Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jinsi vijana wa pwani ya Kenya wanavyotumia michezo kuvutia watalii
Idadi kubwa ya watu wanaoishi katika maeneo ya pwani huchangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa dunia, mchango wao ukiwa na thamani ya takriban dola trilioni 1.5 za Kimarekani kwa mwaka, hii ni kwa mujibu wa Umoja wa mataifa. Mchango huu unatarajiwa kuongezeka maradufu hadi kufikia dola trilioni 3 ifikapo mwaka 2030.
Katika pwani ya Kenya, baadhi ya vijana wanatumia rasilimali ya bahari ili kujikwamua kiuchumi kupitia shughuli mbalimbali, ikiwemo kuvutia watalii kupitia michezo ya baharini.
Mwandishi wa BBC @frankmavura ametuandalia taarifa ifuatayo kutoka Mombasa, nchini Kenya.