Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tazama: Wairan wanaokufa kwa sumu ya pombe na usiri
Wimbi jipya la unywaji wa pombe yenye sumu nchini Iran linaua watu ambao wanaogopa sana adhabu badala ya kutafuta msaada wa haraka wa matibabu.
Pombe imepigwa marufuku katika nchi hiyo ya Kiislamu (isipokuwa kwa baadhi ya dini ndogo), na watu wanaopatikana wakinywa pombe wanaweza kupata adhabu ya viboko 80, kifungo au hata kifo kwa wakosaji wa kurudia.
Marufuku hiyo imekuza unywaji wa pombe kinyemela - na isiyodhibitiwa - inayosambaza pombe kwa watumiaji, ambao hawana njia ya kujua wanakunywa nini haswa.
BBC Idhaa ya Kiajemi ilizungumza na babake msichana aliyefariki wiki mbili zilizopita baada ya kunywa pombe yenye sumu kali ya methanoli.