'Sijakata tamaa ya kuwa dereva licha ya kuupoteza mkono wangu kwenye ajali'

'Sijakata tamaa ya kuwa dereva licha ya kuupoteza mkono wangu kwenye ajali'

Halima Mbwana alikuwa mmoja kati ya madereva wachache wa kike wa mabasi yanayoenda mikoani nchin Tanzania, lakini ndoto yake ilififia ghafla mara baada ya kupata ajali na kupoteza mkono mmoja.

Lakini anasema kutokana na kuipenda sana kazi yake hajakata tamaa bado na anaamini atarudi katika sekta ya usafiri kwa namna yeyote hata kukatisha tiketi au kuendesha malori atakapofanikiwa kupata mkono wa bandia ambao anautarajia ukisimamiwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia, wanawake na makundi maalumu Doroth Gwajima

Video: Eagan salla