Kupigwa na kutishiwa: Jinsi wanawake wa Uzbek wanavyolazimishwa kufanya kazi ya ngono nchini India

Maelezo ya video, Kupigwa, kutishwa, kutishiwa: Jinsi wanawake wa Uzbek wanavyolazimishwa kufanya kazi ya ng
Kupigwa na kutishiwa: Jinsi wanawake wa Uzbek wanavyolazimishwa kufanya kazi ya ngono nchini India
h

Wanawake wawili wa Uzbek waliolazimishwa kufanya kazi za ngono nchini India walifichua unyanyasaji, vitisho na ukatili ambao wamekuwa wakitendewa . Wakizungumza na BBC Hindi, walisema walipigwa na kutishiwa na walanguzi wa binadamu.

Polisi mjini Delhi waliwakamata wasafirishaji wawili wa binadamu huko Goa ambao waliwarubuni kutoka katika nchi maskini za Asia ya Kati kwa kuwaahidi ajira Dubai.

Washukiwa hao waliwapeleka India kupitia Nepal.

Wengi wao wanasema wanahisi "wamekwama" nchini India na hawawezi kuondoka nchini humo kutokana na kesi za kisheria dhidi yao, kwa madai ya kukiuka sheria za uhamiaji.

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi na kuhaririwa na Yusuf Jumah