Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Teknolojia ya kufua nguo kwa kuziloweka kwenye beseni kisha zinajisafisha zenyewe
Sijui kama unapenda kufua nguo au la? Lakini je, umeshawahi kutafakari kwamba unaweza ukaziweka nguo zako kwenye beseni na kuziloweka zijifue zenyewe?
Labda pengine unadhani nazungumzia mashine ya kufua nguo… La hasha!
Nchini Uganda, teknolojia mpya ya kufua nguo kwa kuziloweka kwenye beseni alafu zinajisafisha zenyewe imekuwa ni teknolojia maarufu sana na inayopendwa na wengi.
Beseni hilo maalumu limewapa kipato wanawake wanaofanya biashara ya kufua nguo nchini humo.
Mwandishi wa BBC Agness Penda ametuandalia taarifa hii kutoka jijini Kampala nchini Uganda.