Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Huyu ndiye Panzi mzalendo Tanzania? mdudu wa kipekee mwenye rangi za bendera ya nchi
Panzi Tanzania ni panzi wa kipekee anayepatikana kwenye misitu wa mazingira asili wa Pugu Kazimzubwi uliopo mkoa wa Pwani nchini Tanzania, Panzi huyu amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na rangi zake asilia zenye kufanana za zile za bendera ya Tanzania hivyo kuvuta hisia za wengi wakitaka kujua imewezekanaje.
Msitu huu uliopo umbali wa kilomita 20 kutoka katika Jiji la Dar es Salaam pia unafahamika kwa jina la utani kama mapafu ya jiji la Dar es salaam kutokana na kuwa chanza muhimu cha hewa safi ya oksijeni kwa jiji hilo lenye watu takribani milioni saba
Mwandishi wa BBC Eagan Salla alitembelea msitu wa Pugu Kazimzumbwi na kuandaa taarifa ifuatayo...