Je unajua kuwa unywaji wa maziwa ya wanyama haukuwapo karne za nyuma?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Wanadamu wa awali hawakuweza kunywa maziwa ya wanyama wengine. Lakini sasa watu wengi wanaweza kunywa maziwa ya wanyama wengine.

Kwa nini mwanadamu aliweza kuhimili mageuzi ya maziwa ya wanyama hadi kufikia kiwango cha kuyanywa?

Maziwa ya wanyama yana washindani. 'Maziwa' mbadala yaliyotengenezwa kutoka kwa mimea ya soya au mlozi yanazidi kupata umaarufu.

Maziwa haya mbadala yanafaa kwa wale wanaoathiriwa na maziwa ya wanyama na wasiokula nyama.

Kuna mshindi wa pili mfululizo wa 2018 Uingereza ambaye alipatikana kwa kuuza maziwa ya mlozi katika ladha tofauti.

Lakini maziwa haya mbadala ni nyongeza mpya kwa historia ya uhusiano wa ustaarabu wa binadamu na maziwa ya wanyama.

Historia ya uhusiano huu ni ya maelfu ya miaka na imepitia misukosuko mingi hadi kufikia hapo.

Ikiwa unafikiri juu yake, maziwa ni kitu cha ajabu sana kunywa.

Ni kioevu kinachozalishwa na ng'ombe au mnyama mwingine ili kulisha watoto wake.

Ili kuyakusanya, mtu anapaswa kukamua kiwele cha ng'ombe.

Haijulikani vyema katika tamaduni nyingi.

Mwaka 2000, China ilizindua kampeni ya nchi nzima yenye lengo la kuhimiza watu kutumia zaidi maziwa na bidhaa za maziwa kwa ajili ya afya bora.

Raia wengi waandamizi wa China walikuwa na mashaka juu ya jambo hilo.

Kampeni hii ilifanywa ili kuondokana na mashaka yao. Jibini hutolewa kutoka kwa maziwa kupitia mchakato wa uchachushaji.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Tabia ya kunywa maziwa ni mpya kabisa katika miaka laki tatu ya historia ya mwanadamu.

Miaka elfu kumi iliyopita, hakuna mtu aliyekunywa maziwa isipokuwa mara chache tu.

Watumiaji wa awali wa maziwa walikuwa wakulima na wafugaji wa mapema wa Ulaya Magharibi—watu wa kwanza kunywa maziwa kutoka kwa wanyama wa kufugwa, ikiwa ni pamoja na ng’ombe.

Leo, kunywa maziwa ni kawaida sana katika Ulaya ya Kaskazini, Amerika ya Kaskazini na sehemu nyingine za dunia.

Chakula cha watoto

Kunywa maziwa ya wanyama sio kawaida kibayolojia.

Maziwa yana aina ya sukari inayoitwa lactose. Ni tofauti na sukari inayopatikana kwenye matunda na vyakula vingine vya sukari.

Tunapokuwa watoto, miili yetu huzalisha aina maalum ya kimeng'enya kiitwacho lactase ambacho hutusaidia kusaga lactose katika maziwa ya mama yetu.

Lakini bila kimeng’enya lactase katika mwili, hatuwezi kusaga vizuri lactose (sukari) katika maziwa. Kwa sababu ya hili, ikiwa mtu mzima ata kunywa kiasi kingi cha maziwa, inaweza kusababisha uchungu, maumivu ya tumbo na hata kuhara.

Hata hivyo, baada ya mageuzi kuanza kutokea katika miili watu wengi wanaweza kuhifadhi kimeng'enya chao cha lactase hadi wakiwa watu wazima.

Uwezo wa kumeng'enya sukari ya maziwa uliwawezesha kuendelea kunywa maziwa bila madhara yoyote.

Hili linawezekana kutokana na mabadiliko katika sehemu ya DNA inayodhibiti utendaji wa jeni la lactose.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

"Kwa mara ya kwanza kuona sehemu za jeni yenye kimeng'enya cha kusaga sukari ya maziwa huko Uropa ni karibu miaka 5,000 iliyopita huko kusini mwa Ulaya.

Na kisha ikawa inapatikana sana katika Ulaya ya Kati na miaka 3,000 iliyopita," alisema L'Sigurel, profesa msaidizi katika Jumba la Makumbusho la Humankind mjini Paris.

Jeni inayobaki kuwa hai katika maisha yote kwenye umeng’enyaji wa maziwa imekuwa ikibadilika na sasa hivi inapatikana kwa watu wengi. Zaidi ya asilimia 90 ya watu kaskazini mwa Ulaya wako nayo. Hali ni hiyo hiyo kwa Afrika na Mashariki ya Kati.

Kuna watu ambao jeni zao za kumeng’enya maziwa hufifia baada ya utoto, na kufanya umeng’enyaji wa bidhaa za maziwa kuwa ngumu na chungu.

Hii ikimaanisha wanaweza kunywa maziwa kiasi tu.

Faida za vyakula vya maziwa

Inaaminika kuwa kuna faida nyingine za kunywa maziwa mbali na thamani yake ya lishe.

Wale wanaofuga mifugo pia hupatana na magonjwa kama vile kimeta.

Kunywa maziwa ya ng'ombe kunaweza kutoa kingamwili dhidi ya maambukizo haya.

Hakika, maziwa yanachukuliwa kuwa faida muhimu kwa watoto wachanga wanaonyonyeshwa.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Lakini kukosekana kwa uwezo wa kumeng’enya sukari ya maziwa kunaweza kupunguza uwezekano wa kuw, mtu katika kundi la mifugo atakuwa na mabadiliko sahihi ya kijeni.

"Nadhani sehemu thabiti zaidi ya taswira hii ni kwamba kulikuwa na uhusiano kati ya ufugaji na mtindo wa maisha," Swallow alisema. "Lakini lazima uwe na mabadiliko ya kijeni kwanza."

Sio moja, lakini mambo kadhaa hufanya kazi ili kuongeza uwezo wa umeng’enyaji sukari ya maziwa. Swallow anapendekeza kwamba moja ya kipengele kinaweza kuwa thamani ya lishe ya maziwa, ambayo ina kiasi kikubwa cha mafuta, protini, sukari, na virutubisho vidogo kama vile kalsiamu na vitamini D.

Inaonekana zaidi kwamba mahitaji ya maziwa yanaongezeka katika eneo la Asia ambako watu wengi hawana uwezo wa kumeng’enya sukari ya maziwa.

Hata hivyo, watu huko hawajali suala la usagaji chakula au kuhisi haja ya kusindika maziwa kwa sababu ya faida zake.

Kwa hakika, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa linawashauri wakazi wa nchi zinazoendelea kufuga wanyama wa maziwa wasio wa kiasili ili kuwe na usambazaji wa maziwa hata kama maziwa ya ng'ombe yanakuwa ghali sana au hayapatikani.

Utafiti mkubwa uliochapishwa mnamo Januari 2019 unaelezea 'mlo wa sayari wenye afya' ambao ni mzuri kwa afya yetu na pia kwa mazingira.

Inapendekeza kupunguzwa kwa kiasi kikubwa kwa matumizi ya nyama na bidhaa nyingine za wanyama, na inasemekana kuwa na manufaa sawa na kunywa glasi ya maziwa kwa siku.

Mahitaji ya maziwa hayaondoki. Badala yake, mahitaji ya bidhaa hii bado yanaongezeka ama kuwe na kasi ya umeng’enyaji sukari ya maziwa au la katika miili yetu.