Je Rais Felix Tshisekedi amezitatua changamoto 6 muhimu zinazoikabili DRC?

Democratic Republic of the Congo's newly inaugurated President Felix Tshisekedi raises an official copy of the nation's constitution on January 24, 2019

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati Felix Tshisekedi alipoapishwa kuwa rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo mwaka mmoja kamili uliopita, wakati huo kuingia kwake madarakani kulionekana kama hatua muhimu- ya kwanza ya makabidhiano ya madaraka kwa amani katika nchi hiyo ambayo ilikuwa ni mara ya kwanza katika historia ya miongo sita ya taifa hilo.

Kwa miaka mingi, nchi hiyo, yenye hifadhi nyingi za madini mbalimbali, ikiwa ni pamoja na madini yanayotumiwa katika kutengeneza betri za magari, imekuwa ikigubikwa na mizozo na ufisadi.

Kama mpeperusha bendera ya chama cha upinzani cha UDPS, Bw Tshisekedi alimshinda mgombea aliyekuwa akipendelewa na mtangulizi wake Joseph Kabila katika uchaguzi wa Disemba 2018 .

Lakini matokeo hayo yalipingwa na mgombea mwingine wa upinzani , Martin Fayulu, ambaye alisema alikuwa ndiye mshindi sahihi.

Huu haukua mwanzo mzuri kwa rais ambaye alitumaini kuliunganisha taifa linalokabiliwa na changomoto ikiwa ni pamoja na mlipuko wa Ebola, miaka mitano ya mapigano mashariki , miundo mbinu mibovu na uchumi unaoyumba.

Je amefanya nini kushugulikia masuala sita muhimu zaidi ?

1: Mzozo katika mashariki

Wakati alipoapishwa, rais Tschisekedi aliahidi "kujenga Congo imara, na kuifanya kuwa ya maendeleo , amani na usalama ".

Bw Tshisekedi ,alijaribu kuinua kiwango cha usalama , lakini wananchi wa kawaida hawahisi kuwa salama zaidi ya miezi 12 iliyopita.

Soldiers of the Armed Forces of the Democratic Republic of the Congo (FARDC) sit in a truck bed in a base on July 3, 2019

Chanzo cha picha, Getty Images

Mojawapo ya changamoto za hali ya juu ilikuwa ni kuendelea kwa ghasia mashariki mwa nchi, ambako makumi ya makundi yenye silaha yanasababisha maafa.

Jeshi limeyarejesha maeneo katika mapambano dhidi ya wanamgambo waasi wa Allied Democratic Forces (ADF), kikundi ambacho asilia yake ni Uganda lakini kwa sasa kina ngome yake katika jimbo la Beni DRC.

Lakini mwaka 2019, kikundi hiki cha waasi kiliimarisha mashambulio ya ulipizaji kisasi dhidi ya raia, na kuwauwa raia 200 ndani ya kipindi cha miezi mitatu.

"Wakati wa kampeni za uchaguzi , nilipata fursa ya kutembelea majimbo haya na kushangazwa na hali hii iliyomsikitisha ," Bw Tshisekedi aliiambia BBC.

" Nilichukua uamuzi wakati ule wa kujitolea kufanya kila liwezekanalo kuleta amani ."

Rais aliagiza jeshi kuhamishia ngome katika mji wa Beni, ambao umekuwa kitovu cha mashambulizi ya waasi wa ADF. Baadhi yawanajeshi walibadilishwa , na hivyo kuleta nguvu mpya katika mapambano dhidi ya wanamgambo.

Map
Presentational white space

Katika makabiliano dhidi ya kundi lingine, takribani viongozi wawili wa kikundi cha kihutu cha Rwanda cha FDLR waliuawa.

Lakini makundi mengine madogo bado yanahusika katika ghasia katika kanda hiyo, huku baadhi wakihusika katika katika biashara haramu ya madini.

Mashambulio dhidi ya raia yanaendelea, huku waasi , wakijihami kwa mapanga wakiwa na uwezo wa kufanya mashambulizi wakati wowote.

Wakati huo huo jeshi, limekuwa likikosolewa kwa kujaribu kupigana vita vya kawaida dhidi yao.

2: Mlipuko wa Ebola

Wakati alipoingia madarakani, Rais Tshisekedi, alikabiliwa na kusambaa kwa virusi vya corona, pia katika eneo la mashariki mwa nchi kumekuwa ni mlipuko mbaya zaidi wa pili Ebola wa dunia, ambapo Shirika la Afya Duniani liliutangaza kama dharura ya afya ya kimataifa.

Kutoamianiana baina ya wakazi na wahudumu wa afya, kulichochea habari za uongo na upotoshaji, kuongezeka kwa mashambulio ya maafisa wa kukabiliana na Ebola na hivyo kuendelea kudumaza mapambano dhidi ya virusi hatari vya Ebola.

Chanjo mbili kwa sasa zinazotumiwa katika eneo lililoathiriwa kuzuia kusambaa kwa virusi.

Serikali ya Tshisekedi ilipata usaidizi mwingi kutoka kwa mashirika ya nje na inaonekana kwamba kiwango cha maambukizi mapya kinashuka, lakini WHO inasema n vigumu kuthibitisha hili kwani kuna maeneo kadhaa ambayo ni vigumu kufikiwa kwasababu sio salama.

Lakini kujiuzulu kwa Waziri wa afya Oly Ilunga mwaka jana kutokana na kutokubaliana na jinsi maafisa husika walivyoshughulikia mlipuko kulimfanya kila mmoja miongoni mwa maafisa hao kuwa na mtizamo sawa wa jinsi ya kupambana na virusi.

3: Mlipuko wa surua

Bw Tshisekedi pia alilazimika kukabiliana na kusambaa wa ugonjwa surua.

Virusi hivyo vinavyoambukizwa sana kutoka kwa mtu mmoja kuelekea mwingine vimewaathiri zaidi ya watu 300,000 tangu mwanzoni mwa mwaka 2019, huku maambukizi yakiripotiwa katika kila majimbo 26 nchini humo.

Takriban watu 6,000 wamekufa - zaidi ya wale waliokufa kutokana na Ebola - kutokana na janga, ambalo WHO inasema ni mlipuko mbaya zaidi wa surua kuwahi kushuhudiwa duniani

A handout photo made available by the World Health Organization (WHO) shows a child receiving a vaccination for measles at a health center in Goma

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Serikali, ikisaidiwa na mashirika ya kimataifa, imeanza mpango mpango mkubwa wa kutoa chanjo
Presentational white space

Serikali ya Bw Tshisekedi, ikisaidiwa na WHO na mashirika mengine ya kimataifa, imewachanja zaidi ya watoto milioni 18 walio chini ya umri wa miaka mitano kote nchini.

Lakini ukosefu wa fidha za kutosha za kununua chanjo na barabara mbovu vimekwamisha uwezo wa maafisa wa afya kumfikia kila mtoto.

Hali mbaya ya milipuko wa Ebola na surua ni ushahidi wa kimsingi wa tatizo la mifumo ambayo ina mizizi yake ya muda mre ya usimamizi mbaya wa nchi, kuliko muda aliohudumu Bw Tschiseketi mamlakani.

Serikali yake imeweza kuunganisha usaidizi wa mashirika ya kimataifa ya misaada lakini ataendelea kukabiliwa na changamoto nyingi katika muda uliosalia wa muhula wake wa miaka mitano.

4: Kuijenga nchi

Mara alipoingia madarakani , rais alianza kile alichokiita "mpango wa siku 100 za kwanza za dharura".

"Kwa uwezo mdogo sana [tulianza] kujenga shule, kukarabati hospitali, barabara, na kutengeneza vivuko ili kusaidia safari za maeneo ya mito ," aliiambia BBC.

Presentational grey line

Shirika lisilo la kiserikali linalofuatilia matumizi nchini Congo lilikosoa jinsi mchakato wa utoaji wa mikataba ulivyofanyika.

Zaidi ya hayo, si miradi mingi ambayo ilikamilika na pia miradi hiyo ni sehemu ndogo sana ya miundo mbinu inayohitajika nchini.

Na kuna hofu kuwa matumizi ya ziada huenda yasitumiwe kulipia gharama za kuboresha huduma kama serikali inavyosema.

5: Kuepuka umasikini

Kwa kuzingatia wastani wa pato la mwananchi mmoja , DRC inahesabiwa miongoni mwa nchi tano masikini zaidi, licha ya utajiri mkubwa wa madini iliyonao.

Wakongo wengi huishi kwa kutumia chini ya dola 2 kwa siku, kwa mujibu wa Benki ya dunia.

Kiwango hiki kimedumu tangu mwanzoni mwa karne hii, lakini nchi bado ina safari ndefu.

Rais Tschisekedi amesema kuwa anataka kuushugulikia umasikini na kama sehemu ya juhudi hizo ameongeza matumizi ya serikali.

Katika kipindi cha miezi 12, iliyopita bajeti ya serikali imepanda kwa karibu dola bilioni 6.

Supporters of Felix Tshisekedi, who was named provisional winner of Democratic Republic of Congo"s presidential election, celebrate outside the Union for Democracy and Social Progress (UDPS) headquarters in Kinshasa on January 10, 2019

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wafuasi wa Bw Tshisekedi walitumaini kuwa ataboresha hali zao

Hili bila shaka limeibua swali juu ya jinsi ya kuchangisha fedha.

Maafisa wa karibu na rais wanaamini kuwa pesa zinaweza kupatikana kwa kuzuia ufisadi serikalini.

Lakini hadi sasa, hakuna kiasi kikubwa cha fedha ambacho kimefichuliwa na hakuna afisa wa ngazi ya juu ambaye amehukumiwa kwa kosa la ufisadi.

Msemaji wa serikali amesema kuwa mfumo wa mahakama bado unafanya uchunguzi.

Ushuru katika baadhi ya maeneo , ikiwa ni pamoja na mali, imepanda ili kusaidia kulipia matumizi.

Lakini watu wengi wa kawaida wamechoka kusubiri kuona hali zao za kijamii na kiuchumi zinakuwa bora.

6: Wasiwasi wa kisiasa

Licha ya kushinda urais, Bw Tshisekedi alilazimika kuunda serikali ya muungano na mtangulizi wake Joseph Kabila, ambao unadhibiti viti vingi katika bunge.

Mazungumzo baina ya vyama viwili yalichukua muda wa miezi saba kabla ya kufikia mapatano na hivyo kuundwa kwa serikali.

Mahusiano baina ya vyama viwili yamekuwa ya wasiwasi kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita huku wanasiasa hasimu wakilumbana kwa maneno makali na wakati mwingine hatakupigana.

Democratic Republic of the Congo's newly inaugurated President Felix Tshisekedi (R) walks off the podium with outgoing President Joseph Kabila

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais Tshisekedi amelazimika kufanya kazi na washirika wa mtangulizi wake Joseph Kabila (kushoto)

Lakini inaonekana inaonekana kulikuwa na uamuzi wa kutaka muungano huu ufanye kazi.

Tangu alipochukua mamlaka, Rais Tshisekedi alibuni mazingira ya kisiasa ambayo yalikua kinyume na yale ya miaka ya mwisho ya utawala wa Bw Kabila.

Wafungwa wa kisiasa waliachiliwa na wapinzani muhimu, ambao walikuwa wanaishi uhamishoni wamerejea nchini, ambako sasa wanaendesha shughuli zao za kisiasa bila uoga wa ghasia za ukandamizaji.