‘Lugha ya Kiswahili ni tamu’

Maelezo ya video, Siku ya Kiswahili Duniani:“Lugha ya Kiswahili ni tamu’ Mzungu anayependa Kiswahili
‘Lugha ya Kiswahili ni tamu’

“Lugha ya Kiswahili ni tamu… pia kuna maneno ambayo ukisema na kizungu, haivutii kama vile ukisema kwa Kiswahili”

Elliot Berry almaarufu kama ‘mzungu mwitu’ ama ‘mwalimu wa Kiswahili’ ni mzaliwa wa Uingereza lakini amepata umaarufu nchini Kenya kwa ujuzi wake wa lugha ya Kiswahili japokuwa lafudhi yake imeshangaza wengi kwani ni ya jamii ya Waluhya kutoka Magharibi mwa Kenya.

Mwanahabari wetu @judith_wambare aliwasiliana naye akiwa mjini London na kupata kujua kwanini anapendelea Kiswahili kama lugha yake rasmi ya mawasiliano na maoni yake kuhusu kutengwa kwa siku rasmi ya Kiswahili ambayo ni tarehe 7 mwezi wa Julai