Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Sababu sita za kuwepo kwa utata kuhusu kumbukumbu ya maisha ya Prince Harry
Kumbukumbu ya Prince Harry, Spare, inaonesha mfululizo wa malalamiko na shutuma dhidi ya Familia ya Kifalme ya Uingereza.
Kitabu hicho kitaanza kuuzwa rasmi tarehe 10 Januari, lakini BBC News imepata nakala yake nchini Uhispania ambako imeanza kuuzwa kimakosa.
Simulizi ya Harry kwenye kitabu hicho ni pamoja na madai kwamba alishambuliwa kimwili na kaka yake mfululizo kuhusu mkewe Meghan.
Aliwaua wapiganaji 25 wa Taliban wakati akihudumu nchini Afghanistan, pamoja na kusema kwamba alitumia cocaine alipokuwa mdogo na alizungumza kuhusu mama yake, marehemu Princess Diana.
Kitabu hiki ni simulizi ya Harry.
Kensington Palace na Buckingham Palace zote zimesema hazitazungumza chochote.