Vita vya Gaza: ICC yatafuta vibali vya kukamatwa kwa Netanyahu na viongozi wakuu wa Hamas
Mwendesha mashtaka wa ICC Karim Khan anasema kuna sababu za msingi kuthibitisha kwamba wawili hao walihusika na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu uliotekelezwa kuanzia tarehe 7 Oktoba 2023.
Muhtasari
- Kifo cha Rais wa Iran: Matukio ya hivi punde
- Katika Picha: Ulimwengu waomboleza kifo cha Rais wa Iran
- Tunachojua kuhusu waathiriwa wa ajali ya helikopta Iran
- Katika Picha: Ulimwengu unavyoomboleza kifo cha Rais wa Iran
- Mahakama: Zuma hastahili kugombea uchaguzi wa Mei
- Israel kuunda kamati maalum ya kupambana na uamuzi wa ICC
- ICC yatafuta vibali vya kukamatwa kwa Netanyahu na viongozi wakuu wa Hamas
- Ajali ya ndege Iran: Imam alinusurika kwa muda wa saa moja na kujaribu kutafuta msaada
- Tunafahamu nini kuhusu helikopta iliyoanguka Iran?
- Kifo cha Raisi ni pigo kwa 'ulimwengu wote wa Kiislamu' - kundi la Houthi
- Mazishi ya Raisi kufanyika kesho - ripoti
- Viongozi wa dunia wanasema nini?
- Mohammad Mokhber ni nani, anayetarajiwa kuchukua usukani kama rais wa mpito wa Iran?
- Rais William Ruto kuanza ziara ya kihistoria nchini Marekani
- 'Acha kuitisha Taiwan', rais mpya William Lai aionya China
- Rais wa Iran Ebrahim Raisi afariki dunia katika ajali ya helikopta - TV ya serikali
- Wanajeshi wa Marekani kuondoka Niger katikati mwa Septemba
- Mtu mmoja afariki dunia katika ajali ya msafara wa rais Ghana
- Hakuna kilichothibitishwa lakini mazingira yanafanana na kilichofanyika kwa mwanzilishi wa taifa hilo
- 'Hakuna dalili za yeyote aliye hai' katika eneo la ajali ya helikopta ya Raisi - TV ya serikali
- Waokoaji kufikia helikopta iliyoanguka 'dakika chache zijazo' – chombo cha habari cha serikali
- Vikosi vya uokoaji vyapata helikopta katika harakati za kumtafuta rais wa Iran
- Helikopta iliyombeba rais wa Iran 'yatua kwa shida' - Runinga ya serikali
- Vikosi vya uokoaji vyamtafuta Rais wa Iran Ebrahim Raisi
Moja kwa moja
Asha Juma & Ambia Hirsi
Habari za hivi punde, Liverpool wamemteua Slot kama meneja kuchukua nafasi ya Klopp

Chanzo cha picha, Getty Images
Kocha wa Feyenoord Arne Slot amethibitishwa kuwa meneja mpya wa Liverpool.
The Reds walikubali mkataba wa fidia wenye thamani ya £9.4m na klabu hiyo ya Uholanzi siku ya Ijumaa baada ya kocha huyo mwenye umri wa miaka 45 kutambuliwa kama mrithi wa Jurgen Klopp huko Anfield.
Klopp, ambaye alikuwa akiinoa Liverpool tangu Oktoba 2015, aliondoka katika klabu hiyo kufuatia ushindi wao wa fainali ya msimu dhidi ya Wolves Jumapili.
Mholanzi Slot ataanza rasmi kazi Liverpool mnamo 1 Juni, akipewa kibali cha kufanya kazi.
Kifo cha Rais wa Iran: Matukio ya hivi punde
- Iran imetangaza siku tano za maombolezo ya umma baada ya Rais wa Iran Ebrahim Raisi kufariki katika ajali ya helikopta kaskazini-magharibi mwa Iran pamoja na watu wengine saba akiwemo waziri wa mambo ya nje wa Tehran. Ajali hiyo ilitokea karibu na mpaka wa Iran na Azerbaijan, ambapo Raisi alikuwa akikutana na Rais Ilham Aliyev
- Mazishi ya Raisi yatafanyika kesho, na shughuli za kitamaduni zimesitishwa kwa siku saba zijazo
- Mohammad Mokhber ameteuliwa kuwa kaimu rais, na Bagheri Kani, ambaye alikuwa naibu waziri wa mambo ya nje, sasa ni waziri wa mambo ya nje.
- Katika nchi za Magharibi, viongozi kutoka Umoja wa Ulaya, Nato na Shirika la Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) zimetuma rambirambi zao wakati Iran ikimuomboleza kiongozi wake aliyefariki.
- Makundi ya Hezbollah, Hamas na Houthis yanayoungwa mkono na Iran, ambayo yameorodheshwa na nchi zingine duniani kuwa ni mashirika ya kigaidi, pia yametoa salamu zao za rambirambi kwa wananchi wa Iran.
- Chanzo cha ajali ya helikopta bado haijabainika, lakini Urusi (mshirika wa karibu wa Tehran) imetoa msaada wake katika uchunguzi huo.
- Rais wa mpito Mokhber tayari amehutubia kikao cha baraza la mawaziri mjini Tehran, lakini utaratibu wa kikatiba unaonyesha kwamba uchaguzi mpya unatarajiwa kufanyika katika siku 50 zijazo.
- Kifo cha Raisi kimeibua hisia mbalimbali duniani, kuanzia waandamanaji waliokusanyika nje ya ubalozi wa Iran mjini Berlin hadi bendera zinazopepea nusu mlingoti mjini Moscow, Beirut na kwingineko.
Katika Picha: Kuanzia maandamano dhidi ya utawala wa Iran hadi bendera zinazopepea nusu mlingoti
Kifo cha Rais wa Iran Ebrahim Raisi kimeibua hisia mbalimbali duniani.
Kuanzia waandamanaji wanaokusanyika nje ya ubalozi wa Iran mjini Berlin hadi bendera zinazopepea nusu mlingoti mjini Moscow, Beirut na kwingineko, ulimwengu unaendelea kuguswa na kifo cha Raisi.

Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Mjini Berlin, waandamanaji kutoka Baraza la Kitaifa la Upinzani dhidi ya Iran wako nje ya ubalozi wa Iran, wakiwa wameshikilia mabango yanayoonyesha uso wa Rais wa Iran Ebrahim Raisi ukiwa umepchorwa kwa rangi nyekundu. 
Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Huko Beirut, bendera ya taifa ya Lebanon inapepea nusu mlingoti katika Ikulu ya Serikali huku serikali ikitangaza siku tatu za maombolezo. 
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Nchini Iraq, viongozi wa kidini katika ofisi ya mwakilishi wa Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei wanaomboleza vifo vya Raisi na wengine. 
Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/Shutterstock
Maelezo ya picha, Picha ya Raisi, yenye maneno ya Kirusi, "Tunaomboleza" ikionyeshwa nje ya ubalozi wa Irani huko Moscow Tunachojua kuhusu waathiriwa wa ajali ya ndege Iran

Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Warusi wamekuwa wakitoa heshima kwa waliofariki katika ajali ya helikopta kwenye Ubalozi wa Iran mjini Moscow Tumekuwa tukiripoti kwwa Rais wa Iran Ebrahim Raisi alifariki katika ajali ya helikopta siku ya Jumapili pamoja na abiria wengine saba.
Wafuatao ni waathiriwa wengine waliokuwa naye katika msafara wa rais Raisi.
- Mmoja wa wanadiplomasia wakuu wa Iran, Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian, na gavana wa Jimbo la Azerbaijan Mashariki mwa Iran, Malik Rahmati, pia walifariki katika ajali hiyo.
- Abiria wengine walikuwa: Mohammad Mehdi Mousavi, mkuu wa timu ya usalama ya rais; marubani wenza Kanali Mohsen Daryanush na Kanali Seyyed Taher Mostafavi; na fundi Maj Behrouz Qadimi
- Imamu wa Ijumaa wa Tabriz, Mohammad Ali Al-e Hashem, pia alikuwa kwenye meli. Alinusurika kwa saa moja baada ya ajali hiyo na kujaribu kuwasiliana na ofisi ya rais, kulingana na mkuu wa Shirika la Kudhibiti Mgogoro wa Iran.
Mahakama ya juu nchini Afrika Kusini yamzuia Zuma kugombea uchaguzi

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Jacob Zuma anaendesha kampeni kikamilifu dhidi ya ANC, aliyokuwa akiiongoza Mahakama ya juu zaidi nchini Afrika Kusini imemzuia rais wa zamani Jacob Zuma kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu utakaofanyika wiki ijayo.
Mahakama ya Kikatiba iliamua kwamba kifungo chake cha miezi 15 jela kwa kupuuza agizo la mahakama - uhalifu chini ya sheria za Afrika Kusini - kilimfungia.
Bw Zuma alipatikana na hatia mwaka wa 2021 kwa kukataa kutoa ushahidi wake katika uchunguzi wa ufisadi wakati wa uongozi wake uliokamilika mwaka wa 2018.
Amekuwa akifanya kampeni chini ykupitia chama kipya kilichoanzishwa cha Umkhonto weSizwe (MK) baada ya kutofautiana na chama tawala cha African National Congress (ANC).
Katibu mkuu wa MK Sihle Ngubane amesema chama hicho kimesikitishwa na uamuzi huo, lakini hautaathiri kampeni za chama na uso wa Bw Zuma utaendelea kubaki kwenye karatasi ya kupigia kura katika uchaguzi wa tarehe 29 Mei.
"Bado ni kiongozi wa chama. [hukumu] haiathiri kampeni yetu hata kidogo," alisema.
Wananchi wa Afrika Kusini huvipigia kura vyama vya siasa, huku wagombea walio juu ya orodha zao wakipata viti vya ubunge kulingana na idadi ya kura ambazo chama kinapata.
Tume ya uchaguzi ilisema jina la Bw Zuma sasa litaondolewa kwenye orodha ya wagombea ubunge wa MK, huku ikithibitisha kwamba sura yake itasalia kwenye karatasi za kupigia kura, sambamba na nembo ya chama chake.
Wanachama wa MK waliimba na kucheza nje ya mahakama wakimuonyesha Bw Zuma kama mwathiriwa, huku wale waliokuwa ndani - wengine wakiwa wamevalia mavazi ya kitamaduni ya Kizulu - walikaa kimya huku Jaji Leona Theron akisoma hukumu hiyo kwa kauli moja.
Bw Zuma bado hajatoa maoni yake kuhusu uamuzi huo.
Wafuasi wake walizua ghasia baada ya kupelekwa jela mwaka wa 2021, na baadhi ya viongozi wake walitishia ghasia iwapo mahakama ingemwita kugombea ubunge.
Lakini maafisa wa MK wamebadili kauli yao wakisema lengo la chama ni kupata thuluthi mbili ya kura ili katiba ya Afrika Kusini ibadilishwe, na Bw Zuma arejeshwe mamlakani.
Mahakamani, mawakili wake walikuwa wamedai kwamba kwa sababu aliachiliwa baada ya miezi mitatu jela na mrithi wake, Rais Cyril Ramaphosa, kifungo chake kilichosalia kilifutwa.
Lakini mahakama ilikataa, ikisema urefu wa muda aliokaa gerezani haukuwa na maana.
Katiba ya Afrika Kusini ilipiga marufuku mtu yeyote aliyehukumiwa kifungo cha miezi 12 jela, bila chaguo la faini, kuhudumu bungeni ili kulinda uadilifu wa "utawala wa kidemokrasia" ulioanzishwa baada ya kumalizika kwa mfumo wa ubaguzi wa rangi mwaka 1994, Jaji Theron alisema.
Maelezo zaidi:
Habari za hivi punde, Israel kuunda kamati maalum ya kupambana na uamuzi wa ICC
Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel muda mfupi uliopita ametangaza kuwa kamati maalum itaundwa kufuatia tangazo hkutoka kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu.
Israel Katz anasema kamati hiyo itaundwa kupambana na uamuzi wa ICC, ambao anasema unanuia kufunga mikono ya taifa la Israel na kulinyima haki ya kujilinda.
Katz anaitaja hatua ya mahakama - ambayo imeomba hati ya kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel na kiongozi wa Hamas huko Gaza - "shambulio la moja kwa moja" dhidi ya waathiriwa wa shambulio la Oktoba 7.
"Hakuna nguvu duniani" itazuia Israel kuwarudisha mateka nyumbani na kuwaangamiza Hamas, anasema.
Anaongeza kuwa anapanga kuzungumza na wenzake kote duniani kuhakikisha wanapinga uamuzi wa mwendesha mashtaka wa ICC Karim Khan.
Hamas imepokeaje uamuzi huo?
Afisa mkuu wa Hamas Sami Abu Zuhri anaiambia Reuters kwamba kutafuta vibali vya kukamatwa kwa viongozi watatu wa Hamas ni sawa na "kunalinganisha mwathiriwa na mnyongaji".
Pia anadai uamuzi huo unaihimiza Israel kuendeleza kile alichokiita "vita vyake vya maangamizi".
Habari za hivi punde, ICC yatoa ombi la kukamatwa kwa Netanyahu na viongozi wakuu wa Hamas

Chanzo cha picha, Getty / EPA
Maelezo ya picha, Benjamin Netanyahu (kushoto) na Yahya Sinwar Mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ametuma maombi ya hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na kiongozi wa Hamas huko Gaza kwa uhalifu wa kivita.
Karim Khan KC anasema kuna sababu za kuridhisha na za kuaminika kwamba wawili hao waliwajibika kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu kuanzia tarehe 7 Oktoba 2023.
Waziri wa ulinzi wa Israel Yoav Gallant na kiongozi wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh, mkuu wake wa kijeshi Mohammed Deif pia wanasakwa ili kukamatwa.
Mahakama ya ICC, yenye makao yake makuu mjini The Hague, imekuwa ikichunguza hatua za Israel katika maeneo yanayokaliwa kwa miaka mitatu iliyopita - na hivi karibuni zaidi hatua za Hamas pia.
Bw Netanyahu hivi majuzi alitaja matarajio ya viongozi wakuu wa Israel kujiunga na orodha inayotafutwa ya ICC "ghadhabu ya idadi ya kihistoria".
Majaji wa ICC sasa wataamua kama wanaamini kuwa ushahidi unatosha kutoa hati za kukamatwa - jambo ambalo linaweza kuchukua wiki au miezi.
Bw Khan aliwashutumu viongozi wa Hamas kwa kufanya uhalifu ikiwa ni pamoja na kuangamiza, mauaji, utekaji nyara, ubakaji na unyanyasaji wa kingono, na mateso.
"Uhalifu dhidi ya binadamu uliowasilishwa ulikuwa sehemu ya shambulio lililoenea na la kimfumo dhidi ya raia wa Israel na Hamas na vikundi vingine vyenye silaha," alisema katika taarifa.
Ajali ya ndege Iran: Imam alinusurika kwa muda wa saa moja na kujaribu kutafuta msaada
Maelezo zaidi yanapoendelea kujitokeza kuhusu ajali ya helikopta iliyomuua rais wa Iran Ibrahim Rahisi, taswira ya kutisha ya kile kilichotokea baada ya ndege kuanguka imeanza kujitokeza.
Mmoja wa abiria waliokuwemo ndani ya ndege hiyo alikuwa Mohammad Ali Al-Hashem, Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Tabriz, mji ambao msafara huo ulikuwa unaelekea.
Kwa mujibu wa Mohammad Nami, mkuu wa Shirika la Kudhibiti Migogoro ya Iran, Al-Hashem alinusurika kwa saa nzima baada ya ajali hiyo.
Alijaribu hata kuwasiliana na ofisi ya rais.
“Hakuna uchunguzi wa chembechembe za vinasaba, DNA iliyohitajika kubaini abiria,” anasema aliambia mwandishi wa BBC.
Watu wote tisa wakiwemo wafanyakazi wa ndege walifariki katika ajali hiyo ya helikopta.
Tunafahamu nini kuhusu helikopta iliyoanguka Iran?

Chanzo cha picha, Crown copyright
Huku maelezo yakianza kujitokeza polepole, vyombo vya habari vya serikali ya Iran vinaripoti kwamba helikopta iliyombeba rais na waziri wa mambo ya nje ilikuwa Bell 212.
Haijulikani helikopta hiyo ilikuwa imefanya kazi kwa muda gani, lakini aina hiyo ya ulitengenezwa kwa jeshi la Canada katika miaka ya 1960.
(Kama ukumbusho, miongo kadhaa ya vikwazo vya Marekani na kimataifa vilianza baada ya mapinduzi ya Iran mwaka 1979)
Helikopta hizo zilitengenezwa na kampuni ya Bell Helicopter ya Marekani na kutumika sana na waendeshaji wa serikali, ikiwa ni pamoja na vyombo vya sheria vya Marekani na polisi wa kitaifa wa Thailand.
Jeshi la wanamaji na jeshi la anga la Iran lina jumla ya 10, kulingana na nyaraka ya Jeshi la Anga la Dunia la 2024 la FlightGlobal, lakini haijulikani ni ngapi serikali ya Iran zinafanya kazi.
Zinaweza kutumiwa kufanya mambo tofauti, ikiwa ni pamoja na kubeba watu na mizigo, na zinaweza kuwekwa silaha kwa ajili ya kupigana.
Shirika la habari la serikali la IRNA linasema kuwa helikopta iliyombeba rais inaweza kubeba abiria sita na wafanyakazi wawili.
Kulingana na Wakfu wa Usalama wa Ndege, shirika lisilo la kiserekali, ajali mbaya ya hivi punde zaidi iliyohusisha ndege aina ya Bell 212 ilitokea Septemba 2023 wakati mwanamitindo aliyekuwa akiendeshwa kwa faragha ilianguka kwenye ufuo wa Falme za Kiarabu.
Tukio la hivi punde la kifo nchini Iran lilitokea Aprili 2018, wakati Bell 212 ilikuwa ikimsafirisha mgonjwa aliyekumbwa na mshtuko wa moyo.
Kifo cha Raisi ni pigo kwa 'ulimwengu wote wa Kiislamu' - kundi la Houthi
Hapo awali, tulikufahamisha kauli kutoka kwa washirika wawili wa Iran katika eneo hili - Hamas, huko Gaza, na Hezbollah, ambayo inahudumu kusini mwa Lebanon.
Sasa waasi wa Houthi wa Yemen - ambao, kama Hamas na Hezbollah, wanaungwa mkono na kufadhiliwa na Iran wametoa rambi rabi zao kuhusu kifo cha rais wa Iran Ibrahim Rahisi.
Msemaji wa Houthi Mohammed Abdulsalam katika chapisho kwenye X, zamani Twitter, nasema kwamba kifo cha Rais Raisi ni "pigo sio tu kwa Iran bali pia kwa ulimwengu wote wa Kiislamu na Palestina na Gaza".
Anaongeza kuwa Wapalestina "wanahitaji sana uwepo wa rais wa aina hiyo ambaye aliendelea kutetea" haki yao ya uhuru.
Kundi la waasi la Houthi linaichukulia Israel kuwa adui yake na limeshambulia meli za mizigo katika Bahari ya Shamu katika miezi ya hivi karibuni kujibu vita huko Gaza.
Mazishi ya Raisi kufanyika kesho - ripoti
Chombo cha habari cha Iran, Tasnim, ambacho kina mfungamano na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini humo, kinaripoti kuwa mazishi ya Rais Ebrahim Raisi yatafanyika kesho Tabriz - mji aliokuwa akisafiria jana.
Kituo hicho kinasema mazishi ya watu wengine wote waliofariki pia yatafanyika, ikinukuu kauli ya maafisa katika jimbo la Azerbaijan Mashariki mwa Iran.
Miili hiyo kwanza itapelekwa kwa idara ya uchunguzi wa kitaalamu huko Tabriz.
Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei pia ametoa taarifa rasmi na kutangaza siku tano za maombolezo ya kitaifa kwa heshima ya rais Raisi.
Wakati huo huo Baraza la mawaziri la Iran limemteua Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Ali Bagheri Kani kuwa kaimu waziri wa mambo ya nje, kufuatia kifo cha Hossein Amir-Abdollahian, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.
Inafuatia mkutano wa matawi matatu ya serikali ya Iran - mtendaji, sheria na mahakama.
Makamu wa Kwanza wa Rais Mohammad Mokhber anatarajiwa kuchukua nafasi ya rais.
Katiba ya Iran inasema makamu wa kwanza wa rais ataongoza kwa kipindi cha mpito kwa muda wa siku 50 iwapo rais atafariki akiwa madarakani.
Mokhber ameiambia televisheni ya taifa kwamba watafuata njia ya Rais Raisi katika "kutekeleza majukumu waliyopewa bila usumbufu wowote".
Viongozi wakuu wa kikanda dunia wanasema nini?

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov Viongozi wa kimataifa wameanza kutoa maoni yao kuhusu habari kwamba Rais wa Iran Ebrahim Raisi amefariki dunia. Hivi ndivyo wanavyosema:
- Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amechapisha kwenye mtandao wa X akisema "amehuzunishwa sana na kushtushwa na kifo cha kutisha" cha Rais Raisi na taifa lake "anasimama na Iran" wakati huu wa "majonzi"
- Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif amesema kifo cha Raisi ni "hasara kubwa" na taifa lake litaadhimisha siku ya maombolezo.
- Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu Mohammed bin Zayed Al Nahyan anasema nchi yake inasimama na Iran wakati huu, shirika la habari la Reuters linaripoti.
- Wakati Rais Nicolás Maduro wa Venezuela amemsifu Rais Raisi kama rafiki asiye na masharti na kiongozi wa kipekee.
- Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov anasema Rais Raisi na Hossein Amir-Adollahian "walijulikana kama marafiki wa kweli na wa kutegemewa wa nchi yetu".
"Jukumu lao katika kuimarisha ushirikiano wa kunufaisha kati ya Urusi na Iran na ushirikiano wa kuaminiana ni muhimu sana," anasema, na kuongeza kuwa "mawazo na mioyo ya Urusi iko pamoja na [Iran] katika nyakati hii ya huzuni".
Ikumbukwe kuwa nchi za Magharibi zinaishutumu Iran kwa kutuma mara kwa mara ndege zisizo na rubani kwa Urusi ili kuzitumia katika vita vyake dhidi ya Ukraine. Iran inasema ilitoa "idadi ndogo" ya ndege zisizo na rubani kwa Urusi kabla ya vita kuanza mnamo Februari 2022.
Wakati huo huo, Rais wa Syria inayokumbwa na vita Bashar al-Assad "alithibitisha mshikamano wa Syria na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na familia za marehemu na wenzi wake".
Iran imekuwa ikiunga mkono pakubwa utawala wa Assad wakati wa miaka mingi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.
Soma zaidi:
Mohammad Mokhber ni nani, anayetarajiwa kuchukua usukani kama rais wa mpito wa Iran?

Chanzo cha picha, Getty Images
Sasa tuangazie kwa undani zaidi makamu wa kwanza wa rais Mohammad Mokhber ni nani, kwani kuna uwezekano mkubwa atateuliwa kuwa rais wa mpito na Kiongozi Mkuu wa Iran, ambaye hatimaye ndiye mwenye kauli ya mwisho katika masuala yote ya serikali:
•Mokhber alichaguliwa kuwa makamu wa kwanza wa rais kwenye uchaguzi wa 2021 ambao Rais Raisi aliingia madarakani.
•Mwanadiplomasia huyo mkuu mwenye umri wa miaka 68 anajulikana kwa kuwa karibu na Kiongozi Mkuu Ali Khamenei
•Atakuwa sehemu ya baraza la watu watatu litakaloandaa uchaguzi mpya wa rais katika muda wa siku 50 zijazo
•Mokhber alitembelea Moscow mwezi Oktoba wakati Iran ilipokubali kusambaza makombora ya ardhini na ndege zisizo na rubani kwa jeshi la Urusi.
•Mnamo mwaka wa 2010, Umoja wa Ulaya ulimjumuisha Mokhber kwenye orodha ya watu na mashirika iliyokuwa ikiwekea vikwazo kwa madai ya kuhusika katika "shughuli za nyuklia au makombora ya masafa marefu". Aliondolewa kwenye orodha hiyo miaka miwili baadaye
•Mokhber hapo awali alikuwa mkuu wa Setad, mfuko wa uwekezaji unaohusishwa na kiongozi mkuu
•Mwaka 2013, Wizara ya fedha ya Marekani iliongeza hazina hiyo ya Setad na kampuni 37 ilizozisimamia kwenye orodha ya mashirika yaliyowekewa vikwazo.
Soma zaidi:
Rais William Ruto kuanza ziara ya kihistoria nchini Marekani
Rais William Ruto wa Kenya anaanza ziara ya kihistoria nchini Marekani, ambayo inatarajiwa kuwa mapinduzi kwa Kenya yenye kulenga kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbilo.
Ziara hiyo ambayo ni ya kwanza kwa kipindi cha miaka 15, ilifanyika na rais Daniel Arap Moi mwaka 1980 na Rais Mwai Kibaki mwaka 2003.
Inachukuliwa kama mfano mwema hasa ikizingatiwa kuwa mara ya mwisho ziara ya kiongozi wa Afrika ilifanyika mwaka 2009, wakati Rais George Bush alipokuwa mwenyeji wa rais John Kufour.
Rais anatarajiwa kuiwakilisha Kenya kama kitovu na eneo la kimkakati la uwekezaji.
Pia anatarajiwa kutoa hamasa kwa makampuni ya Marekani kuchukua fursa iliyopo na kuwekeza katika sekta mbalimbali.
Msemaji wa Ikulu Hussein Mohamed, alisema safari ya rais itaangazia ushirikiano wa miongo sita kati ya nchi hizo mbili na kuvutia ushirikiano zaidi.
'Acha kuitisha Taiwan', rais mpya William Lai aionya China

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais mpya wa Taiwan aliyeapishwa William Lai ameitaka China kuacha kutishia kisiwa hicho na kukubali kuwepo kwa demokrasia yake.
Aliitaka Beijing kuchagua mazungumzo ya kuleta makubaliano badala ya kuendeleza makabiliano muda mfupi baada ya kuapishwa siku ya Jumatatu.
Pia alisema Taiwan haitarudi nyuma kuhusu vitisho kutoka kwa China, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikidai kisiwa hicho ni chake.
Bw. Lai anachukiwa na China ambayo inamwona kama "mtu anayetaka kujitenga".
Pia imeongeza shinikizo kwa Taiwan katika miaka ya hivi karibuni.
Uvamizi wa kijeshi unaofanywa na Uchina kuzunguka maji na anga ya kisiwa hicho umekuwa jambo la kawaida katika miaka michache iliyopita na kusababisha hofu ya migogoro.
Katika hotuba yake, Bw Lai aliitaja hii "changamoto kubwa ya kimkakati kwa amani na kiongozi huyomwenye umri wamiaka 64 pia alishikamana kwa karibu na mbinu iliyotumiwa na rais mtangulizi wake Tsai Ing-wen, ambaye urithi wake utaelezwana utunzaji wake wa tahadhari lakini thabiti kuihusu Beijing.
Bw Lai, daktari aliyegeuka kuwa mwanasiasa, alishinda kinyang'anyiro cha urais mwezi Januari, na kupata muhula wa tatu ambao haujawahi kushuhudiwa kwa Chama chake cha Democratic Progressive (DPP).
Alihudumu kama makamu wa rais wa Bi Tsai tangu 2020, na kabla ya hapo kama waziri mkuu wake. Katika siku zake za ujana, alijulikana kuwa mwanasiasa mwenye msimamo mkali zaidi ambaye alitaka waziwazi uhuru wa Taiwan.
Soma zaidi:
Habari za hivi punde, Rais wa Iran Ebrahim Raisi afariki dunia katika ajali ya helikopta - TV ya serikali

Chanzo cha picha, Reuters
Rais Ebrahim Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian na wengine kadhaa wamethibitishwa kufariki dunia katika ajali ya helikopta iliyotokea Jumapili kaskazini-magharibi mwa Iran, televisheni ya taifa imesema.
Uchambuzi na Lyse Doucet, Mwandishi mwandamizi wa kimataifa
Rais Ebrahim Raisi alikuwa karibu kufikia nafasi ya juu ya madaraka katika Jamhuri ya Kiislamu na alipendekezwa sana kupanda hadi nafasi hiyo.
Kufariki ghafla kwa Rais Ebrahim Raisi katika ajali ya helikopta siku ya Jumapili kumezua gumzo la nani hatimaye atachukua nafasi ya kiongozi mkuu Ayatollah Ali Khamenei mwenye umri wa miaka 85 ambaye afya yake imekuwa ikifuatiliwa na wengi kwa muda mrefu.
Hatima mbaya ya rais wa Iran mwenye misimamo mikali haitarajiwi kuvuruga mwelekeo wa sera ya Iran au kuitikisa Jamhuri ya Kiislamu kwa njia yoyote ile.
Lakini itakuwa majaribu kwa mfumo ambao watu wenye msimamo mkali wa kihafidhina sasa wanatawala maeneo yote ya mamlaka, waliochaguliwa na ambao hawajachaguliwa.
Wapinzani wake watafurahishwa na kuondoka kwa mwendesha mashtaka wa zamani anayeshutumiwa kwa jukumu muhimu katika mauaji makubwa ya wafungwa wa kisiasa katika miaka ya 1980 ambayo alikanusha; watatumaini mwisho wa utawala wake utaharakisha mwisho wa utawala huu.
Kwa wahafidhina watawala wa Iran, mazishi ya serikali yatakuwa tukio lililojaa hisia; pia itakuwa fursa ya kuanza kutuma ishara zao za mwendelezo.
Nafasi nyingine muhimu ambayo lazima ijazwe ni nafasi ya kiongozi huyo kwenye Bodi ya Wataalamu, ambayo ina mamlaka ya kuchagua kiongozi mkuu mpya, wakati mabadiliko hayo muhimu zaidi yatakapowadia.
Soma zaidi:
Wanajeshi wa Marekani kuondoka Niger katikati mwa Septemba

Chanzo cha picha, AFP
Marekani na Niger wamekubaliana kwamba wanajeshi wa Marekani wataondoka nchini humo kabla ya Septemba 15," walitangaza katika taarifa ya pamoja siku ya Jumapili.
Walisema nchi hizo mbili "zimefikia makubaliano ya kujiondoa ili kutekeleza uondoaji wa vikosi vya Marekani, ambayo tayari imeanza".
Marekani imeitegemea Niger kama msingi wake mkuu wa kufuatilia shughuli za kikanda za wanajihadi.
Taarifa hiyo ilipongeza "kujitoa mhanga kwa pamoja kwa majeshi ya Niger na Marekani katika mapambano dhidi ya ugaidi".
Taarifa hiyo ilisema kujiondoa huko hakutaathiri kuendelea kwa uhusiano kati ya Marekani na Niger.
"Marekani na Niger zimejitolea kufanya mazungumzo ya kidiplomasia yanayoendelea ili kufafanua mustakabali wa uhusiano wao wa pande mbili," taarifa hiyo ilisema.
Mnamo mwezi Machi, Niger ilitangaza kumalizika kwa makubaliano yake ya kijeshi na Marekani. Msemaji wa jeshi Kanali Amadou Abdramane aliishutumu Marekani kwa kuleta pingamizi kuhusu washirika ambao Niger iliwachagua.
Kanali Abdramane aliishutumu Marekani kwa "mtazamo wake wa kudharau" na "tishio la kulipiza kisasi".
Mvutano uliongezeka kati ya Marekani na Niger baada ya rais mteule, Mohamed Bazoum, kupinduliwa mwaka jana.
Niger iko katika eneo la Sahel barani Afrika, ambalo linachukuliwa kuwa kitovu kipya cha kimataifa cha kundi la Islamic State.
Soma zaidi:
Mtu mmoja afariki dunia katika ajali ya msafara wa rais Ghana
Mtu mmoja amethibitishwa kufariki huku wengine wakipata majeraha tofauti tofauti kufuatia ajali iliyohusisha magari kadhaa ya msafara wa Rais Nana Akufo Addo siku ya Jumapili.
Chanzo kamili cha ajali hiyo hakijajulikana.
Msafara huo ulikuwa ukirejea kutoka Kumasi kuelekea mji mkuu, Accra.
Dereva wa mojawapo ya magari hayo alipoteza maisha, huku wengine katika usalama wa rais wakipata majeraha mbalimbali na wamepata matibabu ya awali katika hospitali iliyo karibu.
Wamesafirishwa hadi Accra kwa matibabu zaidi.
Baadhi ya magari pia yameharibika kiasi cha kutoweza kurekebishwa. Taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais ilionyesha kuwa Rais Akufo Addo yuko salama na alisafiri kurejea Accra kwa helikopta ya kijeshi.
Barabara kuu ya Accra-Kumasi ni ya njia moja, na ajali hutokea mara kwa mara, mara nyingi husababisha vifo.
Hakuna kilichothibitishwa lakini mazingira yanafanana na kilichofanyika kwa mwanzilishi wa taifa hilo

Chanzo cha picha, Reuters
Kwa walioishi Iran mwishoni mwa miaka ya 1980, siku zilizotangulia kutangazwa rasmi kwa kifo cha Ayatollah Khomeini, mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu, picha na mazishi yaliyofuata bado yapo kwenye kumbukumbu za watu.
Vyombo vya habari vya Jamhuri ya Kiislamu vilitayarisha mazingira kwa kuwataka watu kumuombea dua kiongozi huyo. Waaminifu walijibu kwa kukusanyika misikitini usiku kucha. Hatimaye kulipopambazuka hali katika misikiti hiyo ilibadilika kutoka kumuombea dua na afya njema hadi maombolezo ya msiba wake. Na kisha likafuatia tangazo rasmi la serikali saa 07:00.
Ripoti za vyombo vya habari vya serikali na sauti ya hotuba ya kiongozi mkuu wa sasa Ayatollah Ali Khamenei katika saa za mwisho inaonekana kufanana na hali hiyo - kuwataka umma kusali, wafuasi kukusanyika kwenye uwanja wa Tehran kufanya maombi, na hakikisho kwamba shughuli za kila siku za nchi hazitaathiriwa.
Soma zaidi:
