Shambulio la Israel kaskazini mwa Gaza ladokeza mpango wa jenerali mstaafu wa "kujisalimisha au kufa njaa" kwa ajili ya vita

Ujumbe umetumwa kwenye mitandao ya kijamii na msemaji wa Kiarabu wa jeshi la Israel akiwaonya watu wanaoishi katika eneo la 'D5' kaskazini mwa Gaza kuhamia kusini.

Muhtasari

  • Harris atoa rekodi ya vipimo vya afya yake
  • Lupita Nyong'o alaani ukandamizaji wa 'kutisha ' Kenya
  • Hezbollah yawaonya Waisraeli kukaa mbali na maeneo ya kijeshi
  • Mamia ya Land Rover kuandikisha rekodi mpya Tanzania
  • Tazama: Mnara wa Kanisa Katoliki la kihistoria ukianguka wakati lilipoteketeza kwa moto
  • Mwanamke afungwa jela kwa kuwaua wazazi wake na kuficha miili
  • Mashambulizi ya Israel yawauwa takriban watu 20 kaskazini mwa Gaza, huku IDF likiwaamrisha watu zaidi kuhama

Moja kwa moja

Na Dinah Gahamanyi

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya mubashara kwa leo, tukutane tena hapo kesho majaaliwa.

  2. Shambulio la Israel kaskazini mwa Gaza ladokeza mpango wa jenerali mstaafu wa "kujisalimisha au kufa njaa" kwa ajili ya vita.

    f

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Wapalestina na mashirika ya misaada yanashuku kuwa Israel inatumia mbinu ya mkakati mpya kaskazini mwa Gaza

    umamosi asubuhi, ujumbe ulitumwa kwenye mitandao ya kijamii na msemaji wa Kiarabu wa jeshi la Israel akiwaonya watu wanaoishi katika eneo la 'D5' kaskazini mwa Gaza kuhamia kusini.

    Majengo ya D5 ni ya mraba yaliyoko kwenye ramani za Gaza na Jeshi la Ulinzi la Israeli (IDF). Majengo haya ni kizuizi ambacho kimegawanywa katika maeneo kadhaa madogo.

    Ujumbe huo ambao ni wa hivi punde zaidi katika mfululizo, ulisema: "IDF inafanya kazi kwa nguvu kubwa dhidi ya mashirika ya kigaidi na itaendelea kufanya hivyo kwa muda mrefu. Eneo lililotengwa, ikiwa ni pamoja na makazi yaliyoko huko, linachukuliwa kuwa eneo hatari la mapigano. Wakazi wa eneo hilo zima wahamishwe mara moja kupitia Barabara ya Salah al-Din hadi eneo la kibinadamu."

    Eneo la kibinadamu lililoteuliwa na Israel katika ujumbe huo ni al-Mawasi, ambalo hapo awali lilikuwa eneo la kilimo kwenye pwani karibu na Rafah. Iimejaa watu wengi na halina usalama zaidi kuliko sehemu nyingine nyingi za Gaza.

    BBC Verify imefuatilia na kuthibitisha angalau mashambulizi 18 ya anga katika eneo hilo.

    Unaweza pia kusoma:

  3. Harris atoa rekodi ya vipimo vya afya yake

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Mgombea wa urai wa Kidemocrat Kamala Harris ni mwenye "afya bora" na "ana uthabiti wa mwili na kiakili" unaohitajika kuhudumu kama rais, daktari wake alisema katika barua.

    Katika barua hiyo iliyoandikwa na daktari wa Harris Joshua Simmons, anasema makamu wa rais ana historia ya mizio ya msimu na urticaria (hali ya kawaida ya ngozi).

    Simmons anasema mizio yake "imedhibitiwa vyema" na dawa za dukani ikiwa ni pamoja na dawa ya pua, matone ya macho na Allegra (kidonge cha mzio), lakini kwamba hahitaji tena mara nyingi baada ya miaka mitatu ya kinga ya allergen.

    Hakuwahi kupata "dalili kali", anasema.

    Kwa nini Harris alitoa rekodi zake za matibabu?

    Huku ikiwa imesalia chini ya mwezi mmoja kabla ya siku ya uchaguzi, Harris anatumai ufichuzi wake wa matibabu utaweka shinikizo kwa mpinzani wake, Trump.

    Trump, mwenye umri wa miaka 78, na Warepublican mara nyingi wamekuwa walimshambulia Rais Joe Biden, mwenye umri wa miaka 81, kama mzee sana mara nyingi akimtaka afanye vipimo vya utambuzi wa afya yake.

    Lakini kwa kuwa Harris ndiye mteule, Wanademokrasia wanatumai kubadilisha meza, wakitaka kutilia shaka umri wa Trump na kufaa kwa kazi hiyo.

  4. Lupita Nyong'o alaani ukandamizaji wa 'kutisha ' Kenya

    h

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Muigizaji Lupita Nyong'o amelaani hatua ya mamlaka ya Kenya dhidi ya maandamano makubwa ya kupinga ushuru yaliyoanza mwezi Juni.

    Waandamanaji walikabiliwa na ukatili wa polisi, kulingana na mashirika ya haki za binadamu , na makumi ya watu waliuawa na wengine wengi kutekwa nyara.

    Bi Nyong'o, ambaye baba yake alifungwa jela na kuteswa chini ya utawala wa rais wa zamani, Daniel arap Moi, ameiambia BBC: "Inashangaza kujua kwamba serikali hii inatumia mbinu ambazo nilidhani ziliachwa hapo awali."

    Katika jibu lake serikali ilisema haiwezekani kulinganisha tawala mbili "tofauti sana" na kwamba "inajutia kifo chochote kilichotokea".

    Lakini Nyong'o, mshindi wa tuzo ya Oscar ambaye alikulia nchini Kenya lakini kwa sasa anaishi nchini Marekani, amesema jinsi serikali inavyoshughulikia maandamano "inasikitisha".

    "Kadiri mambo yanavyobadilika, ndivyo yanavyoendelea kuwa yalivyo... sijui hadithi hii inaishaje," alisema Nyong'o, ambaye ameigiza katika filamu za Hollywood kama vile 12 Years a Slave na Black Panther, wakati wa mahojiano kuhusu posikasti yake mpya.

    "Ninashukuru sana vijana ambao wako mstari wa mbele kupigania Kenya tofauti," Lupita Nyong'o alisema kuhusu waandamanaji wa kizazi hiki.

    Msemaji wa serikali ya sasa ya Kenya, Isaac Mwaura, aliiambia BBC kwamba mamlaka "zinalishirikiana sana na waandamanaji na walikubali matakwa hayo, ikiwa ni pamoja na rais kutoidhinisha mswada wa fedha". Ilikuwa hatua za ushuru zenye utata katika muswada huo ndizo zilizua matatizo.

    g

    Chanzo cha picha, Lupita Nyong'o

    Maelezo ya picha, Lupita Nyong'o alizaliwa Mexico baada ya baba yake (pichani) mama na dada yake kutoroka Kenya enzi ya utawala wa rais wa zamani Daniel Arap Moi

    Baba yake Lupita, Anyang' Nyong'o, kwa sasa ni gavana wa kaunti nchini Kenya na kaimu kiongozi wa vuguvugu la Orange Democratic Movement (ODM), mojawapo ya vyama vikuu vya kisiasa nchini Kenya.

    Kuhusu ripoti kwamba watu waliuawa wakati wa maandamano hayo, Mwaura alisema: "Ni takwimu za polisi pekee ndizo rasmi. Serikali inajutia kifo chochote kilichotokea wakati wa maandamano hayo na yeyote ambaye huenda alisababisha hayo atawajibishwa kwa kufuata sheria."

  5. Hezbollah yawaonya Waisraeli kukaa mbali na maeneo ya kijeshi

    h

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Hezbollah imetoa onyo kwa Waisraeli kukaa mbali na maeneo ya kijeshi kaskazini mwa Israel, ili kuokoa maisha yao.

    Taarifa hiyo inasema jeshi la Israel liliweka kambi zake ndani ya maeneo ya makazi kaskazini mwa nchi, ambayo ilisema yanalengwa na makombora na ndege zake zisizo na rubani.

    Hezbollah imekuwa ikirusha makombora kila siku kaskazini mwa Israel.

    Mashambulizi ya anga ya Israel katika kipindi cha wiki tatu zilizopita nchini Lebanon yanaaminika kuwaua makumi ya viongozi wa Hezbollah, na tangu wakati huo, taarifa za kundi hilo zimekuwa chache.

    Onyo hili kwa Waisraeli kwamba wanapaswa kukaa mbali na vituo vya jeshi katika miji ya kaskazini linaweza kuwa na nia ya kuwakumbusha wafuasi wa Hezbollah kwamba bado ina uwezo wa kuleta uharibifu mkubwa.

    Inaangazia shutuma za Israel dhidi ya Hezbollah kwamba inaficha wapiganaji wake na silaha katika maeneo ya raia.

    Hezbollah pia iliionya kuwa Israel imeshuhudia mashambulio yake machache tu . Bado haijabainika ni kiasi gani cha silaha zao kimeharibiwa na mashambulizi ya hivi majuzi ya Israel.

    Unaweza pia kusoma:

  6. Mamia ya Land Rover kuandikisha rekodi mpya Tanzania,

    Madereva wa magari ya aina ya Land Rover kutoka nchini mbalimbali wamekusanyika Arusha, kaskazini mwa Tanzania katika tamasha maalumu lenye lengo la kuvunja rekodi mpya ya Dunia.

    Tamasha hilo la siku tatu, limeanza leo na kutarajiwa kutamatika siku ya Jumatatu Oktoba 14.

    Hii leo shughuli zilianza mpema asubuhi eno la Kingori nje kidogo ya jiji la Arusha kwa kusanyiko la magari hayo mpakani mwa mkoa wa Kilimanjaro na Arusha ambapo kila gari ilibandikwa namba yake ya ushiriki na baadae msafara ulianza na polepole na kwa shamra shamra nyingi ulikitaza maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha ambapo wakazi walifurika kushuhudia.

    Rekodi ya sasa ya Dunia ya mkusanyiko wa magari mengi ya Land Rover kwa mujibu wa kitabu cha Guinness ni ya mwaka 2018 inashikiliwa na jimbo la Bavaria nchini Ujerumani ambapo magari 632 yalijitokeza na kutengeneza msafara uliofika umbali wa kilometa 7.4.

    f

    Chanzo cha picha, Eagan Salla/BBC

    Eagan Salla/BBC

    Chanzo cha picha, Eagan Salla/BBC

    Eagan Salla/BBC

    Chanzo cha picha, Eagan Salla/BBC

    f

    Chanzo cha picha, Eagan Salla/BBC

    Eagan Salla/BBC

    Chanzo cha picha, Eagan Salla/BBC

    Eagan Salla/BBC

    Chanzo cha picha, Eagan Salla/BBC

    Eagan Salla/BBC

    Chanzo cha picha, Eagan Salla/BBC

  7. Tazama: Mnara wa Kanisa Katoliki la kihistoria ukianguka wakati lilipoteketeza kwa moto

    Maelezo ya video, Tazama mnara wa kanisa la kihistolia la Chile lililoteketea kwa moto ukiporomoka

    Video inaonyesha tukio la kushangaza wakati ambapo kanisa la kihistoria huko Iquique, Chile, lilipoharibiwa kwa moto. Vikosi 12 vya kuzima moto vilifika kukabiliana na moto huo huo katika Kanisa la San Francisco siku ya Ijumaa, lakini hawakuweza kuliokoa, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

    Lilikuwa kanisa la kwanza la Kikatoliki kujengwa nchini, kwa mujibu wa Hazina ya Makumbusho ya Dunia, na lilitangazwa kuwa mnara wa kitaifa mwaka wa 1994.

    Maafisa wa eneo hilo walisema kwamba hakukuwa na vifo, na kwamba sababu ya moto ilikuwa bado inachunguzwa..

  8. Mwanamke afungwa jela kwa kuwaua wazazi wake na kuficha miili yao

    h

    Chanzo cha picha, Essex Police

    Maelezo ya picha, Virginia McCullough aliishi kando ya miili ya wazazi wake kwa miaka minne

    Mwanamke "mdanganyifu" ambaye aliwaua wazazi wake na kuishi kando ya miili yao kwa miaka minne katika nyumba ya familia yao amefungwa kifungo cha maisha jela nchni Uingereza.

    Mabaki ya miili ya Lois mwenye umri wa miaka 71 na John McCullough, wenye umri wa miaka 70, yalipatikana kwenye mifuko ya kulalia nyumbani kwao huko Great Baddow, Essex, mnamo mwezi Septemba 2023.

    f

    Chanzo cha picha, Family handout

    Maelezo ya picha, Miili ya Lois na John McCullough ilikuwa imefichwa katika sehemu tofauti za nyumba yao, ikiwa imefichwa kwenye mifuko ya kulalia.

    Mtoto wao Virginia McCullough, 36, alikiri kumuua babake kwa sumu na kumuweka kwenye "kaburi la kujitengenezea nyumbani",na kumuua mama yake kwa kisu mnamo Juni 2019.

    Mshtakiwa, huyo ambaye aliwaambia polisi "jipeni moyo, angalau mmemkamata mtu mbaya", atalazimika kutumikia kipindi cha chini cha miaka 36 kabla ya kuangalia uwezekano wa kuachiliwa au la.

  9. Mashambulizi ya Israel yawauwa takriban watu 20 kaskazini mwa Gaza, huku IDF likiwaamrisha watu zaidi kuhama

    h

    Chanzo cha picha, Reuters

    Takriban watu 20 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mashambulio ya Israeli katika eneo la Jabalia kaskazini mwa Gaza Ijumaa usiku, shirika la habari la Reuters, limewanukuu madaktari wakisema.

    Shirika la madaktari wasio na mipaka (MSF) linasema kuwa maelfu ya watu wamekwama katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia.

    Katika chapisho la X, mratibu wa mradi wa MSF Sarah Vuylsteke anasema "hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia au kutoka".

    Naye dereva wa MSF Haydar, ambaye pia amekwama katika kambi hiyo, anasema "Naogopa kubaki, na pia ninaogopa kuondoka".

    Vikosi vya Israel vilianza mashambulizi katika eneo hilo wiki moja iliyopita, vikisema vinalenga kuwazuia Hamas kujipanga upya.

    Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, watu 61 waliuawa katika mashambulizi ya jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaza siku ya Ijumaa. Madaktari pia walitoa idadi sawa na hiyo ya vifo.

    kaimu mkurugenzi wa Hospitali ya Al Awda huko Jabalia Dkt Mohammed Salha, amekiambia kipindi cha BBC Newshour kuwa eneo la Jabalia limezingirwa kwa siku saba.

    Israel imekuwa ikifanya operesheni mpya ya ardhini katika eneo hilo, ikilenga kukabiliana upya na wapiganaji wa Hamas.

    Anasema hospitali hiyo itaishiwa na mafuta kwani wanajeshi wa Israel "wanaitenga Jabalia na eneo lote la Gaza".

    Dkt Salha ameongeza kuwa Waisraeli wanawashinikiza watu kaskazini mwa Gaza kuondoka. "Hakuna dawa, hakuna vifaa vya matibabu, hakuna maji safi, hakuna mafuta, kwa hivyo ni shinikizo, shinikizo kwa watu hawa kuhama na kwenda moja kwa moja kusini."

    Unaweza pia kusoma:

  10. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya mubashara ya leo, ikiwa ni Jumamosi tarehe 12.10.2024