Tazama: Meli ya kivita ya China yaitishia ile ya Jeshi la Wanamaji la Marekani katika mkondo wa bahari wa Taiwan

Tazama: Meli ya kivita ya China yaitishia ile ya Jeshi la Wanamaji la Marekani katika mkondo wa bahari wa Taiwan

Jeshi la Wanamaji la Marekani linasema moja ya meli zake ililazimika kupunguza mwendo baada ya meli ya kivita ya China kukata maji mbele yake ghafla katika Mlango bahari wa Taiwan siku ya Jumamosi.

Meli hizo zilikuja umbali wa mita 137 kutoka kwa kila moja katika namna inayoelezwa kuwa "sio salama".

Wanamaji wa Marekani na Canada walikuwa wakifanya mazoezi ya pamoja katika bahari hiyo.