Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mbunge wa zamani wa Arusha, Godbless Lema amesema atarejea nchini Tanzania wakati wowote
Godbless Lema, mjumbe wa kamati kuu ya chama cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania na mwenyekiti wa kanda ya Kaskazini, pia alikuwa mbunge wa Arusha mjini kwa miaka kumi mfululizo, amethibitisha kwamba atarejea nchini humo wakati wowote kuanzia sasa.
Kauli hiyo inakuja siku moja baada ya Serikali ya Tanzania kuwataka wapinzani walioondoka nchini humo na kwenda ughaibuni kwa kigezo cha ukosefu wa usalama kurejea nyumbani.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi hiyo, Hamad Yusuf Masauni, aliongeza kwamba hakuna mwanasiasa yeyote aliye katika tishio la usalama nchini Tanzania.
Lema na Tundu Lissu ambaye ni makamu mwenyekiti wa Chadema aliyewania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, walikimbia nchi hiyo mara baada ya uchaguzi kwa madai ya kuhofia usalama wao.
Lema alizungumza na Mwandishi wetu Regina Mziwanda