Video ya nadra inayoonyesha wavulana wa Korea Kaskazini wakihukumiwa kwa kutazama kipindi cha TV

Video ya nadra inayoonyesha wavulana wa Korea Kaskazini wakihukumiwa kwa kutazama kipindi cha TV

Picha za video zilizopatikana na BBC Korea zinaonyesha Korea Kaskazini ikiwahukumu hadharani wavulana wawili wa kiume kwa miaka 12 ya kazi ngumu kwa kutazama kipindi cha televisheni cha Korea Kusin cha K-dramas.

Picha hiyo ambayo inaonekana kuwa imerekodiwa mwaka 2022, inaonyesha wavulana wawili wenye umri wa miaka 16 wakiwa wamefungwa pingu mbele ya mamia ya wanafunzi katika uwanja wa nje.

Pia inaonyesha maafisa wa waliovaa sare wakiwakemea wavulana kwa "kutotafakari kwa kina makosa yao". Pyongyang imepiga marufuku matumizi ya burudani yoyote ya Korea Kusini ndani yan chi hiyo.