Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mzee aweka tangazo kumtafuta mke Tanzania
Mzee wa miaka 75 nchini Tanzania ameweka bango lenye sifa za mke anayemtaka, katikati ya mtaa anaoishi.
Athuman Bakari Mchambua mkazi wa Dar es Salaam amechukua hatua hiyo baada ya kifo cha mke wake.
Amesema hawezi kutumia njia nyingine yoyote isipokua udahili ama mahojiano kumpata mke.
Mwandishi wa BBC Munira Hussein alimtembelea nyumbani kwake na kuandaa taarifa hii.