganda amewataka raia wote wa Uganda kuwa makini.
"Vitisho vya mabomu bado vinaendelea, haswa kutoka kwa washambuliaji wa kujitoa mhanga, Fred Enanga aliwaambia waandishi wa habari.
"Tunaamini bado kuna wanachama zaidi wa makundi ya ugaidi wa ndani, haswa wale wa kitengo cha mabomu ya kujitoa mhanga ambacho kimebuniwa na ADF [Allied Democratic Forces]. Na hii inahitaji umakini wa jamii. Kwa kweli tunahitaji kuwa macho sana
"Mbinu ya kushambulia kwa kutumia mabomu wanayotumia ndio mkakati wao ya hivi punde ya mashambulizi."
Jeshi la Nigeria 'liliwapiga risasi na kuwaua waandamanaji wa #EndSars': ripoti
Jopo la uchunguzi, lililoundwa na mamlaka nchini Nigeria kuchunguza tukio la waandamanaji kupigwa risasi mjini Lagos mnamo Oktoba 2020, limewasilisha ripoti juu ya kile kilichokea usiku huo.
Toleo lililovuja la ripoti hiyo, iliyokabidhiwa kwa gavana wa jimbo hilo leo, inadai kuwa wanajeshi wa Nigeria waliwapiga risasi kimakusudi waandamanaji waliokuwa wakipinga ukatili wa polisi kwenye barabara ya Lekki Tollgate, kisha wakajaribu kuificha.
Waandamanaji hao walikuwa wakiendesha kampeni dhidi ya ukatili wa polisi.
Pia ilibaini kuwa baada ya jeshi hilo kurudi nyuma, askari polisi waliendelea na vurugu na kujaribu kufanya usafi katika eneo la tukio na kuweka miili kwenye lori na kutoa risasi.
Baadhi ya matokeo yanalingana na ripoti za awali za Amnesty International, pamoja na vyombo vya habari vya ndani na kimataifa.
Gavana wa Jimbo la Lagos Babajide Sanwo-Olu, ambaye alianzisha jopo hilo, ameahidi "kutilia maanani" matokeo yake.
- Kampeni ya End Sars: Jinsi maandamano dhidi ya ukatili wa polisi yalivyoenea duniani
- Kwanini kikosi cha Sars kinachukiwa Nigeria?
Milipuko Uganda: Sita wauawa wakiwemo washambuliaji watatu
Watu sita wameuawa wakiwemo watatu waliohusika katika shambulio hilo lililotokea majira ya asubuhi katika mji mkuu wa Uganda, Kampala.
Msemaji wa polisi Fred Enanga amesema taarifa za kiintelijensia zinaonesha kuwa wahusika wa mashambulio hayo ni wanamgambo wa Allied Democratic Forces (ADF).
Alisema mshambuliaji wa nne alifuatwa na kuekwa kizuizini na polisi walipata koti lenye bombu la kujitoa mhanga nyumbani kwake.
Bw Enanga aliongeza kuwa watu 33 walijeruhiwa na watano kati yao wako katika hali mbaya. ADF ilidai moja ya milipuko miwili mjini Kampala mwezi uliopita.
Mashambulio hayo mawili yalifanyika katika tofauti ya dakika 3 asubuhi ya leo katika kituo cha polisi cha kukagua magari karibu na kituo cha polisi cha central na mwengine ukatokea katika barabara ya bunge inayopita karibu na bunge la taifa hilo.
Haftar atangaza kuwania urais Libya
Jenerali wa Libya, Khalifa Haftar, ambaye jeshi lake liko mashariki mwa nchi hiyo, ametangaza kuwa ana nia ya kugombea urais katika uchaguzi utakaofanyika mwezi ujao.
Katika hotuba yake kwa njia ya televisheni, Jenerali Haftar amesema uchaguzi ndio njia pekee ya kutoka katika mgogoro mkubwa wa Libya.
Mwendesha mashtaka wa kijeshi, Mohamed Gharouda, tayari amewataka wasimamizi wa uchaguzi kukataa uwezekano wa Jenerali Haftar kugombea, kwa sababu ya mashambulizi aliyoanzisha dhidi ya mji mkuu wa Tripoli mwaka 2019.
- Mwanawe Gaddafi atangaza nia ya kutaka kuongoza Libya
Watu wanne waliuawa katika milipuko Uganda - ripoti
Watu wanne, miongoni mwao maafisa wawili wa polisi, wameuawa katika milipuko miwili tofauti katika mji mkuu wa Uganda, Kampala, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti.
Tovuti inayomilikiwa na serikali ya New Vision ilisema kuwa miili miwili imepatikana katika eneo la mlipuko karibu na jengo la bunge.
"Miili miwili imepatikana baada ya mlipuko katika barabara ya Bunge katikati mwa Kampala," ilisema.
Televisheni ya kibinafsi ya Urban inasema kwamba maafisa wawili wa polisi walithibitishwa kuuawa katika shambulio tofauti,lililolenga kituo kikuu cha polisi katika mji mkuu.
Tovuti ya Independent inasema hospitali kuu mjini Kampala imezidiwa na idadi ya waathiriwa wa milipuko hiyo miwili.
Milipuko hiyo miwili inafuatia shambulio la bomu la Oktoba 23 katika mgahawa mmoja mjini Kampala, ambapo mtu mmoja aliuawa.
Kundi linalojiita Islamic State baadaye lilidai kufanya shambulizi hilo.
Mume wake Agnes Tirop afunguliwa mashtaka ya mauaji
Mahakama ya Kenya imemshtaki mume wa mwanariadha wa Kenya Agnes Tirop kwa mauaji.
Ibrahim Rotich hatahivyo amekana kutekeleza mauaji hayo.
Mashtaka yaliwasilishwa wiki moja baada ya mshukiwa kuagizwa kufanyiwa uchunguzi wa afya ya akili yake.
Agnes Tirop – mwanariadha wa mbio za masafa marefu aliyevunja rekodialipatikana amefariki nyumbani kwake huko mjini Iten mkoa wa bonde la Ufa baada ya kudungwa kisu mwezi uliopita.
Habari za hivi punde, Askari wa gereza wakamatwa kufuatia kutoroka kwa wafungwa
Serikali ya Kenya inasema kwamba vitengo vya usalama viko katika hali ya tahadhari kufuatia kutoroka kwa wafungwa watatu waliopatikana na hatia ya kuwa magaidi kutoka kwa jela inayolindwa zaidi nchini Kenya.
Mmoja ya waliotoroka alihukumiwa kwa shambulio la 2015 katika chuo kikuu cha Garissa ambapo takriban watu 150 waliuawa.
Mwengine alikuwa amepatikana na hatia kwa jaribio lililotibuliwa la bunge la Kenya , na mwengine wa tatu kwa kuvuka Somalia kujiunga na al-Shabab.
Vitengo vya usalama vimeimarisha usalama katika mipaka ya Kenya huku Askari jela saba wakikamatwa.
Maafisa wa upelelezi wanachunguza jinsi watu wanaotajwa kuwa hatari zaidi wanaweza kutoroka katika jela ya kamiti – jela inayolindwa zaidi nchiniambayo ipo kilomita 20 Kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa Nairobi.
Katika taarifa, waziri masuala ya ndani Fred Matiangi alisema kwamba wachunguzi wanachunguza iwapo wafungwa hao walitoroka kutokana na uzembe au ulegevu wa maafisa . Tayari serikali imetoa zawadi ya
$550,000 (£408,000) iwapo mtu yeyote atawajulisha polisi walipo .
Malala Yousafzai: "Sikuelewa ndoa hadi nilipoingia kwenye chumba cha mume wangu"
Chini ya wiki moja baada ya ndoa yake, mwanaharakati na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Malala Yousafzai amefichua kwamba hapo awali alikuwa haelewi ndoa, kulingana na Vogue. Uingereza.
Katika mahojiano na mwandishi wa BBC Andrew Marr, Mpakistani huyo mwenye umri wa miaka 24 anasema "ana wasiwasi sana" na masaibu wanayopitia wasichana katika sehemu mbalimbali za dunia.
Mtangazaji huyo alianza kwa kumpongeza Malala kwa kufunga ndoa wiki iliyopita, kisha akamuuliza ni kitu gani kilimbadilisha kuhusu ndoa, japo awali alipinga?
Malala alinyamaza na kusema; "Sipingi ndoa. Usawa kati ya mume na mke ni muhimu sana kwangu.
Na jukumu la utamaduni kwa wanawake ambao wanajikuta katika hali kama hiyo pia linafaa kuzingatiwa. "
Lakini Malala anasema sivyo, kwani anasema “ana bahati sana” kuwa na mwenzi wa maisha (mume) anayemuelewa na anajiamini kuwa anaweza kuendeleza mapambano yake ya kupigania haki za wasichana.
Malala aliwahi kupinga ndoa katika mahojiano na Vogue mwezi Julai, alisisitiza kuwa; "Bado sielewi kwa nini watu wanaolewa."
"Ikiwa unataka kuishi na mtu, kwa nini unapaswa kusaini mahali, kwa nini musiishi kama marafiki? Mama yangu wakati mmoja alinigombeza, akisema; usiseme tena. "Lazima uolewe. Ndoa ni kitu kizuri."
Habari za harusi yake zimekuwa gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii, haswa Twitter, ambapo maelfu ya watu wamekuwa wakituma salamu za pongezi kwa maharusi hao.
Mwanaharakati huyo mwenye umri wa miaka 24 alitangaza ndoa yake kwenye akaunti yake ya Twitter, akisema yeye na familia yake walifanya sherehe ndogo ya harusi nyumbani kwao huko Birmingham, Uingereza.
Mumewe Asser Mlik ni mchezaji wa kriketi maarufu, ambaye anashikilia wadhifa wa Meneja Mkuu wa Bodi ya Kriketi ya Pakistani (PCB)
Majengo ya bunge la Uganda yakikaguliwa
Maafisa wa usalama wanakagua majengo ya bunge mjini Kampala, Uganda kufuatia milipuko miwili katikati mwa jiji, ambayo moja ililipuka karibu na bunge.
Spika wa Bunge ameahirisha vikao vya leo. Mapema polisi walimwondoa spika na maafisa wengine.
Mwandishi wa habari wa Uganda ametuma video ya mbwa wa kunusa kwenye mtandao wa twitter wakiwa ndani ya majengo ya bunge:
Ubalozi wa Marekani ulikuwa umeonya kuhusu mashambulizi zaidi nchini Uganda
Ubalozi wa Marekani mjini Kampala, Uganda ulikuwa umeonya kuhusu "uwezekano wa mashambulizi zaidi ya kigaidi nchini Uganda", wiki tatu zilizopita.
Onyo hilo lilikuwa katika tahadhari ya usalama ya tarehe 26 Oktoba.
Tahadhari hiyo ilitolewa baada ya milipuko mingine miwili mjini Kampala, ambapo kundi la wanamgambo lilidai kutekeleza.
Ubalozi huo uliwaonya raia wa Marekani wakati huo "kukaa macho na kufahamu mazingira yao wanaposafiri nchini Uganda"
Waathiriwa wa milipuko ya Uganda watibiwa katika hospitali ya Kampala - ripoti
Wodi ya majeruhi ya hospitali kuu katika mji mkuu wa Uganda, Kampala, imejaa watu waliojeruhiwa katika milipuko ya asubuhi, tovuti ya habari ya Independent inaripoti.
Inasema wengi wa waliojeruhiwa ambao walikuwa wameletwa katika Hospitali ya Mulago kwa magari ya wagonjwa ni maafisa wa polisi.
Moja ya milipuko hiyo ilitokea karibu na Kituo Kikuu cha Polisi katika wilaya kuu ya kibiashara ya Kampala.
Kituo cha runinga cha NTV kimezungumza na daktari katika kituo kingine cha afya ambaye alisema walipokea majeruhi 17. Kumi na wawili walishauriwa kwenda Mulago huku wengine watano wakirudishwa nyumbani.
Milipuko Uganda:Polisi watumia mbwa wa kunusa katika maeneo ya milipuko
Polisi nchini Uganda wanatumia mbwa wa kunusa kutafuta ushahidi zaidi na kugundua vilipuzi vyovyote kwenye maeneo ya milipuko katikati mwa mji mkuu, Kampala.
Mmoja ulitokea karibu na kituo kikuu cha polisi ambacho pia kiko karibu na bunge.
Gazeti la Daily Monitor lilichapisha picha za operesheni hiyo:
Meja Jenerali Abel Kandiho, Mkuu wa Ujasusi wa Kijeshi (CMI) na maafisa wengine wa usalama wamefika katika eneo la tukio.
Maafisa wa usalama wameongeza doria katika jiji lote, NTV Uganda inaripoti.
Gazeti la Daily Monitor linaripoti kuwa bunge limesitisha vikao vyake .
Nusu ya madereva waliozuiliwa Ethiopia waachiwa huru - UN
Serikali ya he Ethiopia imewaachilia madereva wa misaada walio na mkataba wa Umoja wa Mataifa waliokamatwa wiki iliyopita, kulingana na msemaji wa Umoja wa Mataifa.
Katika kikao mjini New York, Farhan Haq alisema Jumatatu kwamba madereva 34 wameachiliwa lakini wengine 36 bado wanazuiliwa.
Alitumai kuwa wafanyikazi waliosalia wa kandarasi na wafanyikazi 10 wa kitaifa wa UN waliokamatwa na mamlaka siku ya Ijumaa wataachiliwa.
Kukamatwa kwao kwa wafanyikazi wa UN na wafanyikazi wa kandarasi kulifuatia tangazo la serikali ya shirikisho la hali ya hatari mapema mwezi huo.
Kukamatwa kwa wafanyakazi wa UN na wafanyakazi wa kandarasi kunafuatia tangazo la hali ya hatari iliyowekwa na serikali mapema mwezi huu.
Hatua hiyo ilichukuliwa wakati wappiganaji waasi wa Tigray walitishia kuingia mji mkuu, Addis Ababa.
Siku ya Jumatatu, msemaji wa UN pia alitangaza kutolewa kwa msaada wa dharura wa dola milioni 40 kwa Waethiopia.
"Fedha hizi zitasaidia kuipiga jeki oparesheni za dharura katika maeneo yaliyoathiriwa na ghasia huko Tigray na kushughulikia mapema hali ya ukame kusini mwa Ethiopia," msemaji alielezea.
Maelfu ya watu wameuawa na mamilioni ya wengine kuyahama makazi yao katika vita vya mwaka mzima kati ya mamlaka ya Ethiopia na wapiganaji waasi wa Tigray People's Liberation Front (TPLF).
Ghasia za Capitol: Ukaidi wa Steve Bannon baada ya kujisalimisha kwa FBI
Mshirika wa Trump Steve Bannon ameusuta utawala wa Biden alipojisalimisha kwa FBI ili kujibu mashtaka kwa kukataa kushirikiana na uchunguzi wa ghasia wa bunge la Capitol.
"Hili litakuwa kosa la kuzimu," mtaalamu huyo wa zamani wa mikakati alisema nje ya ofisi ya FBI Washington.
Bw Bannon, 67, anakabiliwa na kifungo cha hadi mwaka mmoja na faini ya $100,000 (£75,000) iwapo atapatikana na hatia.
Alishtakiwa rasmi siku ya Ijumaa katika kesi hiyo.
Bw Bannon anashutumiwa kwa kukaidi wito wa kutoa ushahidi kuhusu anachojua kuhusu mipango ya maandamano hayo ambayo yaliishia kwa tukio la wafuasi wa Trump kuvamia Bunge la Congress.
Wafuasi wa Rais wa zamani Donald Trump walivamia jengo la Bunge mnamo 6 Januari wakati matokeo ya uchaguzi wa 2020 yakiidhinishwa ndani.