Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tazama: Mnyoo ulivyovutwa kutoka kwenye ubongo wa mwanamke
Vimelea hivyo - ambavyo kwa kawaida hupatikana katika chatu – huenda vingekuwepo kwa miezi miwili, wanasayansi wanasema. wanasayansi wanasema mnyoo wa sm8 umepatikana hai katika ubongo wa mwanamke wa Australia, ikiwa ni mara ya kwanza duniani.
Myoo huo ulivutwa kutoka kwa sehemu ya mbele ya ubongo wa mgonjwa iliyoharibiwa wakati wa upasuaji huko Canberra mwaka jana.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 64, alikuwa na dalili kama maumivu ya tumbo, kikohozi na jasho la usiku, ambalo lilibadilika na kuwa kusahau na udhaifu.
Madaktari wanasema kuwa vimelea hivyo vyekundu vingeweza kuwa hai katika ubongo wake kwa hadi miezi miwili.