Israel yaendelea kuishambulia Beirut, wakazi wa kusini mwa Lebanon watakiwa kuhama
Israel inaonekana iko tayari kuanzisha operesheni mpya kusini mwa Lebanon baada ya Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) kwa lugha ya Kiarabu kutoa arifa mpya za kuhama.
Muhtasari
Mwanamke mmoja auawa, watu wengine wajeruhiwa katika shambulio Israel
Israel yaendelea kushambulia, wakazi wa kusini mwa Lebanon watakiwa kuhama
Jeshi la Israeli latangaza kumuua kamanda mwingine wa Hezbollah
“Ndugu yangu, tafadhali nisamehe,” Gachagua ‘amuangukia’ Rais Ruto
Watu 23 wauawa katika mashambulizi ya Israel- Maafisa wa Lebanon
Israel yafanya mashambulizi Beirut, Hezbollah yarusha makombora kuvuka mpaka
Netanyahu asema wito wa Macron wa kuwekewa vikwazo vya silaha ni 'fedheha'
Moja kwa moja
Lizzy Masinga
Mwanamke mmoja auawa, watu wengine wajeruhiwa katika shambulio Israel
Chanzo cha picha, Reuters
Mwanamke mmoja mwenye miaka 25 ameuawa, huku watu wengine kadhaa wamejeruhiwa katika shambulio la risasi katika kituo kimoja cha basi nchini Israel.
Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi "shambulio linaloshukiwa kuwa la kigaidi" limetekelezwa katika mji wa Beersheba, kusini mwa Israel muda mchacHe uliopita.
Shirika la magari ya wagonjwa la Israeli limesema kuwa madaktari wake wanawatibu watu 10, baadhi wakiwa na majeraha ya risasi.
Polisi wameeleza kuwa mshukiwa aliyetekeleza shambulio hilo ameuawa.
Israel yaendelea kushambulia, wakazi wa kusini mwa Lebanon watakiwa kuhama
Chanzo cha picha, Reuters
Israel inaonekana iko tayari kuanzisha operesheni mpya kusini mwa Lebanon baada ya Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) kwa lugha ya Kiarabu kutoa arifa mpya za kuhama.
Avichay Adraee ametoa wito kwa wakazi wa karibu vijiji 25 kusini mwa Lebanon kuondoka.
"Mtu yeyote ambaye yuko karibu na wanachama wa Hezbollah, mitambo au silaha anaweka maisha yake hatarini," anasema.
"Wakazi wa kijiji, lazima mhame nyumba zenu," anaongeza, huku akisema wanapaswa "kuhamia mara moja kaskazini mwa Mto Awali" ulioko kaskazini mwa mji wa kusini mwa Lebanon wa Sidon.
"Tutawajulisha wakati muafaka na salama wa kurejea majumbani mwenu," Adraee anaongeza.
Jeshi la Israeli latangaza kumuua kamanda mwingine wa Hezbollah
Chanzo cha picha, HUGO BACHEGA/BBC
Jeshi la Israel, IDF, kimetangaza kuwa limemuua kamanda mwingine wa ngazi za juu wa kundi la wanamgambo wa Hezbollah - Khader Ali Tawil.
Taarifa ya jeshi la Israel imesema kuwa Tawil ameuawa katika shambulio la anagani lililotekelezwa na ndege vita.
Kwa mujibu wa Israel kamanda huyo alikuwa akifanya kazi kwa ukaribu na makamanda wengine wawili wa Hezbollah, Muhammad Haidar na Hassan Nathir al-Ra'ini, amabao waliuawa mwanzoni mwa wiki.
Hezbollah hata hivyo haijatoa kauli yoyote kuhusu taarifa hiyo ya Israeli toka ilipochapishwa asubuhi ya leo.
Jeshi la Israel linawatuhumu makamanda hao watatu wa Hezbollah kwa kutekeleza shambulio la kombora amabalo liliupiga mji wa Kfar Yuval uliopo kaskazini mwa Israel karibu na mpaka wa Lebanon.
Shambulio hilo lilisababisha kifo cha watu wawili nchini Israel.
“Ndugu yangu, tafadhali nisamehe,” Gachagua ‘amuangukia’ Rais Ruto
Chanzo cha picha, X/Rigathi Gachagua
Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, ambaye anakabiliwa na hatari kuondolewa madarakani, amemuomba msamaha mkuu wake, Rais William Ruto.
Bw Gachagua ametoa ombi hilo kwa Ruto mapema leo Jumapili, Oktoba 6, akisema kwamba ingawa hajui kosa lolote, anataka apewe nafasi nyingine ya kuwahudumia Wakenya.
“Nataka kumuomba ndugu yangu, Rais William Ruto: ikiwa nimekukosea kwa namna yoyote katika jitihada zetu za kufanya kazi, tafadhali fungua moyo wako na unisamehe,” Bw Gachagua ameyasema hayo akiwa kanisani huko Karen, jijini Nairobi.
Maombi ya Righathi kwa Rais Ruto hayakuishia kwake tu, "Ikiwa mke wangu (Dorcas Rigathi) amekukosea kwa njia yoyote tafadhali fungua moyo wako kumsamehe."
Naibu Rais huyo liyekalia kuti kavu amewaomba msamaha wabunge, na pia rai awa kawaida wa msamaha pia kama huo kwa Wakenya waliotaka aondolewe madarakani wakati wa ushiriki wa umma katika kutoa maoni.
"Kwa watu wa Kenya, katika utumishi wetu kote nchini, tunapokuhudumia, ikiwa kuna jambo lolote ambalo tumefanya au kusema ambalo unaona halifai, ambalo unaona halikubaliki, tafadhali unisamehe."
Hali ya kisisasa imepamba moto nchini Kenya toka mwanzoni mwa juma lililopita baada ya hoja ya kutaka kumuondosha madarakani Bw Gachagua ilipowasilishwa rasmi bungeni na kupokelewa.
Hivi sasa michakato ya kikatiba inaendelea katika kufanikisha ama kuiangusha hoja hiyo.
Wandani wa Rais wa Kenya William Ruto waliwasilisha hoja bungeni siku ya Jumanne ya kumshtaki Naibu Rais Rigathi Gachagua wakimtuhumu kwa kuchochea chuki za kikabila na kuidhoofisha serikali.
Pia wanadai kwamba Gachagua amejihusisha na masuala ya ufisadi , kuihujumu serikali na kukuza siasa za kikabila. Tofauti kati ya rais Ruto na Gachagua zimeongezeka katika siku za hivi karibuni.
Gachagua anasema ametengwa na amekanusha shutuma za washirika wa Ruto kwamba alihusika na maandamano ya kupinga serikali mapema mwaka huu.
Watu 23 wauawa katika mashambulizi ya Israel- Maafisa wa Lebanon
Chanzo cha picha, JOEL GUNTER/BBC
Katika dakika chache zilizopita, wizara ya afya ya Lebanon imetoa taarifa kadhaa kuhusu waliouawa na kujeruhiwa kutokana na mashambulizi ya anga ya Israel yaliyotokea kote nchini hapo jana.
Kwa jumla, watu 23 walikufa na wengine 93 walijeruhiwa baada ya uvamizi katika maeneo kadhaa, ikiwa ni pamoja na kusini mwa Lebanon, na katika eneo la mashariki la Bekaa na Baalbek-Hermel.
Israel yafanya mashambulizi Beirut, Hezbollah yarusha makombora kuvuka mpaka
Chanzo cha picha, Reuters
Milipuko mikubwa imetikisa tena viunga vya kusini mwa Beirut ikiwa siku nyingine ya mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon.
Vyombo vya habari vya Lebanon vilielezea milipuko hiyo kuwa " mibaya sana", vikisema magari ya wagonjwa yalikimbilia kwenye maeneo yaliyoathiriwa.
Mpaka kati ya Israel na Lebanon bado kuna mvutano, huku jeshi la Israel likiripoti kuwa roketi 30 zilirushwa kaskazini mwa nchi na Hezbollah.
Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) lilisema kuwa roketi hizo zimerushwa katika maeneo ambayo wakazi wamehamishwa.
Kwingineko katika eneo la Mashariki ya Kati, ndege za kivita za Israel zimeshambulia msikiti mmoja huko Deir al-Balah katikati mwa Gaza na kuua takribani watu 21, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Palestina.
Jeshi la Israel lilisema Hamas ilikuwa ikitumia boma hilo, karibu na hospitali ya al-Aqsa, kama kituo cha amri na udhibiti, lakini walioshuhudia walisema ni makazi ya watu waliokimbia makazi yao.
Netanyahu asema wito wa Macron wa kuwekewa vikwazo vya silaha ni 'fedheha'
Chanzo cha picha, Reuters
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amemkosoa Rais wa
Ufaransa Emmanuel Macron kuhusu wito wake wa kusitisha uwasilishaji wa silaha
kwa Israel ili zitumike Gaza.
Macron aliambia redio ya Ufaransa kwamba "kipaumbele ni kwamba turudi
kwenye suluhisho la kisiasa, kwamba tuache kuwasilisha silaha kupigana huko
Gaza".
Katika mkutano wa kilele mjini Paris siku ya Jumamosi, rais
wa Ufaransa alionesha wasiwasi wake kuhusu mzozo wa Gaza kuendelea licha ya
wito wa kusitisha mapigano, na pia alikosoa uamuzi wa Israel kutuma wanajeshi
wa ardhini nchini Lebanon.
Netanyahu alijibu: "Aibu kwao," akimaanisha Macron
na viongozi wengine wa Magharibi ambao wametoa wito wa kile alichokitaja kuwa
vikwazo vya silaha kwa Israel.