Wafungwa wa Kipalestina walioachiliwa wawasili Ukingo wa Magharibi baada ya Hamas kuwaachilia mateka

Basi lililokuwa limebeba wafungwa wa Kipalestina walioachiliwa limewasili katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa , baada ya kutoka katika gereza la Ofer la Israel.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Dinah Gahamanyi

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya mubashara kwa leo, tukutane tena hapo kesho.

  2. Man Utd imemsajili kijana mwenye umri mdogo Heaven kutoka Arsenal

    g

    Chanzo cha picha, Manchester United

    Maelezo ya picha, Ayden Heaven aliwahi kucheza West Ham kabla ya kujiunga na akademi ya Arsenal

    Manchester United imemsajili beki wa timu ya taifa ya Uingereza Ayden Heaven kutoka Arsenal kwa mkataba wa miaka minne na nusu.

    The Red Devils wanasema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18, ambaye aligharimu ada ya fidia ambayo haijatajwa, mara moja atajiunga na kikosi cha kwanza.

    Kijana huyo alijiunga na Arsenal akiwa na umri wa miaka 13 mnamo 2019 na akacheza kwa mara ya kwanza kama mchezaji wa akiba katika ushindi wa Kombe la EFL huko Preston mnamo mwezi Oktoba.

    "Ninajivunia sana kujiunga na Manchester United. Ninashukuru kwa kila mtu ambaye alisaidia kutimiza ndoto hii," alisema.

    "Kuna mengi ambayo nataka kufikia kwenye mchezo, nitakuwa nikitoa kila kitu ili kuendeleza maendeleo yangu na kuwa mchezaji bora zaidi ninayeweza kuwa."

    Mkurugenzi wa ufundi wa Manchester United Jason Wilcox alisema: "Tunafuraha kwamba Ayden amejiunga na Manchester United. Tayari ni beki mwenye kipaji cha hali ya juu ambaye yuko tayari kujiunga na kikosi chetu cha kwanza ili kuongeza maendeleo yake.

    "Klabu hii ina rekodi ya kipekee ya kusaidia wachezaji wachanga na tunaamini kwamba Ayden yuko mahali pazuri kufikia uwezo wake bora."

    Heaven ni mchezaji wa pili kijana kujiunga na United kutoka Arsenal msimu huu baada ya mshambuliaji Chido Obi-Martin mwenye umri wa miaka 17 kuhamia kaskazini mwezi Oktoba.

  3. Vita vya Ukraine: Watu 7 waliuawa na wengine kujeruhiwa Poltava Ukraine

    g

    Chanzo cha picha, @dsns_telegram

    Watu 3 waliuawa na wengine 10 walijeruhiwa kutokana na mgomo wa Poltava, ikiwa ni pamoja na mtoto mmoja.

    Huko Poltava, kombora la Urusi liligonga jengo la makazi: mlango kutoka kwa ghorofa ya 1 hadi ya 5 uliharibiwa, moto ulizuka, Huduma ya Dharura ya Jimbo la Ukraine iliripoti. Aidha, kwa mujibu wa waokoaji, nyumba za jirani na magari 12 yaliharibiwa.

    Kwa mujibu wa takwimu za hivi punde, watu watatu waliuawa na wengine kumi kujeruhiwa, akiwemo mtoto mmoja.

    Shughuli za uokoaji wa dharura zinaendelea.

    g

    Chanzo cha picha, @dsns_telegram

    g

    Chanzo cha picha, @dsns_telegram

    Vita vya Ukraine: soma zaidi

    • YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
    • UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
    • UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
    • KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
    • ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
    • PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
  4. Takriban watu 700 wameuawa katika vita vya DRC tangu Jumapili - UN

    h

    Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/Shutterstock

    Umoja wa Mataifa unasema kuwa takriban watu 700 wameuawa katika mapigano makali huko Goma, mji mkubwa zaidi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, tangu Jumapili.

    Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric anasema watu 2,800 walijeruhiwa wakati kundi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda lilipochukua mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini.

    Wapiganaji hao sasa wanasemekana kuelekea kusini kuelekea mji wa Bukavu, mji mkuu wa Kivu Kusini.

    Migogoro mashariki mwa Kongo ilianza miaka ya 1990, lakini imeongezeka sana katika wiki za hivi karibuni.

    Vuguvugu la M23 linaloundwa hasa na Watutsi, linasema kuwa linapigania haki za walio wachache, huku serikali ya Congo ikisema kuwa vuguvugu hilo linaungwa mkono na Rwanda, kutaka kudhibiti eneo hilo la mashariki lenye utajiri wa madini.

  5. Wafungwa wa Kipalestina walioachiliwa wawasili Ukingo wa Magharibi baada ya kuachiliwa na Hamas

    Wafungwa wa Kipalestina wamewasili kwa basi katika Ukingo wa Magharibi.

    Kivuko hicho - ambacho Gaza inakiita "lango lake kwa ulimwengu" - kimefungwa kwa raia tangu Mei 2024.

    Umati wa watu ulikusanyika huku wafungwa wa Kipalestina wakiachiliwa.

    Umati wa watu ulikusanyika karibu na basi wakati wafungwa wakitoka nje ya gari.

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    h

    Chanzo cha picha, Reuters

    Reuters

    Chanzo cha picha, Reuters

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Wagonjwa wapelekwa Misri

    Baada ya kupokelewa kundi la kwanza la Wapalestina waliojeruhiwa wanaohitaji matibabu wamehamishwa hadi Misri kutoka Gaza baada ya kufunguliwa tena kwa kivuko cha mpaka cha Rafah kusini mwa ardhi hiyo.

    Wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas inasema wagonjwa 50 wameondoka Gaza hadi Misri kupitia kivuko ili kupata huduma za matibabu.

    Soma zaidi:

  6. Tunayofahamu kuhusu mateka wa Israel walioachiliwa na Hamas

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Wanaume watatu wa Israel waliopaswa kuachiliwa leo wote wameachiliwa huru na Hamas.

    Watu hao wameelezewa kama:

    Yarden Bibas , 34, ambaye wanawe wawili ndio mateka wachanga zaidi waliochukuliwa na Hamas tarehe 7 Oktoba 2023, aliachiliwa mapema leo asubuhi katika mji wa kusini wa Khan Younis. Mkewe Shiri, 33, na wanawe wawili - Ariel, watano, na Kfir, wawili - bado hawajaachiliwa huku jeshi la Israel likisema "wanajali sana" kuhusu ustawi wao.

    Ofer Kalderon , 53, Mfaransa-Israeli, pia aliachiliwa huko Khan Younis leo. Alichukuliwa kutoka Nir Oz pamoja na watoto wake wawili, Erez na Sahar - watoto wote wawili waliachiliwa mnamo Novemba 2023 kama sehemu ya usitishaji vita wa muda wa mapema. Rais wa Ufaransa Macron amekaribisha kuachiliwa kwake.

    Keith Seigel , mwenye umri wa miaka 65, raia wa Marekani-Israel, alichukuliwa na Hamas pamoja na mkewe Adrienne, anayejulikana pia kama Aviva, kutoka nyumbani kwao huko Kfar Aza. Adrienne aliachiliwa mnamo Novemba 2023.

    mateka hao watatu wameachiliwa kwa kubadilishana zaidi ya wafungwa 180 wa Kipalestina, ambao wanatarajiwa kuachiliwa baadaye leo.

    Soma zaidi:

  7. Habari za hivi punde, Tazama: Mateka watatu wa Israel wakabidhiwa kwa Msalaba Mwekundu huko Khan Younis

    Maelezo ya video, Mateka wawili wa Israel wakabidhiwa kwa Msalaba Mwekundu huko Khan Younis

    Mateka wawili wa Israeli wamekabidhiwa kwa Shirika la Msalaba Mwekundu katika hafla iliyoratibiwa sana huko Khan Younis. Ofer Kalderon, 53, na Yarden Bibas, 34, walikuwa miongoni mwa mateka waliopelekwa Gaza na Hamas wakati wa mashambulizi ya Oktoba 7.

    Ni mara ya nne kuachiliwa huru kwa mateka tangu mkataba wa kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas uanze tarehe 19 Januari.

    Kwa kubadilishana Israel baadaye itawaachilia zaidi ya Wapalestina 180 ambao wamekuwa wakishikiliwa katika jela za Israel.

  8. Watu si waliokuwa ndani ya ndege ya matibabu wafariki Philadelphia

    h

    Chanzo cha picha, Mwakilishi wa Pennsylvania Jared Solomon

    Ndege ndogo ya usafiri wa kimatibabu imeanguka katika majengo kadhaa kaskazini-mashariki mwa Philadelphia, na kuteketeza kwa moto nyumba na magari na kujeruhi watu waliokuwa ardhini.

    Ndege hiyo ilikuwa katika shughuli ya usafiri wa kimatibabu siku ya Ijumaa jioni na ilikuwa imewabeba wafanyakazi wanne, mgonjwa mtoto na wasindikizaji wa mgonjwa, Jet Rescue Air Ambulance, kampuni ya matibabu ya ndege, ilisema katika taarifa.

    "Tunajua kuwa kutakuwa na hasara," Gavana wa Pennsylvania Josh Shapiro alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika eneo la ajali, na kuiita "janga kubwa la anga".

    Wahudumu wa dharura walikimbilia eneo la ajali jioni huku wakazi wakijaa kwenye mitaa iliyojaa vifusi na vipande vya ndege hiyo.

    Walioshuhudia walielezea tukio la kutisha na watu walijeruhiwa na majengo kuteketea.

    Ndege hiyo ilikuwa imembeba mtoto ambaye alikuwa akipokea matibabu nchini Marekani kutokana na hali yake ya kutishia maisha na alikuwa akirejea Tijuana, Mexico, Shai Gold, msemaji wa Jet Rescue Air Ambulance, alikiambia kituo cha habari cha NBC .

    Msichana huyo aliandamana na mama yake, rubani, rubani, daktari na mhudumu wa afya, msemaji huyo alisema.

    Soma zaidi:

  9. Baba wa mateka mdogo miongoni mwa wanaume watatu watakaoachiliwa Jumamosi, Hamas yasema

    g

    Chanzo cha picha, Family handout

    Maelezo ya picha, Yarden Bibas akiwa na mkewe Shiri na watoto wao wawili, Ariel na Kfir

    Kundi la wapiganaji la Palestina Hamas limetoa majina matatu ya mateka ambalo linasema litawaachilia Jumamosi chini ya makubaliano ya kusitisha mapigano na Israel.

    Ni Waisraeli Ofer Kalderon, 53, na Yarden Bibas, 34, na Mmarekani-Israel Keith Siegel, 65.

    Bw Bibas ndiye babake Kfir, mateka mdogo zaidi ambaye alikuwa na umri wa miezi 10 alipotekwa nyara na Hamas. Mkewe Shiri na mwana wao mwingine Ariel, wanne, pia walitekwa.

    Ofisi ya waziri mkuu wa Israel imesema Israel imepokea orodha ya watu waliotekwa nyara.

    Israel itaachilia huru kundi jingine la wafungwa wa Kipalestina.

    Itakuwa ni mara ya nne ya kubadilishana mateka kwa wafungwa tangu usitishaji mapigano ulipoanza kutekelezwa tarehe 19 Januari.

    Baadhi ya mateka 251 walichukuliwa na Hamas iliposhambulia Israel tarehe 7 Oktoba 2023, na kuua takriban watu 1,200.

    Shambulio hilo lilizusha vita ambavyo vimeharibu Gaza. Mashambulizi ya kijeshi ya miezi 15 ya Israel yaliwauwa Wapalestina 47,460 katika eneo hilo, kulingana na wizara ya afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas.

    Soma zaidi:

  10. Ufaransa kupendekeza azimio la Umoja wa Mataifa la 'kuongeza shinikizo kwa Rwanda' kuhusu mzozo wa DRC

    h

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Balozi wa Ufaransa wa Umoja wa Mataifa Nicolas de Riviere

    Ufaransa itapendekeza rasimu ya azimio kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambayo inalenga "kuongeza shinikizo kwa Rwanda" kuondoa wanajeshi wake mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Balozi wa Ufaransa wa Umoja wa Mataifa Nicolas de Riviere amesema.

    "Natumai azimio hili linaweza kupitishwa hivi karibuni," alisema, akiongeza kuwa hafikirii azimio hilo lingetishia vikwazo vyovyote katika hatua hii.

    "Tunachohitaji ni ujumbe mzito na wa wazi wa Baraza la Usalama katika mfumo wa azimio, unaohimiza hatua ya sasa kusitisha na kuhimiza uondoaji wa wanajeshi wa kigeni, na kutaka kuanzishwa tena kwa mazungumzo," de Riviere aliongeza.

    Rasimu ikishasambazwa kwa wajumbe 15, baraza litajadili lugha kabla ya kura kuratibiwa. Azimio la baraza hilo linahitaji angalau kura tisa za kuunga mkono na hakuna kura ya turufu ya Marekani, Urusi, Uchina, Uingereza au Ufaransa kupitishwa.

    Ujumbe wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa ulisema baadaye Ijumaa kwamba ili kuunga mkono juhudi za upatanishi, Ufaransa pia ilikuwa katika "mawasiliano ya karibu na washirika wake katika Umoja wa Mataifa huko New York ili kuhimiza kuanzishwa tena kwa mazungumzo kati ya DRC na Rwanda, yaliyowezeshwa na Angola ndani ya Umoja wa Mataifa- yanayofahamika kama mchakato wa Luanda."

    Unaweza pia kusoma:

  11. Hujambo na karibu kwa matangazo haya ya mubashara ya Jumamosi tarehe 01.02.2025