Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Godbless Lema:Aliyekuwa mbunge wa Arusha aachiwa huru Kenya
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, ameachiliwa na polisi nchini Kenya baada ya kukamatwa kwa madai ya kuingia nchini humo kinyume na sheria.
Kwa mujibu wa wakili wake, George Wajackoyah, Lema ambaye alikua ameambatana na familia yake alikua akielekea jijini Nairobi kwa ajili ya kutafuta makazi ya muda baada ya kutishiwa maisha.
Sasa mamlaka za kenya zimemruhusu Lema na familia yake kubaki nchini Kenya wakati akiendelea na taratibu za kuwa mhamiaji wa muda.
Baada ya kuachiliwa, Lema amewaeleza wanahabari kwamba alitoroka Tanzania akihofia uhai wake baada ya kupokea vitisho: