Yanga mbioni kuandikisha historia

Yanga mbioni kuandikisha historia

Jumapili hii, timu ya Yanga ya Tanzania itashuka dimbani katika fainali mkondo wa kwanza ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya USM Alger kutoka Algeria.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa jijini Dar es Salaam, huku ule wa marudiano ukipigwa Juni 3 jijini Algiers.

Timu hiyo inaendelea na mazoezi huku hamasa ikiwa ni kubwa.

Mwandishi wa BBC, Alfred Lasteck ametuandalia taarifa hii kutoka jijini Dar es Salaam.

Video: Eagan Salla