Burundi: Waathiriwa wa mafuriko wazungumza

Burundi: Waathiriwa wa mafuriko wazungumza

Yamekua ni maisha ya shida kwa Bi Nizigiyimana Shadi muathiriwa wa mafuruko katika mji wa Gatumba nchini Burundi.

Bi Nizigiyimana ni mmoja wa wakazi wanaoishi katika makazi ya muda baada ya wenzake kuhamishwa katika maeneo salama.

Mafuriko katika eneo hili yamekuwa yakitokea mara kwa mara kutokana na mto Rusizi kuvunja kingo zake na kupanda Kwa viwango vya maji katika Ziwa Tanganyika.

Aliielezea BBC masaibu aliyonayo kutokana na athari za mafuriko hayo.

Video: Egan Salla

Ripota: Dinnah Gahamanyi