Haya ndio makao makuu ya kuku wa kukaanga duniani?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa nini mji mdogo wa Nakatsu - wenye takriban maduka 50 ya kuku aina ya "Karaage" - unachukuliwa kuwa na kuku bora zaidi wa kukaanga nchini Japani, na pengine duniani kote?
Karaage, kwa majin aya kijapan ni mojawapo ya chakula maarufu zaidi nchini Japani, ni aina laini na tata ya kuku wa kukaanga ambao ni chakula kikuu kote nchini humo.
Chakula hiki kitamu kinapendwa sana kiasi kwamba kila mwaka, mamia ya maelfu ya watu hupiga kura katika shindano maalumu la nchi nzima ili kubaini ni migahawa gani ya kuku wa 'Karaage' inayopika na kuandaa kuku watamu zaidi na kutoa huduma bora zaidi.
Ingawa migahawa kutoka miji mingine mikubwa kama Tokyo, Kyoto na Osaka hushiriki katika shindano hilo kubwa, lakini ni migahawa kutoka mji mmoja mdogo, Nakatsu City, ulioko katika mkoa wa Oita kwenye kisiwa cha Kyushu kusini, ambayo kwa kawaida hupata tuzo nyingi zaidi. Hushinda karibu kila mwaka
Shindano la 'Karaage Grand Prix' linavyochagiza utamu wa kuku

Chanzo cha picha, Karaage festival ExCo
Shindano la Karaage Grand Prix ni shindano la kila mwaka nchini Japani ambalo mshindi wake hujivunia kuwa ndio wenye kuku wa kukaanga watamu zaidi, wenye ladha nzuri zaidi, na karibu maduka ama migahawa 1,000 huingia kwenye shindano.
Hadi mwaka 2022, shindano hili limezidi kupata umaarufu, huku wakazi wa kawaida wakipata nafasi ya kupiga kura kwenye maeneo wanayopenda. Lakini mnamo 2023, sheria zinabadilika, majaji wanaletwa kwa ajili ya kuonja ladha, na taji la kweli la kuku watamu ama 'Karaage' bora hatimaye litazawadiwa.
Kwa nini mji huu mdogo wa Nakatsu unachukuliwa kuwa na kuku bora zaidi wa kukaanga duniani

Chanzo cha picha, Karaage festival ExCo
Pamoja kuongezwa kwa waonjaji, maduka na migahawa ya kuku wa Karaage ya Nakatsu City yana mengi zaidi ya kuthibitisha kuliko migahawa na maduka mingine duniani.
Ubora wa kuku wake unajengwa na namna wanavyowaunga wa kutumia viungo mbalimbali ikiwemo soya, tangawizi, chumvi, kitunguu saumu, matunda na viungo vingine ambavyo hutoa ladha nzuri kwa mlaji.
Upishi wake ni wa kitamaduni na wa kihistoria uliodumu miaka na miaka na vizazi na vizazi.
Na historia hiyo ya upishi wake wa kitamaduni unaufanya mji huu kujijengea sifa kama mji mkuu au makao makuu ya kuku wa kukaanga, ambapo papa sifa hiyo ya kuku wa kukaanga wa Karaage imevuka mipaka kutokana na kuwepo kwa muda mrefu.
Asili ya kuku wa Karaage

Chanzo cha picha, Karaage festival ExCo
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Kawaida watu hupanga foleni kuzunguka migahawa ama maduka ya kuuza kuku hawa kununu hasa kwa ajili ya wapendao. Inaonekana kama zawadi na kitu kikubwa cha thamani kumpelekea mtu.
Anthony Bourdain aliwahangaikia sana: "Nimezoea nyama hizi za kuku waliokaangwa sana... Ni jambo la kufurahisha. Ninajua mahali pa kupata Lawson katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Narita, na siwezi kuingia kwenye ndege bila kubeba kuku hawa."
Kuna hata filamu ya karaage iliyotayarishwa na Jumuiya ya Karaage ya Japan inayoita vitafunio hivyo kama "Chakula cha kitaifa".
Asili ya kuku hawa wa Karaage ilianzia Karne ya 16 wakati wamishonari Wareno walifika kwenye ufukwe wa Japani wa Kisiwa cha Kyushu kupitia bandari ya Nagasaki na kuleta mbinu zao za kukaanga.
Polepole, wakaazi wa Japani walianza kuiga baadhi ya mbinu hizi za Magharibi na kuongeza ubunifu wao wa upishi wa kitamaduni.
Lakini umaarufu wake hakuwa mkubwa hadi baada ya Vita vya Pili vya dunia ambapo kuku wa kukaanga, na haswa Karaage, ikawa msingi wa ubora wa kuku wa leo.
Baada ya vita, Japani iliharibiwa, uhaba wa chakula ulikuwa mkubwa, na kwa ukosefu wa mchele, lishe ya Wajapani ilibadilika sana. Tambi na pamoja kuku wa nyama, ambao ni kuku wanaofugwa kwa ajili ya nyama ndio vyakula vilivyokuw aangalau rahisi kuvipata. Unaweza kufuga kuku chini ya miezi miwili ukala nyama kuliko ng'ombe au nguruwe.

Chanzo cha picha, Karaage festival ExCo
Kisiwa cha Kyushu kilikuwa tayari kimejulikana kama kituo cha kuku (leo zaidi ya nusu ya kuku wote wa nyama hutoka Kyushu ) na mbinu mpya za kupikia nyama ya kuku zilianza haraka na kusaidia kulisha nchi zingine yenye njaa duniani.
Baada ya vita kuku wengi walifugwa na kuandaliwa hapo na kutumwa kwenye nchi zenye njaa duniani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Nakatsu Karaage Association, Masahiko Inoue, anaangalia shindano la Grand Prix ya 2023 pamoja na nafasi ya Nakatsu katika ulimwengu wa karaage.
"Mashindano yajayo ni muhimu kwa sababu watu watajua ni mgahawa ama duka gani ambalo kweli ni nambari moja. Lakini mwishowe, nataka kila mtu ajue kuwa kuku wetu 'Nakatsu karaage' ni wa kipekee. Na kwamba ina chapa inayoonyesha inatoka kwa Nakatsu."
Karaage inawakilisha ustahimilivu, inaonyesha ustadi, na ni ukumbusho wa jinsi Japani iliweza kupambana na matatizo. Na kwa wakaazi wa Nakatsu, ni chakula cha roho ambacho huhisi kama nyumbani.












