Fahamu pete maalum ya kuzuia Ukimwi inavyofanya kazi

Fahamu pete maalum ya kuzuia Ukimwi inavyofanya kazi

Wataalamu nchini Kenya wanasema ipo haja ya kuzingatia njia tofauti za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi badala ya zile ambazo zimekuwa zikitumika kwa muda mrefu kama kumeza tembe za kila siku.

Ulimwengu unapoadhimisha siku ya Ukimwi Duniani Kenya inajivunia kuidhinisha matumizi ya pete ya maalum inayofahamika kwa kama Dapivirine ring katika vituo sita vya afya Kaunti za Nairobi, Mombasa na Kisumu ili kuwapa wanawake na wasichana chaguo zaidi ya moja ya kupambana na Ukimwi.

Lakini je, pete hii ni nini na inafanya kazi vipi?

Ambia Hirsi amezungumza na Caleb Owino mshauri wa kiufundi wa maswala ya Ukimwi.

Video: Anne Okumu