Virusi vya corona: Je mpango wa chanjo wa Covax ni nini na utafanya kazi vipi?
Chanjo ni mojawapo ya suluhu ya kukabiliana na janga la Covid-19, wanasema wataalamu wa afya. Lakini kuna hofu kuwa nchi tajiri zaidi duniani zinaweza kujilimbikizia dozi za chanjo na kuzifanya nchi masikini zaidi kukosa chanjo kwa ajili ya watu wake. Mpango wa dunia unaoitwa Covax unajaribu kugawa chanjo kwa usawa miongoni mwa mataifa yote. Lakini je unaweza kufanikiwa kufikia hilo.

