Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ezekiel Kitiku: Aieleza BBC namna alivyopotezana na marafiki zake Israel
Serikali ya Israel imethibitisha utambulisho wa watu wawili kutoka Tanzania wanaoaminika kushikiliwa na Hamas tangu shambulio la Oktoba 7 dhidi ya jamii za kusini mwa Israel, karibu na mpaka na Gaza.
Joshua Loitu Mollel na Clemence Felix Mtenga walikuwa nchini Israel kama sehemu ya programu ya mafunzo ya kilimo, kulingana na taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel.
BBC imezungumza na Ezekiel Kitiku mmoja wa wanafunzi kutoka Tanzania anayeishi Israel kuhusu matukio ya siku ya shambulizi hilo na mara ya mwisho kuzungumza na wenzake wanaodaiwa kuzuiliwa na Hamas.