Kwaheri
Asante sana kwa kufuatilia matangazo yetu ya moja kwa moja leo.
Unaweza pia kuendelea kuzisoma taarifa zetu kupitia Chaneli yetu ya WhatsApp kwa kubofya hapa.
Tukutane tena kesho panapo majaaliwa .
Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Makumi ya watu wamejeruhiwa katika shambulizi la Israel dhidi ya mji mkuu wa Lebanon huku makabiliano ya mpakani yakiongezeka.
Asha Juma, Ambia Hirsi & Lizzy Masinga
Asante sana kwa kufuatilia matangazo yetu ya moja kwa moja leo.
Unaweza pia kuendelea kuzisoma taarifa zetu kupitia Chaneli yetu ya WhatsApp kwa kubofya hapa.
Tukutane tena kesho panapo majaaliwa .
Magari ya wagonjwa yamekuwa yakiwasili katika hospitali za Beirut yakiwa na watu 59 waliojeruhiwa katika shambulizi la leo.
Wizara ya afya ya Lebanon inasema wanane kati yao wako katika hali mbaya.
Jeshi la Israel limeanzisha uchunguzi baada ya maafisa wake kupigwa picha wakitupa miili ya Wapalestina watatu juu ya paa la nyumba wakati wa uvamizi katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu.
Picha za tukio hilo, zilizopigwa katika mji wa kaskazini wa Qabatiya, karibu na Jenin, zinaonekana kuonyesha tingat la jeshi la Israel likichukua na kutoa miili hiyo.
Picha hizo zimezua hasira kubwa. Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilisema Ijumaa kuwa ni "tukio kubwa" ambalo "haliendani" na maadili yake na kile kinachotarajiwa kutoka kwa vikosi vyake.
Maafisa wa eneo la Palestina wanasema kuwa takriban watu saba waliuawa na wanajeshi wa Israel huko Qabatiya siku ya Alhamisi.
Chini ya sheria za kimataifa, wanajeshi wana jukumu la kuhakikisha kuwa miili, ikiwa ni pamoja na ya wapiganaji wa adui, inahifadhiwa kwa heshima.
IDF ilisema ilifanya operesheni ya kukabiliana na ugaidi huko Qabatiya, ambapo wanamgambo wanne waliuawa katika "makabiliano ya risasi" na wengine watatu kuuawa baada ya shambulio la ndege isiyo na rubani dhdi ya gari.
Alhamisi asubuhi mwandishi wa habari mjini Qabatiya aliambia BBC kuwa wanajeshi wa Israel walikuwa wamezingira jengo moja mjini humo
Alieleza jinsi watu wanne waliokuwa ndani ya nyumba hiyo waliotorokea kwenye paa walivyopigwa risasi na mlenga shabaha.
Mapigano yaliendelea katika mji huo na yalipotulia, alisema aliona wanajeshi wa Israel wakipanda juu ya paa na kutupa miili hiyo chini ambapo ilipakiwa kwenye tingatinga.
Kamanda mkuu wa Hezbollah, Ibrahim Aqil, ameuawa katika shambulio la Israel kwenye vitongoji vya kusini mwa Beirut, kulingana na ripoti za Reuters na shirika la habari la AFP.
Aqil aliripotiwa kuuawa pamoja na wanachama wasomi wa Hezbollah wa kikundi cha Radwan walipokuwa wakifanya mkutano.
Lengo la shambulizi la Israel huko Beirut siku ya Ijumaa lilikuwa kamanda huyo wa operesheni za Hezbollah Ibrahim Aqil, kulingana na ripoti ya Redio ya Jeshi la Israel, ikinukuu chanzo cha usalama ambacho hakikutajwa jina, kulingana na Reuters.
Shirika la habari la AFP pia linanukuu chanzo kilicho karibu na Hezbollah kilichosema kuwa Aqil, ni mkuu wa pili wa kundi linaloungwa mkono na Iran.
Aqil ni nani?
Aqil, anayejulikana pia kama Tahsin, ni kiongozi mkuu katika kundi la Hezbollah.
Mnamo 1980, alikuwa mwanachama wa kikundi kilichopanga shambulio la Ubalozi wa MArekani huko Beirut na kambi ya wanamaji.
Mashambulizi hayo yaliua watu 63 na 307 mtawalia.
Mnamo mwaka wa 2019, Marekani ilimtaja Aqil kama gaidi na tovuti Wizara ya Sheria inasema anahudumu katika baraza kuu la kijeshi la Hezbollah - Baraza la Jihad.
Mwaka jana, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilisema itatoa zawadi ya $7m (£5.2m) kwa taarifa zitakazopelekea kutambuliwa, mahali, kukamatwa au kuhukumiwa kwa Aqil.
Soma zaidi:
Watu tisa wamethibitishwa kuuawa mjini Beirut kwa mujibu wa wizara ya afya ya Lebanon.
Taarifa zinasema watu 59 wamejeruhiwa katika shambulio la anga lililotekelezwa na Israel hapo awali, Wanane kati ya waliojeruhiwa wako katika hali mbaya.
Israel iliushambulia mji mkuu wa Lebanon kwa ndege mara ya mwisho mwezi Julai, katika shambulio lililomuua mkuu wa jeshi la Hezbollah Fuad Shukr.
Naibu mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas, Saleh al-Arouri, aliuawa katika shambulio la anga la Israel huko Beirut mwezi Januari.
Hii ni mara ya tatu kwa mji mkuu wa Lebanon kulengwa katika mashambulizi ya anga na Israel mwaka 2024.
Majeshi ya Israel yamewaua takriban Wapalestina 14 katika shambulio la hivi karibuni la anga na makombora katika maeneo ya kaskazini na kati, kulingana na matabibu.
Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa maafisa walisema makombora ya Israel yalishambulia kambi ya wakimbizi ya Nuseirat katikati mwa Gaza, na shambulio la anga likashambulia nyumba moja kaskazini mwa Gaza.
Wakazi pia waliiambia Reuters, kwamba vifaru vilisonga mbele zaidi kaskazini magharibi mwa Rafah - karibu na mpaka na Misri.
Jeshi la Israel limesema kuwa vikosi vinavyoendesha shughuli zao mjini Rafah katika wiki zilizopita viliwaua mamia ya wanamgambo wa Hamas, wakapata mahandaki na vilipuzi na kuharibu miundombinu ya kijeshi.
Wizara ya afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas imesema takriban Wapalestina 41,270 - ikiwa ni pamoja na watoto 11,355 - wameuawa huko tangu Oktoba 7, na wengine zaidi ya 95,000 kujeruhiwa.
Umoja wa Mataifa unasema Wapalestina 689, wameuawa katika Ukingo wa Magharibi tangu tarehe 7 Oktoba.
"Idadi kubwa ya vifo vya watoto imeweka kihistoria," makamu mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Mtoto aliwaambia waandishi wa habari, akiongeza kuwa "huu ni ukiukwaji mkubwa sana ambao ni nadra kushuhudiwa".
Nchini Israel, mamlaka zinasema takriban watu 1,200 waliuawa katika mashambulizi ya Hamas tarehe 7 Oktoba, huku watu 251 wakipelekwa Gaza kama mateka.
Idadi rasmi ya Israeli kwa wale walioshikiliwa huko Gaza sasa ni 101 - ikiwa ni pamoja na watu wanne waliochukuliwa mateka mwaka 2014 na 2015. Wawili kati ya watu hao wanaaminika kufariki dunia.
Jeshi la Ulinzi la Israel limethibitisha hivi punde kwamba takriban roketi 140 zimerushwa kaskazini mwa Israel kufikia sasa hivi.
Ulinzi wa anga ulinasa "baadhi" ya roketi 120, IDF inasema, ambazo zilirushwa katika maeneo ya Milima ya Golan, Safed na Upper Galilee.
Huduma za zimamoto na uokoaji zinazima moto huo uliosababishwa na roketi zilizoanguka, IDF inasema.
Takriban roketi 20 zaidi zilirushwa huko Meiron na Netua, inaongeza. "Nyingi zilianguka kwenye maeneo ya wazi" na hakuna majeraha yaliyoripotiwa kutokana na mashambulizi haya, inaongeza.
Polisi wa Israel wameripoti mtu mmoja alipata majeraha madogo upande wa kaskazini, lakini hawakueleza ni wapi hasa au kama alijeruhiwa na vifusi au moto.
Hezbollah inasema ilishambulia maeneo ya kaskazini mwa Israel
Wakati huohuo, Hezbollah imesema imeanzisha mashambulizi kadhaa kwenye maeneo ya jeshi kaskazini mwa Israel.
Hezbollah inasema ililenga makombora na mizinga ya Israel katika kambi ya Yoav na makao makuu ya ulinzi wa anga na makombora huko Kila.
Kambi ya makombora ya ulinzi huko Beria pia ililengwa, inasema.
Kundi hilo pia linasema lililenga maeneo mawili ya jeshi katika Milima ya Golan yanayokaliwa na Israel ikiwa ni pamoja na kambi ya Al-Ulaika, kaskazini mwa Katzrin na takriban kilomita 20 kutoka mpaka wa Lebanon na Palestina - na kambi ya Yarden.
Soma zaidi:
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris ameelezea nia yake ya kutumia bunduki yake iwapo mvamizi angeingia nyumbani kwake.
"Ikiwa mtu ataingia nyumbani kwangu, anapigwa risasi," alisema katika mazungumzo ya utani wakati wa hafla iliyotiririshwa moja kwa moja mjini Michigan na mwenyeji wake Oprah Winfrey siku ya Alhamisi.
Baada mgombea huyo wa urais wa chama cha Democratic aliendelea: "Pengine sikupaswa kusema hivyo, lakini whudumu wangu watalishughulikia hilo baadaye."
Harris, ambaye aliangazia wakati wa mjadala wa hivi majuzi wa rais kwamba alikuwa mmiliki wa bunduki, aliendelea kusisitiza kwamba aliunga mkono marufuku ya silaha zinazotumiwa vibaya.
Silaha ya aina hiyo "iliundwa kuwa chombo cha vita", alimwambia Winfrey.
"Haina nafasi katika makazi ya kiraia."
Alipoulizwa na Winfrey kuthibitisha kama alikuwa mmiliki wa bunduki kwa "muda" mwenyewe, Harris alikiri kuwa nayo.
Alisisitiza kuwa alikuwa mfuasi wa Marekebisho ya Pili ya Marekani, ambayo yanalinda haki ya umiliki wa bunduki.
Picha zilizochuliwa zaonyesha moshi ukifuka katika kijiji cha Kfar Kila, kusini mwa Lebanon - huku kukiwa na mashambulizi ya kuvuka mpaka kati ya Jeshi la Ulinzi la Israel na Hezbollah.
Polisi wa Israel waripoti majeruhi upande wa kaskazini baada ya shambulio la roketi
Mapema kidogo, mamlaka nchini Israel ziliripoti jeraha "dogo" baada ya roketi kurushwa katika eneo la kaskazini.
Katika ujumbe kwenye mtandao wa Telegram, Polisi wa Israel anaongeza kuwa maeneo kadhaa "yanawaka moto" na wazima moto wamefika eneo la tukio kukabiliana na hali hiyo.
Soma zaidi:
Hezbollah inasema kuwa imefanya mashambulizi kadhaa ya roketi kaskazini mwa Israel.
Kundi hilo linaloungwa mkono na Iran linasema kuwa linalenga maeneo ya kijeshi.
Haya yanajiri baada ya Israel kufanya mashambulizi makali ya anga usiku kucha kusini mwa Lebanon, huku jeshi likisema ndege zake za kivita zinalenga kuharibu mitambo ya kurusha makombora ya Hezbollah.
Soma zaidi:
Msururu wa maroketi yamerushwa kutoka Lebanon hadi kaskazini mwa Israel, jeshi la Israel linasema. Kengele zimewashwa kaskazini.
Wizara ya Afya ya Rwanda imetangaza kuwa imeanza kutoa chanjo dhidi ya ugonjwa wa homa ya Nyani (Mpox).
Kama ilivyotangazwa na afisa mkuu kutoka kituo cha Afrika cha kudhibiti magonjwa, Rwanda imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuanza kutoa chanjo hiyo mwezi wa saba mwaka huu.
Rwanda ilithibitisha wagonjwa wawili wa kwanza wa Mpox lakini hakuna aliyeripotiwa kufariki dunia hadi hivi sasa.
Kulingana na Daktari Nicaise Ndembi kutoka Kituo cha Afrika cha Kudhibiti Magonjwa, Rwanda imekuwa nchi ya kwanzakutoa chanjo dhidi ya homa ya nyani – ambapo kwa mjibu wa wizara ya afya ya Rwanda zoezi la kutoa chanjo hiyo ni kuanzia, "wafanyabiashara wa mipakani, wahudumu wa afya, wafanyakazi wa hoteli na wengine walioko katika hatari ya kuambukizwa kwa urahisi".
Chanjo ambayo Rwanda ilianza kutoa ni dozi 1,000 ilizopewa na Nigeria miongoni mwa dozi 10,000 ambazo Marekani ilitoa kwa Nigeria mwishoni mwa mwezi uliopita wa Agosti, kulingana na maafisa wa Kituo cha Afrika cha Kudhibiti Magonjwa.
Mmoja wa wafanyakazi wa Wizara ya Afya nchini Rwanda aliambia BBC kwamba chanjo hii inatolewa kwa njia ya "Mobile Clinics" (magari yanayotoa huduma ya matibabu na yenye mahitaji yote) na kwamba zoezi hilo linatarajiwa kukamilika leo.
Jean Kaseya, mkuu wa kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC), aliwaambia waandishi wa habari kwamba chanjo nchini Jamhuri ya demokrasi ya Kongo - ambayo inachukuliwa kuwa kitovu cha Mpox – itaanza kutolewa "wiki ya kwanza ya mwezi ujao".
Kituo hicho kinasema kuwa chanjo nchini Rwanda ilianza Jumanne ya wiki hii ikilenga maeneo yanayopakana na DR Congo.
Mwezi Julai Rwanda ilithibitisha wagonjwa wawili wa kwanza wa Mpox. Wizara ya afya ilitangaza kwamba waliougua wamepona na hakuna aliyeripotiwa kuuawa hadi sasa.
Tangu mapema mwaka huu, Afrika imeripoti kesi 29,152 za Mpox na vifo 738 katika nchi 15.
Soma zaidi:
"Niliona watu wasio na mikono wala macho," Sara Rammal, ambaye kwa sasa anaishi Beirut, ameiambia BBC.
Alilazimika kuondoka nyumbani kwake kusini mwa Lebanon muda mfupi baada ya Hamas kushambulia Israel tarehe 7 Oktoba na hana uhakika ni lini ataweza kurejea, huku Israel ikishambulia maeneo ya Hezbollah katika eneo hilo.
Rammal anaeleza zaidi kile alichoshuhudia huko Beirut: "Nilimwona baba akiwa amembeba mtoto wake wa miaka saba akivuja damu huku mkono wake ukiwa umekatwa. Alikuwa akimkimbiza hospitalini."
Anasema anawafahamu wahudumu wa afya ambao walifariki "kwa sababu vifaa vyao vya mawasiliano viliingiliwa na Israel".
Hadi kufikia sasa, Israel haijadai kuhusika na mashambulizi hayo.
Soma zaidi:
India imepuuzilia mbali ripoti ya habari inayodai kuwa serikali ilishindwa kuwazuia wanunuzi wa Ulaya kuhamisha makombora yaliyotengenezwa na India hadi Ukraine.
Katika taarifa iliyochapishwa Alhamisi, Reuters ilidai kwamba makombora yaliyouzwa na watengenezaji silaha wa India kwa wateja wake wa Ulaya yalielekezwa kwenda Ukraine.
Ripoti hiyo ilidai kuwa uhamishaji wa silaha umekuwa ukiendelea kwa zaidi ya mwaka mmoja, huku Delhi ikiwa haichukui hatua yoyote kukomesha hilo licha ya maandamano ya mara kwa mara kutoka Moscow.
Wizara ya mambo ya nje ya India imeita ripoti hiyo "uvumi" na ya "kupotosha".
Ripoti hiyo "inamaanisha ukiukaji wa India, ambapo hakuna kitu kama hicho kilichotekelezwa, na kwa hivyo, sio sahihi na ni yenye nia mbaya," Randhir Jaiswal, msemaji wa wizara hiyo aliandika kwenye mtandao wa X (zamani ulijulikana kama Twitter).
Bw Jaiswal aliongeza kuwa India ina "rekodi inayoweza kufuatiliwa kikamilifu na majukumu yake kimataifa" juu ya kutoeneza silaha na ina sheria zake dhabiti za usafirishaji.
Moscow bado haijajibu ripoti hiyo au taarifa ya Delhi.
Ukraine, ambayo inapambana na mashambulizi mapya kutoka kwa Urusi, inaripotiwa kukabiliwa na uhaba wa risasi na silaha zingine.
Soma zaidi:
"Adui alivuka sheria zote. Hakujali chochote hata kidogo, si kwa maadili, si kibinadamu, si kisheria."
Hivyo ndivyo kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah alivyoelezea mashambulizi ya hivi karibuni kote Lebanon katika hotuba yake ya televisheni hapo jana.
Alisema mashambulizi ya mabomu kwa kutumia vifaa vya mawasiliano na simu za upepo ni "pigo lisilokuwa na kifani", lakini aliapa kwamba Hezbollah itaendelea kupigana na kutoa "adhabu ya haki".
Nasrallah aliongeza kuwa ulikuwa "uchokozi mkubwa dhidi ya Lebanon" ambao unaweza kuitwa "uhalifu wa kivita au tangazo la vita".
Wakati wa hotuba yake siku ya Alhamisi, ndege za kivita za Israel ziliruka chini juu ya Beirut na kusababisha kelele katika mji mkuu.
Saa kadhaa baadaye, Israel inasema ilianzisha mashambulizi ya anga nchini Lebanon yakilenga maeneo ya Hezbollah.
Kwa muktadha: Hezbollah imemlaumu adui yake, Israel kwa milipuko ya vifaa. Maafisa wa Israel hadi sasa wamekataa kutoa maoni.
Unaweza kusoma;
Kama ambavyo tumekuwa tukiripoti, Vikosi vya Ulinzi vya Israel vinasema viligonga shabaha za Hezbollah nchini Lebanon mara moja ili "kudhoofisha" "uwezo na miundombinu" ya kikundi.
"Kwa miongo kadhaa, Hezbollah imekuwa na silaha kwenye nyumba za raia, kuchimba vichuguu chini yake na kutumia raia kama ngao za binadamu," IDF ilisema kwenye chapisho la X.
"IDF inafanya kazi kuleta usalama kaskazini mwa Israeli ili kuwezesha kurejea kwa wakazi makwao na kufikia malengo ya vita," iliongeza.
Baadaye, jeshi lilisema, jeshi la anga lilipiga mitambo takribani 30 ya kurusha makombora maeneo ya miundombinu ya Hezbollah na yenye takribani mitutu 150 ya kurushia makombora, pamoja na "miundombinu na kituo cha kuhifadhi silaha katika maeneo mengi kusini mwa Lebanon".
Unaweza kusoma;
Mwanaharakati Bob Micheni Njagi na ndugu Jamil na Aslam Longton, ambao walikuwa wamebatizwa jina la Kitengela Watatu baada ya kutekwa nyara mwezi mmoja uliopita katika mji wa Kaunti ya Kajiado, wako hai.
Watatu hao walisema waliachiliwa alfajiri ya Ijumaa, Septemba 20, saa chache baada ya Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja kuapishwa.
Ndugu hao wa Longton walisema waliachiliwa na waliowateka na kuahidi kutoa taarifa zaidi kupitia kwa rais wa Chama cha Wanasheria nchini (LSK) Faith Odhiambo.
Video iliyotumwa kwenye ukurasa wa X na Bi Odhiambo ilionesha kuwa ndugu hao wa Langton waliachiliwa mahali fulani huko Gachie na wakatembea hadi kwenye nyumba ambapo walidaiwa kuchaji simu zao za mkononi kabla ya kumpigia simu rais wa LSK.
"Mnamo saa moja asubuhi Bob Njagi alifanikiwa kutafuta njia hadi kituo cha polisi cha Tigoni na kupata usaidizi. Yuko hai," Bi Odhiambo alisema.
"Kwa familia, marafiki na kila Mkenya ambaye ameendelea kuniombea, napenda kuthibitisha kuwa mimi ni mzima na pamoja na familia yangu. Sasa ni wakati wa kunyamazisha kelele, kushukuru kwa maisha na kila mtu atafakari kwa nini Kenya.
Watatu hao waliotekwa nyara mnamo Agosti 19 huko Kitengela, waliachiliwa muda mfupi kabla ya Naibu Inspekta Jenerali Gilbert Masengeli kuashiria kwamba angefika kortini kuomba msamaha mahakamani na kueleza waliko.
Bw.Masengeli alipatikana na hatia ya kudharau mahakama na Jaji Lawrence Mugambi na kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela.
Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg, katika hotuba yake ya kuaga kabla ya kuondoka katika wadhifa wake, alisema kuwa kupatikana kwa amani nchini Ukraine kimsingi kunategemea kiasi cha silaha zinazotolewa kwa Kiev.
Stoltenberg pia alibainisha kuwa mazungumzo ya amani yatalazimika kufanywa kwa ushiriki wa Urusi, na alionesha imani kuwa Ukraine itakuwa mwanachama wa muungano huo.
"Nguvu za kijeshi ni sharti la mazungumzo," Stoltenberg alisema. "Lazima tuzungumze na majirani zetu, bila kujali hilo linaweza kuwa gumu kiasi gani. Lakini mazungumzo yanafanya kazi pale tu yanapoungwa mkono na ulinzi mkali. Hilo linaonekana wazi katika kesi ya Ukraine."
Wakati huohuo, nguvu za kijeshi zina mapungufu yake, ambayo inaonekana wazi katika mfano wa Afghanistan, aliongeza. "Kwa kuipa Ukraine silaha zaidi, tunaweza kumfanya Putin atambue kwamba hawezi kupata anachotaka kwa nguvu, na kuifanya iwe ya gharama kubwa sana kiasi kwamba atalazimika kukiri kwamba Ukraine ina haki ya kidemokrasia ya kubaki kuwa nchi huru ya kidemokrasia," aliendelea.
"Kitendawili ni kwamba kadiri tunavyoweza kusambaza silaha kwa Ukraine, ndivyo kuna uwezekano mkubwa kwamba tutaweza kufikia amani na kumaliza vita.
Na jinsi msaada wetu wa kijeshi wa muda mrefu unavyotegemewa, ndivyo vita vitaisha haraka. " Kwa mujibu wa Katibu Mkuu anayemaliza muda wake wa muungano huo, makubaliano yoyote ya baadaye lazima yaungwe mkono na uungaji mkono mkubwa wa kijeshi kwa Ukraine na dhamana ya usalama inayotegemewa ili kuhakikisha amani ya kudumu.
Stoltenberg pia alibainisha kuwa hakuwezi kuwa na usalama endelevu katika Ulaya bila Ukraine imara, na hakuwezi kuwa na usalama wa kudumu kwa Ukraine bila uanachama wake katika NATO. "Mlango wa NATO uko wazi," alisema. "Na Ukraine itajiunga."
Unaweza kusoma;
Israel inasema ndege zake za kivita zimeshambulia zaidi ya mitambo 100 ya kurushia roketi za Hezbollah na "maeneo mengine ya kigaidi" ikiwa ni pamoja na kituo cha kuhifadhi silaha kusini mwa Lebanon.
Vikosi vya Ulinzi vya Israel (IDF) vilisema virusha risasi viko tayari kurushwa dhidi ya Israel.
Haikuweza kufahamika mara moja iwapo kulikuwa na majeruhi.
Shirika la Habari la Taifa la Lebanon limesema kuwa Israel ilifanya mashambulizi 52 kusini mwa nchi hiyo siku ya Alhamisi jioni, na kwamba Lebanon pia ilianzisha mashambulizi katika maeneo ya kijeshi kaskazini mwa Israel.
Hapo awali, kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah alisema milipuko mibaya mapema wiki "ilivuka mistari yote ", akiishutumu Israel kwa kile alichosema kuwa kiliwakilisha tangazo la vita.
Israel haijasema kama ilihusika na mashambulizi hayo, ambayo yalishuhudia vifaa vya mawasiliano kulipuka kwa wakati mmoja nchini kote siku ya Jumanne na Jumatano, na ambayo mamlaka ya Lebanon ilisema iliua watu 37 na kujeruhi 3,000.
Lakini Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant amesema Israel inaanzisha "awamu mpya ya vita", ikizingatia zaidi juhudi zake kaskazini.
Unaweza kusoma;
Zaidi ya watu 70,000 wanaopigana katika jeshi la Urusi sasa wamefariki nchini Ukraine, kulingana na data iliyochambuliwa na BBC.
Na kwa mara ya kwanza, watu wa kujitolea raia ambao walijiunga na vikosi vya jeshi baada ya kuanza kwa vita, sasa wanaunda idadi kubwa zaidi ya watu waliouawa kwenye uwanja wa vita tangu uvamizi kamili wa Urusi uanze mnamo 2022.
Kila siku, majina ya waliouawa nchini Ukraine, kumbukumbu zao na picha kutoka kwa mazishi yao huchapishwa kote Urusi kwenye vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii.
BBC Kirusi na tovuti huru ya Mediazona wamekusanya majina haya, pamoja na majina kutoka vyanzo vingine vya wazi, ikiwa ni pamoja na ripoti rasmi.
Tulikagua kufahamu taarifa hiyo ilikuwa imetolewa na mamlaka au jamaa za marehemu na kwamba walikuwa wametambuliwa kuwa walikufa katika vita.
Makaburi mapya pia yamesaidia kutoa majina ya wanajeshi waliouawa nchini Ukraine, haya huwa yana alama za bendera na shada za maua zinazotumwa na wizara ya ulinzi.
Tumetambua majina ya wanajeshi 70,112 wa Urusi waliouawa nchini Ukraine, lakini idadi halisi inaaminika kuwa kubwa zaidi.
Baadhi ya familia hazitoi hadharani maelezo ya vifo vya jamaa zao na uchanganuzi wetu haujumuishi majina ambayo hatukuweza kukagua, au vifo vya wanamgambo katika Donetsk inayokaliwa na Urusi na Luhansk mashariki mwa Ukraine.
Unaweza kusoma;