Genge la wauza dawa za kulevya Mexico wazua vita kumpamania mtoto wa El Chapo

Chanzo cha picha, Reuters
Vurugu kubwa imeibuka kaskazini mwa Mexico mara baada ya askari kumkamata mtoto wa mfanyabiashara nguli wa dawa za kulevya Joaquín "El Chapo" Guzmán ambaye anatumikia kifungo.
Mapigano hayo yalichukua muda wa saa kadhaa baada ya Ovidio Guzmán López kukamatwa kwenye doria ya kawaida katika mji wa Culiacán.
Picha za video zikionyeshwa wanaume wenye silaha wakiwa wanapambana na polisi, miili ya watu pamoja na magari yaliochomwa moto yakiwa yamefunga barabara.
Bwana Guzmán aliachiwa huru muda mfupi baadae ili kuzuia vurugu kuendelea, mamlaka imeeleza.
Waziri wa ulinzi nchini Mexico, Alfonso Durazo alisema kwamba oparesheni hiyo ilianza kutumia silaha wakati wakiwa ndani ya nyumba ambayo bwana Guzmán alikuwa ameshikiliwa,
Hivyo iliwalazimu kutumia silaha kwa ajili ya usalama wao.
"Walifanikiwa kumkamata bwana Guzmán lakini baadae aliachiwa huru, lakini ili kuzuia mapigano hayo kuendelea katika eneo hilo na kuzuia mauaji ya watu ilibidi wamuachie huru ili kurejesha amani katika mji huo", bwana Durazo alisema.

Chanzo cha picha, Reuters
Rais wa Mexico, Andrés Manuel López Obrador alisema kuwa ataandaa mkutano na kamati ya usalama kujadili suala hilo.
Bwana Obrador alichaguliwa katika jukwaa la kukabiliana na dawa za kulevya nchini humo na kuanzisha jeshi la usalama la kitaifa ili kupambana na wasambazaji hao.
Chini ya uongozi wa El Chapo, wafanyabiashara wa dawa za kulevya wa Sinaloa ndio alikuwa msambazaji mkubwa wa dawa za kulevya kuelekea Marekani, mamlaka yaeleza.
Na sasa El Chapo akiwa gerezani, wafanyabiashara hao walidaiwa kusimamiwa na Ovidio Guzmán, ambaye anashutumiwa kwa usambazaji wa dawa za kulevya nchini Marekani.
Jambo gani lilitokea Culiacán?
Serikali ilisema kuwa Ovidio Guzmán alipatikana katika doria ya kawaida ya polisi.
Kundi la wafanyabiashara wa dawa za kulevya walianzisha mashambulizi makubwa kwa polisi ili kujaribu kumuokoa kiongozi wao.

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images
Ovidio Guzmán, alisemekana kuwa kiongozi wa kundi la Sinaloa , baada ya baba yake kufungwa akiwa na miaka 20 .
Guzmán anatafutwa Mareani kwa mashtaka yanayohusika na dawa za kulevya, vyombo vya habari vya Mexico vimeripoti.
Mapambano ya kumtaka Ovidio Guzmán kuachiwa huru kwa kuvamia ofisi za mwendesha mashtaka na kuendesha mashambulizi katika maeneo mbalimbali ya mji.
Hakukuwa na taarifa rasmi ya idadi ya watu ambao wamekufa katika mapigano hayo.
Maafisa wa serikali waliliambia shirika la habari la Reuters kuwa baadhi ya maafisa walikuwa wamejeruhiwa bila kutaja idadi yao au kueleza hali yao ilikuaje.

Chanzo cha picha, EPA


Mkuu wa ulinzi wa jimbo la Sinalo, Cristobal Castaneda aliiambia kituo cha televisheni cha Televisa Network kuwa watu wawili wameuawa na wengine 21 kujeruhiwa.
El Chapo mwenye umri wa miaka 62 alikutwa na hatia mjini New York kwa makosa 10, yakiwemo usafirishaji wa dawa za kulevya na utakatishaji fedha.













