Virusi vya corona: Makahaba wahangaika kwa ukosefu wa chakula

Makaba

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Familia za makahaba Uganda za kumbwa na uhaba wa chakula

Hatua zilizochukuliwa kama njia ya kuzuia kuenea kwa virusi vya corona zimewafanya watu kote barani Afrika kuhangaika wasijue la kufanya kwasababu ya kupoteza kazi zao na ajira.

Nchini Uganda, marufuku ya usafiri na kutotoka nje usiku imekuwepo kwa karibia miezi miwili sasa lakini serikali ya nchi hiyo imekuwa ikitoa chakula cha msaada kwa walioathirika zaidi na hatua hizo.

Wizara ya Afya nchini humo (Alhamisi) imethibitisha waathirika 218 wa ugonjwa wa Covid-19 lakini hadi kufikia sasa hakuna kifo chochote ambacho kimeripotiwa.

Kwa mujibu wa mwanahabari wa BBC Patience Atuhaire katika mji wa Kampala, miongoni mwa walioathirika zaidi katika hatua zilizochukuliwa na serikali ni wanaofanya kazi ya ukahaba - kundi lililo katika hatari ya kupata virusi vya ukimwi huku baadhi yao wakiwa wameacha kunywa dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi wanazopokea katika hospitali za umma bila malipo.

Je sheria inasemaje kuhusu biashara hii
Maelezo ya picha, Makahaba ni miongoni mwa walioathirika pakubwa na janga la virusi vya corona

Mwanahabari Patience Atuhaire alitembelea eneo la vitongoji duni la kaskazini mwa mji mkuu.

Eneo hilo la Bwaise ni maarufu sana kama makazi ya makahaba na wanapoendesha shughuli zao. Wanawake wengi katika eneo hilo wamekuwa wakifanya kazi hiyo kwa miaka mingi na kuweza kukidhi mahitaji ya familia zao.

Lakini janga la virusi vya corona kwa sasa hivi linafanya kazi hiyo kuwa hata ngumu zaidi huku wengine wakiamua kuhatarisha maisha yao.

Mwanahabri Atuhaire alimtembelea Joelia Namiiro, mkaazi wa eneo hilo mita chache kutoka barabara kuu nyuma tu ya maduka.

Chumba chake kikiwa kimenakshiwa vizuri pamoja na kitanda chenye chandarua cha kuzuia mbu.

Joelia Namiiro, kazi yake ni ukahaba na pia anaishi na virusi vya ukimwi. Kawaida, kazi yake inamuhitaji kuwa kwa ukaribu na wateja wake. Lakini miongozo ya sasa hivi ya shirika la afya nchini humo kunamlazimisha kufanya maamuzi magumu.

Kahaba

Joelia anasema kunapokucha watoto wanaanza kulia kwa njaa, hiyo ni kwasababu hawakupata chakula cha usiku. Kisha anaanza kujiuliza kama itawezekana yeye kuketi tu nyumbani?

''Mimi sina la kufanya zaidi ya kuhatarisha maisha yangu na kumuachia Mola mengine yote.''

Joelia anakiri kwamba amekuwa akihatarisha maisha yake na kwenda kazini usiku kwasababu ni lazima watoto wapate chakula.

''Watoto wangu hawatakufa kwasababu nina wasiwasi wa kupata ugonjwa wa Covid-19.''

Mama huyo mwenye umri wa miaka 30 pia ameacha kunywa dawa za kuzuia makali ya ugonjwa wa virusi vya corona.

Alipata fursa ya kumuonesha Patience Atuhaire kichupa chake cha dawa, ambacho kimefungwa vizuri.

Kutokuwa na mapato ya uhakika kuna maanisha kwamba familia yake inaweza tu kupata chakula iwapo atapata mteja - na nyakati za hivi karibuni wateja wamekuwa kama haluwa kupatikana.

Na sasa basi badala ya kunywa dawa kama inavyotakikana, ameacha kabisa kuzitumia.

Joelia anasema kwamba aliacha kunywa dawa hizo za ARVs kwa sababu hawezi kuzinywa akiwa na njaa.

''Serikali iliweka angalizo katika kukabilina na Covid-19 na kusahau kwamba kuna watu ambao tayari walikuwa wanaishi na magonjwa mengine. Mimi nina virusi vya ukimwi; kuna wengine wenye ugonjwa wa kifua kikuu ambao pia wanatakikana kunywa dawa, lakini hakuna anayeangalia changamoto zetu.''

Bi Joelia anaongeza kwamba hata wakati hatua ya kusalia ndani ilipoanza, walikuwa na changamoto ya kufikia kliniki kuchukua dawa zao kama kawaida. Na ingawa sasa hivi wako nazo, hawezi kuzinywa ikiwa tumbo halijapata chakula chochote.

Aisha pia humtunza dada yake

Chanzo cha picha, BBC

Maelezo ya picha, Makahaba pia nao wanamahitaji kama watu wengine na cha msingi zaidi wanatakiwa kukimu familia zao. Je hilo litawezekana vipi bila kupata wateja?

Akisongea nyumba kidogo tu mbele yake mwanahabari wa BBC alifika nyumbani kwa Doreen Mutoni, ambaye pia anafanya kazi ya ukahaba na ni mshauri wa vijana wa chama cha makahaba eneo hilo.

Wakati huo alikuwa anafua nguo za watoto wake mbele ya nyumba yake ndogo huku akiwa anapika maharagwe kwenye jiko la mkaa karibu nae. Hicho ndio chakula pekee alichokuwa nacho kwa famila yake siku ile.

Bi Mutoni akizungumzia ukosefu wa chakula, alisema kuna wakati utafika watu watasikia kwamba watoto wao wamekufa kwa njaa majumbani.

''Watoto watakufa, sio kwa Covid bali kwa njaa.'' Mutoni amesema.

Mutoni anaongeza kuwa kwa jinsi eneo analoishi lilivyo furika maji, kwa siku ya kawaida angekuwa amepikia watoto wake chai kama njia moja ya kuhakikisha wanapata joto.

''Lakini sinahata sukari. Hatuna hata chakula; ukipata chakula, mara utaona huna mkaa wa kupikia. Ukiwa na pesa ya kununua mkaa, utakosa hata pesa ya kununua chumvi.''

Mutoni anasema mambo yakiwa magumu sana anapigia wateja wake simu pengine siku hiyo unaweza kupata pesa kidogo.

Kwa Mutoni, yeye bado anaweza kumudu kunywa dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi lakini ana wasiwasi kwamba hali ikiendelea hivyo anaweza kufika mahali akashindwa hata kunywa dawa hizo.

Wengi miongoni mwa wafanyabiashara ya ngono Mombasa hutegemea zaidi madereva wa malori wanaotumia barabara ya Nairobi-Mombasa kupata mapato
Maelezo ya picha, Nchini Uganda baadhi ya makahaba wamedokeza kwamba hali ikiendelea jinsi ilivyo ipi siku watu watasikia watoto wao wamekufa kwa njaa wala sio Covid-19

Kulingana natakwimu rasmi, makahaba wanaoishi na virusi vya ukimwi ni asilimia 37 ikilinganishwa na wastani wa taifa wa asilimia 5.7.

Uganda imefanikiwa kupunguza kuenea kwa virusi vya UKIMWI kwa sababu ya kuangazia zaidi walio katika hatari kama vile wanaofanya kazi ya ukahaba.

Dkt. Stephen Watiti, mwanaharakati mashuhuri anayetetea haki za wenye virusi vya ukimwi anahofia kwamba changamoto za janga la Covid-19 huenda zikarejesha nyuma hatua zilizopigwa katika kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi.

Mwanaharakati huyo alithibitisha kuwa kuna wafanyakazi wengi wa ukahaba walioacha kunywa dawa zao ambao wanaomba usaidizi.

Aidha, dkt. Watiti anasema amekuwa akielezea walioathirika na virusi vya ukimwi kwamba ni lazima wale kwanza kabla ya kunywa dawa za kupunguza makali ya virusi vuua ukimwi. Anakiri kuwa tatizo kubwa ni kuwa ukinywa dawa hizo bila kula zinakudhuru.

Coronavirus

Na tatizo jingine, virusi vikiwa juu, kuna wale watakao amka na kujikuta wamepata magonjwa mengine ya kuambukiza kama vile homa ya uti wa mgongo na mengineo.

Katika kipiindi cha wiki mbili za mwanzo za mwezi Machi, Uganda imekuwa ikitekeleza hatua ya kusalia ndani.

Zaidi ya wafanyakazi 100 walikamatwa na polisi katika maeneo mbalimbali nchini humo wakiwa kazini kulingana na chama chao.

Lakini kwa wanawake wengine kama wa eneo la Bwaise kukamatwa kwao sio tatizo na wengi wao wanahatarisha maisha yao.Ameongeza kuwa unapoacha kunywa dawa ya kupunguza makali ya virusi vya ukimwi, virusi vinaongezeka zaidi na hivyo basi uwezo wao wa kuambukizwa wengine pia nao unaongezeka.