Madereva wanawake wanaoendesha malori katika barabara hatari zaidi nchini Mexico

Madereva wanawake wanaoendesha malori katika barabara hatari zaidi nchini Mexico

Chini ya 3% ya madereva wote wa malori duniani kote ni wanawake, ingawa waajiri wanakubali kuwa madereva wanawake ni madereva wenye ujuzi na kufuata sheria za usalama barabarani zaidi.

Lakini nchini Mexico, ambako unyanyasaji wa kijinsia na wizi wa kutumia silaha ni jambo la kawaida, imeonekana kuwa changamoto kuwavutia katika taaluma hiyo.

Makala ya Wanawake 100 wa BBC ilisafiri nao katika baadhi ya barabara hatari nchini humo.

Video hii imetayarishwa na kuhaririwa na Alvaro Alvarez.