Siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho: Fahamu wachezaji wote waliosajiliwa

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 7

01:05 Dario Osario ajiunga na Crystal Palace akitokea FC Midtjylland kwa mkopo.

Dirisha la usajili kwa klabu za Ligi Kuu ya Primia na English Football League (EFL) lilifungwa jana Jumanne saa 23:00 BST.

Tukufahamishe kwa kifupi mikataba yote iliyothibitishwa rasmi katika siku ya mwisho ya usajili, huku ukiendelea kufuatilia habari na tetesi za usajili zinazoendelea kujitokeza.

Pia kumbuka kuwa dirisha la usajili kwa klabu za Scottish Premiership litafungwa Alhamisi saa 17:00 BST, wakati klabu za Women's Super League (WSL) zitakuwa na muda hadi 23:00 BST siku hiyo hiyo kukamilisha usajili wao.

Usajili wa Ligi ya Premier – Septemba Mosi

01:01 Juan Riquelme Angulo amekamilisha uhamisho wake kwenda Sunderland akitokea Independiente del Valle kwa ada ambayo haijawekwa wazi.

00:45 Jean-Matteo Bahoya amehamia Leeds United kutoka Eintracht Frankfurt kwa mkopo.

00:45 Quinten Timber amejiunga na Crystal Palace akitokea Marseille kwa ada ambayo haijatangazwa.

00:15 David Affengruber amesajiliwa na Fulham kutoka Elche kwa ada ambayo haijawekwa wazi.

00:10 Ben Chilwell amejiunga na Crystal Palace akitokea RC Strasbourg kwa ada ambayo haijawekwa wazi.

00:00 Ainsley Maitland-Niles amehama kutoka Olympique Lyon kwenda Everton huku kima chake kikiwa hakijawekwa wazi

23:50 Enzo Fernandez ameondoka Chelsea na kujiunga na Manchester City kwa dau la pauni milioni 125, moja ya uhamisho mkubwa kabisa wa dirisha hili.

23:45 Christos Mouzakitis amehamia Hull City kutoka Olympiakos kwa kiasi cha fedha ambacho hakijawekwa wazi

23:41 Chema Andres amejiunga na Brighton & Hove Albion akitokea VfB Stuttgart kwa ada ya pauni milioni 15.5.

23:30 Sorba Thomas: Amehama kutoka Stoke City kwenda Hull City kwa ada ambayo haijawekwa wazi.

23:30 Zian Flemming: Amejiunga na Ipswich Town akitokea Burnley kwa dau linaloripotiwa kufikia pauni milioni 20.

23:15 Tosin Adarabioyo: Ameondoka Chelsea na kuhamia Tottenham Hotspur kwa ada ambayo haijatangazwa rasmi.

22:50 Jack Grealish: Amejiunga na Everton kwa mkopo akitokea Manchester City hadi mwisho wa msimu.

22:45 Melvin Bard: Amehamia Leeds United kutoka Nice kwa mkataba wa mkopo.

22:31 Robinio Vaz: Amejiunga na Hull City kwa mkopo akitokea AS Roma.

22:30 Manuel Angel: Amehama kutoka Real Madrid kwenda Fulham kwa ada ya takribani pauni milioni 3.

22:30 Hugo Larsson: Amejiunga na Fulham kwa mkopo akitokea Eintracht Frankfurt.

22:15 Brooke Norton-Cuffey: Amehamia Hull City kutoka Genoa kwa dau la pauni milioni 12.

22:05 Tim Iroegbunam: Ameondoka Everton na kujiunga na Hull City kwa ada ya pauni milioni 22.

22:00 Mykhailo Mudryk amejiunga na Tottenham Hotspur akitokea Chelsea kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.

21:00 Iliman Ndiaye amehamia Manchester City akitokea Everton kwa ada inayoripotiwa kufikia pauni milioni 65 (£65m).

20:00 Kevin Danso ameondoka Tottenham Hotspur na kujiunga na Sunderland kwa mkopo.

19:00 Lucca Brughmans amejiunga na Liverpool akitokea Genk kwa ada ya uhamisho ya takribani pauni milioni 30 (£30m).

15:00 Matias Fernandez-Pardo amekamilisha uhamisho wake kwenda Newcastle United akitokea Lille kwa ada ya karibu pauni milioni 51.4 (£51.4m).

13:20 Honest Ahanor amehamia Crystal Palace kutoka Atalanta kwa mkataba wa mkopo.

12:30 Taylor Harwood-Bellis amejiunga na Aston Villa akitokea Southampton kwa ada ya takribani pauni milioni 29 (£29m).

11:30 Ibrahim Mbaye amekamilisha uhamisho wake kutoka Paris Saint-Germain (PSG) kwenda Aston Villa kwa dau la pauni milioni 47 (£47m).

10:30 Ilyas Ansah amehamia Hull City akitokea Union Berlin kwa ada ambayo haijawekwa wazi.

Kimataifa

22:20 Cody Drameh ameondoka Hull City na kujiunga na AS Roma kwa ada ya takribani pauni milioni 3.4.

20:12 Nathan Patterson amehamia Torino kutoka Everton kwa ada ambayo haijawekwa wazi.

20:00 Wilfried Gnonto amejiunga na Fiorentina kwa mkopo akitokea Leeds United.

20:00 Robert Sanchez amehamia Como kwa mkopo kutoka Chelsea.

19:30 Dario Essugo amejiunga na Strasbourg kwa mkopo akitokea Chelsea.

19:30 Hwang Hee-chan amejiunga na Schalke 04 kwa mkopo akitokea Wolverhampton Wanderers.

19:11 Ethan Nwaneri amehamia Borussia Dortmund kwa mkopo kutoka Arsenal.

19:00 Deivid Washington ameondoka Chelsea na kujiunga na Strasbourg kwa ada ambayo haijawekwa wazi.

19:00: Lucca Brughmans amehamia Genk kwa mkopo akitokea Liverpool.

18:41 Nick Woltemade amejiunga na Juventus kwa mkopo kutoka Newcastle United.

18:00 David Moller Wolfe amejiunga na Hamburg kwa mkopo akitokea Wolverhampton Wanderers.

17:30 Cameron Archer amehamia Auxerre kwa mkopo kutoka Southampton.

17:24 Pape Matar Sarr amejiunga na Juventus kutoka Tottenham Hotspur kwa mkopo wenye sharti la kununuliwa moja kwa moja kwa pauni milioni 23.6.

17:00 Harvey Elliott amehamia Valencia kwa mkopo akitokea Liverpool.

17:00 Jean-Clair Todibo amejiunga na RC Lens kwa mkopo kutoka West Ham United.

17:00 Jakov Medic amejiunga na FC Utrecht akitokea Norwich City kwa mkopo.

16:00 Ivo Grbic ameondoka Sheffield United na kuhamia Ludogorets kwa ada ambayo haijawekwa wazi.

13:50 Gabriel Jesus amejiunga na Barcelona akitokea Arsenal kwa ada ya pauni milioni 8.6 (£8.6m).

12:00 Fabio Vieira amehamia Hamburg kutoka Arsenal kwa ada ya pauni milioni 8.6 (£8.6m).

11:00 Kota Takai ameondoka Tottenham Hotspur na kujiunga na Sint-Truidense VV kwa mkopo.

11:00 Sidnei Tavares amejiunga na Wisla Plock akitokea Blackburn Rovers kwa mkopo.

09:31 Marc Guiu ameondoka Chelsea na kuhamia RB Leipzig kwa ada ya takribani pauni milioni 14.6 (£14.6m).

08:45 Luis Semedo amehamia Clermont Foot kutoka Sunderland kwa ada ambayo haijawekwa wazi.

Ligi za Soka za England (EFL)

01:00 Raphael Borges Rodrigues amejiunga na Burton Albion kwa mkopo kutoka Coventry City.

00:45 Dane Scarlett ameondoka Tottenham Hotspur na kuhamia Leyton Orient kwa ada ambayo haijawekwa wazi.

00:32 Oliver Dovin amehamia Leyton Orient kwa mkopo akitokea Coventry City.

00:30 Oliver Skipp amejiunga na Charlton Athletic kwa mkopo kutoka Leicester City.

00:17 David Ozoh ameondoka Crystal Palace na kujiunga na Derby County kwa ada isiyofichuliwa.

00:05 Brian De Keersmaecker amehamia Bristol City kwa mkopo akitokea Oxford United.

00:00 Tyrese Shade amejiunga na Portsmouth kutoka Burton Albion kwa ada ambayo haijawekwa wazi.

23:48 Zech Obiero: Leyton Orient ➜ Gillingham (Mkopo)

23:45 Aidan Borland: Aston Villa ➜ Accrington Stanley (Mkopo)

23:45 Kamari Doyle: Brighton & Hove Albion ➜ Leicester City (Mkopo)

23:45 George Sebine: Huddersfield Town ➜ Rotherham United (Mkopo)

23:30 Connor Barron: Rangers ➜ Middlesbrough (Mkopo)

23:30 Dan Butler: Stevenage ➜ Swindon Town (Mkopo)

23:30 Liam Gibbs amejiunga na Preston North End akitokea Norwich City kwa mkopo.

23:30 Reo Hatate amehamia Burnley akitokea Celtic kwa ada ambayo haijawekwa wazi.

23:30 Johnny Kenny ameondoka Celtic na kujiunga na Preston North End kwa ada ambayo haijawekwa wazi.

23:30 Jay Williams amehamia Colchester United kutoka Crawley Town kwa ada ambayo haijawekwa wazi.

23:15 Myron Boadu amejiunga na Watford kama mchezaji huru baada ya kuwa bila klabu.

23:15 Eli King amehamia Gillingham akitokea Cardiff City kwa ada ambayo haijawekwa wazi.