Machungu ya ushuru mpya wa Trump yaanza kuonekana kwenye masoko ya hisa ya kimataifa
Katikati ya wiki Trump alitangaza ukomo wa chini wa ushuru wa 10% kwa bidhaa zote zinazoingia nchini humo, kiwango hiki na vingine vya juu kulingana na nchi, mbali na masoko ya kimataifa, soko lake la ndani limehitimisha wiki mbaya zaidi tangu 2020.
Maandamano ya kumpinga Trump yanafanyika Ulaya na Marekani
Chanzo cha picha, PA Media
Maelezo ya picha, Waandamanaji katika uwanja wa Trafalgar Square mjini London walimlinganisha rais wa Marekani na Putin wa Urusi
Kumeshuhudiwa maandamano ya kumpinga Trump yanayofanyika
kote Ulaya na Marekani.
Kuanzia Berlin hadi London, waandamanaji wamemshambulia rais
wa Marekani na bilionea mshauri wa Trump, Elon Musk, wakitaka "kukomeshwa
kwa machafuko" na kuelezea kuunga mkono Ukraine.
Maandamano yamepangwa kufanyika katika majimbo yote 50 na
Washington DC leo, huku watu wakiazimia kumpinga Rais Donald Trump na sera
zake.
Kumekuwa na maandamano ya mara kwa mara tangu aingie
madarakani, lakini waandaaji wanasema wanatarajia leo kuwa siku moja kubwa
zaidi ya maandamano tangu Trump aanze muhula wake wa pili.
Wakili mashuhuri nchini Kenya Pheroze Nowrojee afariki dunia
Chanzo cha picha, LSK
Wakili Mkongwe Pheroze Nowrojee amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 84, Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria nchini Kenya Faith Odhiambo amethibitisha.
Odhiambo alimsifu Nowrojee kama mtu mwenye utulivu na tabia ya heshima, ambaye maisha yake yalidhihirisha wajibu wa kutumikia na kujitolea kwenye masuala ya haki.
"Ni siku ya huzuni kwa taaluma ya sheria tunapomuaga mtu ambaye alitufundisha maana ya kuwa wataalamu mashuhuri.
Mioyo yetu inazizima leo, kwani tumempoteza mmoja wa watu wakuu zaidi kuwahi kufanya hivyo," alisema.
"Tunapoenzi kiongozi huyu katika kuheshimu katiba, tunatoa rambirambi zetu za dhati kwa familia yake, marafiki, na kila mtu ambaye ameguswa na maisha yake.
''Wakili Pheroze Nowrojee apumzike kwa amani ya milele." Faith Odhiambo alieleza
Kijana wa wanandoa wa Uingereza wanaoshikiliwa na Taliban aiomba Marekani msaada
Chanzo cha picha, Handout
Mtoto wa wanandoa wa Uingereza ambao walizuiliwa na kundi la
Taliban wiki tisa zilizopita anaiomba Marekani kusaidia kuachiliwa kwa wawili
hao wanaoshikiliwa katika gereza la Afghanistan.
Peter Reynolds, 79, na mkewe Barbie, 75, walikamatwa tarehe
1 Februari wakati wakirejea nyumbani kwao katika jimbo la kati la Bamiyan.
Mtoto wao wa kiume Jonathan aliitaka Ikulu ya White House
kuingilia kati baada ya Faye Hall, Mmarekani ambaye alizuiliwa pamoja nao,
kuachiliwa wiki iliyopita na Taliban, ambayo ilidhibiti madaraka nchini
Afghanistan mnamo 2021.
Aliiambia BBC News kwamba kuzuiliwa kwa wazazi wake - ambao
wameishi Afghanistan kwa miaka 18 na kuendesha miradi ya kielimu -
"kumekuwa "usumbufu ulioichosha sana familia yao.
Bwana Reynolds alisema: "Yeyote ambaye ana uwezo wa kuwasaidia
wakafunguliwa na kuwa huru, iwe ni Taliban, iwe ni serikali ya Uingereza au iwe
ni serikali ya Marekani, ninamuomba – afanye hivyo sasa, tafadhali.
"Na ikiwa una uwezo wa kuweka shinikizo kwa watu
wanaoshikilia uhuru wao, fanya hivyo sasa, tafadhali."
Bi Hall amekuwa raia wa nne wa Marekani kuachiliwa na
Taliban tangu mwezi Januari baada ya mazungumzo kati ya maafisa mjini Kabul -
katika kile ambacho kundi hilo lilieleza kuwa ni "ishara njema" kwa
utawala wa Trump.
Hilo lilimfanya Reynolds kumwomba Rais wa Marekani Donald
Trump moja kwa moja kusaidia katika kuachiliwa kwa Peter na Barbie, katika
video iliyochukuliwa nje ya Ikulu ya White House mapema wiki hii.
Jaguar Land Rover kusitisha usafirishaji kwenda Marekani mwezi Aprili
Kampuni ya kutengeneza magari ya kifahari nchini Uingereza, Jaguar Land Rover (JLR), inasema "itasitisha" usafirishaji wa magari yake kwenda Marekani mwezi Aprili, inapojipanga na namna ya kushughulikia "masharti mapya ya biashara" ya ushuru wa Trump.
"Tunapojitahidi kushughulikia masharti mapya ya biashara na washirika wetu wa biashara, tunachukua hatua za muda mfupi, ikiwa ni pamoja na kusitisha usafirishaji mwezi Aprili, tunapoendeleza mipango yetu ya kati hadi ya muda mrefu," JLR ilisema katika taarifa iliyotumwa kwa barua pepe kwa BBC.
JLR ilithibitisha kusimamishwa kwa mauzo ya nje kwa muda baada ya gazeti la Times kuripoti mpango huo.
Baadhi ya wafanyabiashara wa Marekani wana wasiwasi kuhusu athari za ushuru mkubwa wa Rais wa Marekani Donald Trump kwani ushuru wa 10% sasa umeanza kutumika katika baadhi ya nchi - ikiwa ni pamoja na Uingereza.
Rais wa shirikisho la Black Farmers aliambia BBC kwamba ushuru unaathiri sekta hiyo "moja kwa moja" huku waagizaji wa Marekani wakisema "hatua hiyo haitakuwa na faida".
Kampuni kubwa kama Apple na Nike tayari zinahisi athari za hatua hizo mpya huku soko la kimataifa likikumbwa na msukosuko - Viashiria vyote vikuu vya Wall Street vikiporomoka kwa zaidi ya 5%.
Tanzania yazindua jengo la Mahakama la kwanza kwa ukubwa Afrika na la 6 duniani
Chanzo cha picha, MAELEZO
Tanzania imezindua jengo jipya la Makao Makuu ya Mahakama ya nchi hiyo ambalo ni la kwanza kwanza kwa ukubwa barani Afrika na la sita duniani.
Akiongoza shughuli za uzinduzi wa jengo hilo ambalo litatumika kutoa huduma za kimahakama, Rais Samia Suluhu Hassan amesema: ‘’Nimejionea kazi kubwa iliyofanyika, hakika jengo hili lina kila sifa ya kuitwa jengo kuu la mahakama ya Tanzania’’ alisema rais Samia
‘’Baada ya Kazakhstan Tanzania ni ya pili kuwa na chumba cha judiciary’’aliongeza.
Amesema jengo hilo ni urithi wa kipekee unaoleta hadhi, fursa za kiuchumi, na kuvutia wageni kutoka ndani na nje ya nchi.
Amesema hatua hii ni ya kihistoria nchini Tanzania kwa zaidi ya miaka 100 ambayo muhimili wa mahakama haukuwa na ofisi za makao makuu.
Rais Samia ameshukuru mataifa wahisani kwa ufadhili ikiwemo Benki ya dunia kwa kufanikisha ujenzi hu owa jengo la mahakama kuu,Jengo la Tume ya Utumishi wa Mahakama, na majengo ya makazi ya majaji.
Hatua hii sasa inakamilisha mchakato wa dola ya Tanzania kuhamia Dodoma.
Jengo la Mahakama ya Kuala Lumpur, Malaysia ndilo mahakama kubwa zaidi duniani lililojengwa kwa miaka mitatu na kuchukua eneo la hekta 12.
Tanzania yaacha riba ya 6% ili kukabiliana na soko la Kimataifa
Chanzo cha picha, BOT
Benki Kuu ya Tanzania siku ya Ijumaa ilitangaza kuacha kiwango chake cha riba ya msingi cha asilimia 6% bila mabadiliko, ikisema kuwa ingawa mfumuko wa bei uko chini ya udhibiti, mvutano wa biashara duniani unaweka uchumi kwenye hatari.
Hii ilikuwa ni mara ya nne mfululizo kwa mkutano kuhusu sera za fedha ambapo kiwango hicho kimebakia bila kubadilika.
"Kuweka kiwango cha riba ya benki kuu kutasaidia kupunguza athari hasi za vikwazo vya biashara na migogoro ya kisiasa duniani," alisema Naibu Gavana wa Benki Kuu Yamungu Kayandabila wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Wiki hii Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza ushuru mpya na mkubwa wa forodha ambao umesababisha kushuka kwa masoko ya fedha duniani na kulaaniwa na viongozi wengine wanaokabiliana na mwisho wa enzi ya miongo mingi ya biashara huria.
Benki Kuu ya Tanzania inalenga mfumuko wa bei wa asilimia 5%, na mfumuko wa bei wa bidhaa za walaji ni wastani wa karibu asilimia 3% tangu ilipoanzisha kiwango chake cha sera mnamo Januari 2024.
Uchumi wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki unatarajiwa kukua kwa takriban asilimia 6% mwaka huu, kutoka makadirio ya asilimia 5.4% mwaka 2024, kwa mujibu wa waziri wa fedha na gavana wa benki kuu waliotoa taarifa hiyo Novemba mwaka jana.
Kayandabila alisema kuwa akiba ya fedha za kigeni ya nchi hiyo ilikuwa takriban dola bilioni 5.6, kiasi kinachotosha kuagiza bidhaa kwa kipindi cha miezi minne na nusu hadi mitano mfululizo.
Muuaji wa Urusi yuko tayari kukiri mauaji mengine 11
Chanzo cha picha, Reuters
Alexander Pichushkin, muuaji hatari wa Urusi aliyefungwa maisha mwaka 2007 kwa
kuua watu 48, amesema yuko tayari kukiri mauaji mengine 11, idara ya mahakama
ya Urusi ilisema Jumamosi.
Kwa mujibu wa Reuters Pichushkin, ambaye sasa ana umri wa
miaka 50, alilenga mara nyingi watu wasio na makazi, walevi na wazee, karibu na
Bitsevsky Park, mahali penye mandhari ya kijani kibichi kusini mwa Moscow.
Mauaji hayo yalifanyika katika kipindi cha kutoka 1992 hadi
2006.
Alipewa jina la utani "muuaji wa chessboard" na
vyombo vya habari vya Urusi kwa sababu aliwaambia wapelelezi katika kukiri
kwake kwamba alikuwa na mpango wa kuweka sarafu kwenye kila ubao wa kila muathirika
wa vitendo vyake.
Pichushkin amekuwa akishikiliwa katika gereza la Polar Owl,
katika eneo la Arctic kaskazini mwa Urusi, tangu ahukumiwe.
Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa Telegram siku
ya Jumamosi, Idara hiyo ya Urusi ilisema kuwa Pichushkin aliwaambia wapelelezi
kuwa yuko tayari kukiri mauaji 11 zaidi ya wanaume na wanawake.
Pichushkin kwa muda mrefu amekuwa akishukiwa kwa mauaji zaidi
ya yale ambayo alihukumiwa.
Wakati wa kesi yake alidai kuua watu 63, lakini waendesha
mashtaka walimshtaki kwa mauaji 48 na majaribio matatu ya kuua.
Visiwa vya Falkland navyo vyahisi maumivu ya ushuru wa Marekani
Chanzo cha picha, Getty Images
Ushuru mkubwa uliotangazwa na rais wa Marekani Donald Trump
sio tu unaathiri uchumi wa nchi zenye Uchumi mkubwa kama Uingereza na Canada – Uchumi
mdogo pia zinahisi hivyo, ikiwa ni pamoja na Visiwa vya Falkland.
Idadi ya watu isiyo zidi 3,700 wanaishi kwenye visiwa vya
mbali vya Atlantiki Kusini.
Sasa wanatazamia athari ya ushuru wa 42%.
Janet Robertson, meneja mkuu wa kampuni ya Consolidated
Fishing Limited, anaiambia BBC World Service kwamba Marekani ni soko kuu la bidhaa
zake.
"Tunashangaa yote yataishia wapi," Janet anasema.
Uvuvi "kwa sasa ni sekta muhimu zaidi katika visiwa vya
Falklands", anaongeza.
"Uuzaji wa bidhaa zitokanazo na Samaki katika taifa la
Marekani umekuwa na mchango mkubwa, ambapo kwa kiasi fulani ndiyo sababu
tumeishia kuwekewa ushuru huu mkubwa kulingana na viwango vya ushuru visivyo vya
kawaida ambavyo vimebuniwa na Marekani.’’
Maandamano ya kumpinga Trump yanatarajiwa Marekani na London
Chanzo cha picha, PA Media
Wakati waziri mkuu wa Uingereza akijipanga kuhusu namna ya
kukabiliana na ushuru wa Trump, umati wa watu unakusanyika kote Marekani kuandamana.
Maandamano yamepangwa kufanyika katika majimbo yote 50 na
Washington DC leo, huku watu wakiazimia kumpinga Rais Donald Trump na sera
zake.
Kumekuwa na maandamano ya mara kwa mara tangu aingie
madarakani, lakini waandaaji wanasema wanatarajia leo kuwa siku moja kubwa
zaidi ya maandamano tangu Trump aanze muhula wake wa pili.
Makumi kwa maelfu ya Wamarekani wanatarajiwa kushiriki
katika matukio nchini kote - na kuna maandamano yaliyopangwa London na miji
mingine ya Canada na Ulaya pia.
Wakati huo huo waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer anaripotiwa kutumia wikendi hii kuzungumza na viongozi wa kigeni kuhusu hatua ya ushuru.
Tayari alizungumza na wenzake wa Australia na Italia jana usiku.
Downing Street inasema viongozi wote watatu walikubaliana kwamba "vita vya biashara vya pande zote vitasababisha hasara kubwa sana".
Kwa mujibu wa ofisi hiyo maafisa wa Uingereza "wataendelea kwa utulivu na kazi ya maandalizi, badala ya kukimbilia kulipiza kisasi".
Watoto ni miongoni mwa watu 18 waliouawa katika shambulio la Urusi dhidi ya mji wa Kryvyi Rih
Chanzo cha picha, Ukrainian presidency
Shambulio la kombora lililotekelezwa na Urusi katika mji wa
Kryvyi Rih ulio katikati mwa Ukraine limeua takriban watu 18 na kujeruhi makumi, maafisa wa Ukraine wamethibitisha.
Tisa kati ya waliofariki ni watoto, alisema Rais Volodymyr
Zelensky, ambaye alikulia katika mji huo wa Kryvyi Rih.
Maafisa wa eneo hilo walisema kuwa kombora lilipiga eneo la
makazi ya watu.
Picha zilionyesha mtu mmoja akiwa amelala kwenye uwanja wa
michezo, huku video ikionyesha eneo kubwa la jengo la ghorofa 10 likiwa limeharibiwa
na waathiriwa wakiwa wamelala barabarani.
Wizara ya ulinzi ya Urusi baadaye ilidai "shambulio la
kombora lililotekelezwa kwa umahiri wa
hali ya juu" lililenga mkutano wa "makamanda wa vitengo na wakufunzi
wa mataifa ya Magharibi" katika mkahawa, na kukadiria kuwaua 85.
Hata hivyo haikutoa ushahidi wowote.
Jeshi la Ukraine lilijibu kwa kusema kuwa Urusi inaeneza
habari za uongo kwa kujaribu "kuficha uhalifu wake".
Ilisema kuwa
Moscow ilirusha kombora la aina ya Iskander-M ili kusababisha madhara na hasara.
Shambulio hilo,
mapema Ijumaa jioni, lilikuwa miongoni mwa mashambulizi mabaya zaidi kulenga
mji wa Kryvyi Rih tangu kuanza kwa uvamizi kamili wa Urusi mnamo 2022, na
linakuja wakati Rais wa Marekani, Donald Trump akishinikiza kusitishwa kwa
mapigano.
Zelensky
aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii kwamba takriban majengo matano
yameharibiwa katika shambulizi la ijumaa: "Kuna sababu moja tu kwa nini hali
hii inaendelea: Urusi haitaki usitishaji wa mapigano, na tunashuhudia."
Machungu ya ushuru mpya wa Trump yaanza kuonekana kwenye masoko ya hisa ya kimataifa
Chanzo cha picha, Getty Images
Masoko ya hisa nchini Marekani yamehitimisha wiki yao mbaya zaidi tangu 2020, huku viwango vikubwa vya ushuru wa Donald Trump vikiendelea kusababisha taharuki kwenye masoko ya kimataifa.
Viashiria vyote vikuu vya Wall Street vimeanguka kwa zaidi ya 5%.
Trump, kwa upande mwingine, amesisitiza tena kwamba ushuru kwa bidhaa zinazoingia Marekani uta ‘’imarisha" uchumi wa Marekani.
Baadhi ya ushuru sasa umeanza kutumika - na "bei ya msingi" ya 10% ikipitumika kwa bidhaa kutoka Uingereza na mataifa mengine mengi.
Hayo yanajiri wakati huu kampuni ya kemikali Uingereza ikisema ushuru unaweza kuzuia washindani wa bei nafuu.
Kemikali za asili ni moja ya bidhaa kubwa zinazoingizwa kutoka Uingereza hadi Marekani, zikiambatana na jumla ya karibu £3 bilioni kwa mwaka jana.
Kemikali hizi hutumika katika sekta mbalimbali kubwa, kuanzia kwenye chakula hadi vipodozi, injini, na kilimo.
Badala ya kuhofia ushuru wa Marekani, kampuni ya Robinsons Brothers inadhani kuwa huenda ushuru huu ukasaidia kampuni ya kemikali za asili kurejesha wateja wa Marekani kutoka kwa washindani wa bei nafuu kutoka nje ya nchi.
Chini ya utawala mpya wa Trump, bidhaa kutoka China zitakabiliwa na ushuru wa 34%, wakati bidhaa kutoka India zitatozwa ushuru wa 27%.