Tuzo za Oscars 2022: Will Smith apigwa marufuku kushiriki Oscars kwa miaka 10 kwasababu ya kofi

Will Smith (R) hits Chris Rock as Rock spoke on stage during the 94th Academy Awards in Hollywood, Los Angeles, California

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Will Smith (Kulia) alimzaba Chris Rock kwenye jukwaa wakati wa sherehe za Tuzo za Oscars ceremony, baada ya Rock kutoa mzaha juu ya mke Smith

Will Smith amepigwa marufuku kushiriki katika sherehe za kutoa tuzo za Oscars gala na matukio mengine ya taasisi ya Chuo cha Mafunzo ya Sanaa na Sayansi kwa miaka 10 baada ya mwigizaji huyo wa Marekani kumzaba kofi mchekeshaji Chris Rock katika sherehe ya kutoa tuzo za Oscars.

Taarifa yake taasisi inayotoa tuzo za Oscars ilisema kuwa hafla ya 94 ya Oscars "iligubikwa na tabia ilisiyokubalika na ya madhara tuliyoona Bw Smith akionyesha kwenye jukwaa".

Smith alikuwa ameomba msamaha kwa matendo yake na kujiuzulu katika taasisi ya Chuo cha Mafunzo ya Sanaa na Sayansi.

Mwigizaji huyo alimzaba kofi Rock kwa kufanya mzaha kuhusu kichwa cha mkewe kilichonyolewa upara, ambayo ni matokeo ya hali ya kiafya inayosababisha mtu kupoteza nywele inayofahamika kama alopecia.

Chini ya saa moja baadaye, Bw smith alituzwa tuzo ya mwigizaji bora kwa nafasi yake katika "King Richard", ambapo alicheza kama baba yake wachezaji nyota wa tenisi Venus na Serena Williams.

Will Smith and Jada Pinkett Smith

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wenzi hao walikuwa wakitabasamu mapema jioni kwenye zulia jekundu

Taasisi ya Mafunzo ya Sanaa na Sayansi, ambayo iliandaa sherehe za tuzo, ilikutana siku ya Ijumaa kwa njia ya video kujadili hatua ya kinidhamu dhidi ya Bw Smith.

Katika taarifa yake, ilisema kuwa kumpiga marufuku Smith kunalenga kuwalinda waigizaji na wageni na "kurejesha imani katika taasisi ".

Taasisi hiyo ilisema kuwa wakati wa kofi haikuweza "kushugulikia ipasavyo hali katika ukumbi " na "haikuwa imejiandaa kwa tukio ambalo halikutarajiwa". Iliomba msamaha kwa hili.

Pia ilimshukuru Rock kwa "kuendelea kuwa mtulivu katika hali zisizo za kawaida ".

Katika taarifa ya kujiuzulu, Smith alisema alikuwa "amesaliti imani ya taasisi " na alikuwa "amevunjika moyo" kutokana na matendo yake.

Aliongeza kuwa ata "kubali kikamilifu matokeo yoyote ya mwenendo wangu".

Kujiuzulu kwake kunamaanisha kuwa hataweza kupiga kura katika kura zijazo za wapiga kura wa Oscars.

Will Smith hitting Chris Rock at the Oscars

Chanzo cha picha, Reuters

Tathmini ya Academy Of Motion Picture Arts and Science juu ya tukio hilo, awali ilikuwa imepangwa kufanyika tarehe 18 Aprili, lakini iliharakishwa baada ya Smith kujiuzulu.

Ni waigizaji wachache ambao wamewahi kujiuzulu katika academy. Wajumbe wanne - mwandaaji wa filamu Harvey Weinstein, mwigizaji Bill Cosby, mkurugenzi Roman Polanski na mwandaaji wa sinema Adam Kimmel - ambao walishutumiwa kwa madai ya tabia mbaya za kingono , huku mwigizaji Carmine Caridi akifutwa mwaka 2004 kwa kuigiza video za skrini alizopewa.

Lakini viwango vya maadili vinavyoonyeshwa na taasisi hiyo ya mafunzo ya filamu- vinatoa fursa yah atua mabali mbali za kinidhamu dhidi ya Smith, kama vile kumuondoa katika sherehe zijazo za tuzo za Oscars , kumnyang'anya uwezo wake wa kupata tuzo au kumpokonya tuzo yake mpya aliyoipata ya Oscar.

Ni tuzo moja pekee ya Oscar ambayo iliwahi kuchukuliwa na taasisi kutoka kwa mshindi ambayo ilikuwa ni Makala inayoitwa "Young Americans" aliyoshinda tuzo ya Makala bora zaidi katika mwaka 1969 lakini ilibainika kuwa haikuwa haikustahili kupata tuzo mwaka ule.

Unaweza pia kusoma:

Mwezi uliopita, mwigizaji Whoopi Goldberg - mjumbe wa bodi ya utawala ya Academy Of Motion Picture Arts and Science -alibashiri kuwa Smith atakabiliwa na "madhara makubwa" lakini akasema "hatutachukua tuzo ile kutoka kwake ."

Mbali na hatua hizo za taasisi ya masuala ya filamu , walau studio mbili- Sony na Netflix - zinajiandaa kufanya miradi yake na Smith.

Rock, ambaye alianza safari yake ya hivi karibuni ya uchekeshaji baada ya kutangaza kwenye hafla ya Oscars ,hajaongea hadharani kuhusu kofi alilozabwa na Smith.

Aliwaambia mashabiki kwenye onyesho kwamba "bado anajaribu kufikiria ni nini kilichotokea'' na ataongea kuhusu tukio "katika wakati fulani".