Papa Francis aondoa kiapo cha siri kwa visa vya unyanyasaji wa kingono

Pope Francis, Juni 2019

Chanzo cha picha, Reuters

Papa Francis amefanya mabadiliko ya vile ambavyo kanisa Katoliki inavyokabiliana na visa vya unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto kwa kuondoa kiapo cha siri.

Kulingana na sheria hii mpya, imeondoa ile sheria ya kukaa kimya licha ya kufahamu kinachoendelea kwa wale waliotoa taarifa ya unyanyasaji ama wanaokiri kwamba wamekuwa waathirika.

Viongozi wa kanisani walitaka sheria hiyo iondolewe katika mkutano uliofanyika Februari, mjini Vatican.

''Taarifa za visa vya unyanyasaji bado vinastahili kushughulikiwa kwa uangalifu, uadili na kisiri'', Papa amesema.

Pia ameagiza maafisa wa Vatican kutii sheria za kiraia huku wakiendeleza usiri wa jambo hilo na kusaidia mamlaka za kiraia katika uchunguzi wa kesi hizo.

Papa pia amebadilisha maana ya ponografia ya watoto kulingana na Kanisa Katoliki na kuongeza umri katika suala hilo kutoka miaka 14 au chini yake hadi miaka 18 au chini ya umri huo.

''Kiapo cha usiri kilikuwa sheria chini ya usiri ambacho kililinda taarifa nyeti zenye kuhusishwa na utawala wa Kanisa, sawa na hadhi ya neno hilo kama linavyotumika katika makampuni, au serikali za kiraia'', limesema Kanisa Katoliki.

Uchambuzi na Mhariri wa Masuala ya Kidini: Martin Bashir

Katika siku ya kuzaliwa alipokuwa anatimiza miaka 83, Papa Francis amejibu malalamishi ya muda mrefu ya manusura wa unyanyasaji wa kingono na kutangaza kwamba ushuhuda wowote utakaotolewa Kanisani wenye kuhusishwa na visa vya unyanyasaji wa kijinsia, unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto, na ponografia ya watoto kwa sasa utakuwa unawasilishwa katika mamlaka za serikali.

Kipindi cha nyuma, Kanisa Katoliki limekuwa likishutumiwa kwa kiapo hicho cha usiri kama kigezo cha kutoripoti visa vya unyanyasaji wa kijinsia. Awali, ilikuwa vigumu kutoa ushrikiano kwa serikali kwasababu ingechukuliwa kama ukukiukaji wa sheria hiyo ya kiapo ambako kwa sasa kumeondolewa.

Hii ni hatua ya hivi karibuni zaidi kuchukuliwa na Kanisa Katholiki kushughulikia udhalimu uliotekelezwa na makasisi ambao umejitokeza katika maeneo mbalimbali kote duniani pamoja na kwenye taasisi za kidini.

Pia unaweza kusoma:

Mtatuzi wa suala la unyanyasaji wa kingono, Askofu Charles Scicluna of Malta, ameongeza katika taarifa hiyo ya leo Jumanne, kwamba ikiwa Kanisa hilo litapokea ombi maalum kutoka kwa serikali, basi kuanzia sasa, Kanisa litatoa ushirikiano.