Mikebe ya Coca Cola yagunduliwa kuwa na kinyesi cha binadamu

Coca Cola

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Coca Cola

Polisi wameanzisha uchunguzi wa kile kilichoonekana kuwa kinyesi cha binadamnu, kupatikana kwenye mikebe ya kujazwa soda iliyowasilishwa kwa kiwanda cha Coca Cola huko Ireland kaskazini.

Shughuli za usiku katika kiwanda cha Lisburn zilivurugwa wiki iliyopita wakati mashinde zilikwama.

Kampuni hiyo ilisema kuwa kisa hicho hakikuathiri vinywaji vyovyote ambavyo kwa sasa viko sokoni.

Polisi wanachunguza ripoti kuwa mikebe mingi huenda ilichafuka.

Coca-Cola ina kiwanda kikubwa huko Lisburn

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Coca-Cola ina kiwanda kikubwa huko Lisburn
Kiwanda cha Coca Cola cha Knockmore, Lisburn

Chanzo cha picha, Albert Bridge

Maelezo ya picha, Kiwanda cha Coca Cola cha Knockmore, Lisburn

Msemaji wa Coca-Cola amesema kuwa kampuni hiyo ilikuwa ikifahamu kisa hicho cha mikebe mitupu katika kiwanda cha Knockmore.

"Tatizo hilo lilitambuliwa mara moja na bidhaa zote zilizoathirika kuzuiwa na haziwezi kuuzwa. Hiki ni kisa kilicho kando na hakiathiri biddaa zozote zilizo sokoni."msemaji wa Coca Coa alisema.