Msani Ney wa Mitego afungiwa kufanya maonesho Tanzania

Ney
Maelezo ya sauti, Ney wa Mitego afungiwa kufanya 'Show' Tanzania

Msanii Emmanuel Elibariki maarufu kama ‘Nay wa Mitego’ wa Tanzania amefungukiwa kufanya matamasha nchini humo kutokana na wimbo wake wa ‘Amkeni’.

Ingawa hakusema amefungiwa kufanya matamasha kwa muda gani, Wakili wa Msanii huyo, Jebra Kambole ameithibitishia BBC kwamba Msanii huyo anatuhumiwa na vyombo viwili.

‘Moja kuna kinachoendelea BASATA (Baraza la Sanaa Tanzania) , na kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam, BASATA wana malalamiko wakisema wimbo alioutunga (Amkeni) unaonekana una maneno ya uchochezi, lakini sio hilo tu, wameufungia wimbo wenyewe na wamemkataza kufanya matamasha kwenye maeneo mbalimbali ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania’, alisema Kambole.

Kuhusu Polisi Jebra aliongeza; ‘Kinachoendelea Polisi ni kwamba jana aliitwa akipewa tuhuma kuhusiana na wimbo huo huo (Amkeni), ambao unaonekana una mashairi ambayo wao wanadhani kwamba ni ya uchochezi, tulitoa maelezo ya kwanini tunaona kwamba sio ya uchochezi na tukawaachia Polisi wafanye kazi yao’.

Mahojiano zaidi ya Kambole na BBC kupitia mwandishi wake Martha Saranga unaweza kusikiliza hapa.