Nchi gani ina wahamiaji wengi zaidi duniani?

Wahamiaji kutoka Amerika ya kati wakiwa juu ya Gari moshi wakielekea nchini Marekani

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Idadi ya wahamiaji ni chini ya 4% ya idadi ya watu duniani

Uhamiaji ni moja kati ya mada zinazoleta mvutano katika nyakati hizi.

Lakini sababu ya kutokea kwa wimbi kubwa la wahamiaji duniani zinaweza kukushangaza.

Ulikua ukifahamu, kwa mfano, chini ya 4% ya watu duniani wanaishi katika nchi tofauti na walipozaliwa?

''Kumekua na mazungumzo mengi kuhusu wimbi la uhamiaji, lakini idadi inaonesha hadithi nyingine tofauti,'' Mtaalamu wa masuala ya idadi ya watu Gilles Pison ameiambia BBC

Mtafiti Pison,ni mtafiti wa masuala ya uhamiaji duniani.Moja kati ya mahitimisho yake ni kuwa mtazamo kuhusu uhamiaji unaweza kutofautiana kwa kiasi kikubwa kutokana na taarifa zinazopatikana kuhusu idadi ya watu wanaohamia.

Anatumia mfano wa kile kilichoitwa wimbi la uhamiaji Ulaya mwaka 2015, ambalo lilisababishwa na ukosefu wa utulivu katika nchi za mashariki ya kati kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.

''Pamoja na wingi wake hasusani barani Ulaya, wahamiaji walianza kuingia kwa wingi tangu mwaka 2015 kutokana na mizozo ya mashariki ya kati, bado mtazamo kuhusu uhamiaji kimataifa haujabadilika,'' Pison anaaeleza.

''Umoja wa mataifa unasema inakadiriwa kuwa kulikuwa na wahamiaji wanaokisiwa kuwa milioni 258 mwaka 2017,sawa na (3.4%) idadi ndogo ikilinganishwa na idadi ya watu duniani.''

''Kiasi hiki kimeongezeka kiasi katika kipindi cha miongo kadhaa-miaka 30 iliyopita, mwaka 1990 ilikuwa 2.9% na mwaka 1965 ilikuwa 2.3%.mabadiliko ni kidogo katika kipindi cha miaka 100,''alieleza

Famialia ya wahamiaji

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wahamiaji wa Afghanistan nchini Pakistani

Ulaya ina nchi tatu ambazo ziko kwenye nafasi kumi za kwanza zenye idadi kubwa ya wahamiaji:Uswisi,Uingereza na Uhispania

Lakini Uhispania ni nchi mpya kwenye ambayo wahamiaji huingia kwa wingi.

''Uhispania ilikua nchi iliyokua na wahamaji mpaka mwishoni mwa miaka ya 1980,lakini sasa ina takriban 13% ya watu wake ni wahamiaji, karibu sawa na Marekani,'' anaeleza Pison

Lakini vipi kwa nchi ambazo zinashuhudia watu wake wakihama?

Haitashtusha kuiona India ikiongoza kwa idadi kubwa ya watu wake kuishi nje ya nchi, Watu takribani milioni 16 wanaishi nje ya India-zaidi kidogo ya 1% ya idadi ya watu nchini humo-ikifuatiwa na Mexico, watu milioni 12.5 wanaoishi nje ya nchi hiyo, yaani katika kila raia 10 wa Mexico , mmoja anaishi nje ya nchi hiyo.

Uhamiaji ni mada inayogusa nchi nyingi duniani na kumekua na hofu kuhusu suala hilo

Utafiti wa Pison pia unabainisha nchi ambazo zina sifa ya kutoa na kupokea wahamiaji, mfano ni Uingereza, ambayo suala la uhamiaji limekua kwenye ajenda za kisiasa, na zimechukua nafasi kubwa kwenye maamuzi ya nchi hiyo katika kupiga kura katika kuondoka kwenye umoja wa Ulaya.

Waingereza ina wahamiaji milioni 8.4 lakini pia raia wa nchi hiyo milioni 4.7 wanaishi nje ya nchi hiyo.