Zanzibar kuanzisha vituo maalumu vya kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia

Zanzibar kuanzisha vituo maalumu vya kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia

Zanzibar ipo mbioni kuanzisha vituo maalum vya kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia, huku takwimu za mwaka 2022 zikionyesha kuongezeka kwa vitendo hivyo na kufikia 1360.

Wengi wanaotajwa kuathirika na matukio haya ni wanawake na watoto.

Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani, mwandishi wa BBC David Nkya amefanya mahojiano maalum na mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Taasisi inayojihusisha na masuala ya kijamii ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mama Mariam Mwinyi nyumbani kwake Ikulu, Migombani.