Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mzee aliye na wake wanane na watoto 70 Tanzania
Nchini Tanzania katika mkoa wa Arusha wilayani Monduli, mzee mwenye zaidi ya miaka 100 ana watoto zaidi ya 70 na wajukuu 300.
Mzee Meshuko Ole Mapi, almaarufu Mzee Laibon, amelazimika kuwa na shule yake na soko kwa ajili ya jamii yake hiyo na anasema bado ana azma ya kuendelea kuoa,
Watu kutoka mataifa mbali mbali hufika kumtembelea mzee huyo kama sehemu ya utalii.
Na Mwandishi wa BBC Esther Namuhisa alimtembelea mzee huyo Kaskazini mwa Tanzania.