Virusi vya Corona vinasambaa kabla mwathirika kutambuwa ameambukizwa

Medical team members heading to Wuhan to reinforce hospitals fighting the coronavirus outbreak bid farewell to family members as they board the train at Nanjing South Railway Station in Nanjing City,

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Madaktari wakiaga familia zao kuelekea mji wa Wuhan kuimarisha juhudi za kukabiliana na virusi vya Corona
Muda wa kusoma: Dakika 2

Virusi vipya ya Corona ambavyo vimesambaa kwa watu karibia 2000 vinaambukiza wakati wa kuatamia mayai - na dalili zinakuwa bado hazijaanza kujitokeza na kufanya iwe vigumu kudhibitika, wamesema maafisa wa China.

Baadhi ya watu 56 wameaga dunia kwasababu ya virusi hivyo. Waziri wa afya Ma Xiaowei amewaambia wanahabari kwamba uwezo wa virusi hivyo kusambaa na unaonekana kuongezeka.

Baadhi ya miji ya Uchina imepiga marufuku kabisa usafiri wa sehemu moja hadi nyingine.

Mji wa Wuhan uliopo Hubei, chanzo cha mlipuko wa virusi hivyo kwa sasa umefungiwa kabisa.

Maambukizi yako katika kiwango ambacho ni vigumu kudhibitika", amesema Ma Xiaowei.

Maafisa wameahidi kuongeza juhudi mara dufu za kudhibiti virusi hivyo na kutangaza kwamba biashara ya kuuza wanyama wote wa porini itapigwa marufuku kuanzia leo Jumapili.

Virusi hivyo vinaaminika kwamba vimetokana na wanyama na vimesambaa kwa haraka kati ya wanadamu.

Kipindi cha kuatamia mayai wakati ambao mtu ameambukizwa virusi lakini hakuna dalili zozote zinazojitokeza ni kati ya siku 1 hadi 14, maafisa wanaamini hivyo.

Bila ya kujitokeza kwa dalili mtu hawezi kufahamu ikiwa ameambukizwa virusi vya Corona lakini pia vinaweza kusambaa kwa wakati huo huo.

Presentational grey line

Vizuizi vya barabarani na ukaguzi katika mpaka wa Hubei

Na Stephen McDonnell, Mwanahabari wa BBC Uchina

katika barabara zinazoelekea mji wa Nanyang, watu wanakaguliwa. Yeyote ambaye ni mgonjwa haruhusiwi kuingia kwenye mji huo. Magari yenye namba zi miji mingine pia yanafuatiliwa kwa karibu.

Ndani ya mji huo, hoteli hazikubali wasafiri kutoka mji wa Hudei chimbuko la virusi vya Corona

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Kwa sasa miji mingi ya Uchina imeweka sheria kali za usafiri.

Baadhi ya miji na vijiji haviruhusu mtu mwengine yeyote kuingia isipokuwa wenyeji pekee.

Maafisa kote nchini humo wanachukua hatua kali na kwa haraka ili kupunguza usambaaji wa virusi hivyo vinavyosababisha kifo.

Presentational grey line

Hali ikoje mjini Wuhan?

Sophie, kutoka Uingereza yuko mjini Wuhan. Ameliambia shirika la BBC: "Tumekwama."

"Tumekuwa tu ndani ya nyumba kwa siku nne. Tulifahamu kuhusu virusi vya Corona Desemba 31. Na hali inaendelea kuwa mbaya kila uchao," amesema.

"Inatia hofu, tumesikia kwamba virusi hivi vinaweza kuwa ndani ya mwili kwa wiki mbili bila ya mtu kuonesha dalili zozote za kuugua.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

"Kwa sasa tunafuatiliwa kwa karibu na familia zetu zimeingiwa na hofu."

Taxi hazipatikani barabara na kwa sasa madereza wa kujitolea wanapeleka watu katika hospitali zilizojaa wagonjwa.

"Hakuna magari kwa hiyo tumejitolea kupeleka watu wenye uhitaji hospitalini na kuwarejesha, na baadaye tutapata kinga dhidi ya maambukizi bila malipo, ," Yin Yu ameliambia shirika la habari la AFP.

"Tuko salama," dereva mwengine, Zhang Lin, amesema. "Lazima kuwe na mtu wa kufanya haya. Sisi tumetoka Wuhan, na pia nyinyi wanahabari muko hapa kutusaidia, raia wetu pia wanastahili kujitokeza kusaidia. Hili ni jukumu letu."

Hivi ni virusi gani?

Virusi vyenyewe ni vipya - ambavyo huathiri wanyama.

Virusi hivi vinasababisha matatizo ya kupumua.

Dalili zake zinasemekana kuwa homa, kikohozi kikavu kisha baada ya wiki moja, mwathirika anakuwa na matatizo ya kupumua na kuhitaji matibabu kwa haraka.

Virusi hivyo vipya vinafananishwa na vile vya Sars, ambavyo vilisababisha vifo vya mamia ya watu 2003.

Hadi kufikia sasa, bado hakuna tiba maalum au chanjo dhidi ya virusi hivi.

Na kufikia Jumamosi, nchini Uchina kulikuwa na visa 1975 vilivyothibitishwa vya ugonjwa huo huku visa 2,684 zaidi vikishukiwa kuwa ni virusi hivyo, kulingana na Tume ya Taifa ya Afya ya Uchina.