Jinsi Chuo Kikuu cha MUST Tanzania kinavyowasaidia wanafunzi kuwa wajasiriamali

Jinsi Chuo Kikuu cha MUST Tanzania kinavyowasaidia wanafunzi kuwa wajasiriamali

Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (Mbeya University of Science and Technology - MUST) kimekuwa chuo cha mfano katika kuhawilisha teknolojia kwa wanafunzi.

Chuo hiki kinahakikisha mwanafunzi anapoingia chuoni hapo anapeleka wazo la biashara/kampuni yake anayotaka kuifungua na chuo humsaidia katika usajili na uendelezaji wa wazo hilo la biashara.

Wanafunzi huunda kampuni na kuendesha biashara zao wenyewe wakiwa wangali shuleni jambo linalo pungruza ukosefu wa ajira kwa wanafunzi wamalizapo elimu ya chuo kwani huendelea na Biashara zao walizozianzisha wakiwa chuoni.

Mwandishi wa BBC Frank Mavura amepata fursa ya kushuhudia kampuni chache alipokitembelea chuo hicho mkoani Mbeya, nchini Tanzania.