Godbless Lema: Akamatwa Kenya kwa madai ya kuingia nchini humo kinyume na sheria

Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini Kaskazini mwa Tanzania Godbless Lema anashikiliwa nchini Kenya baada ya kudaiwa kuingia nchini humo kinyume na taratibu.

Kwa mujibu wa wakili wake, Lema ambaye alikua ameambatana na familia yake alikua akielekea jijini Nairobi kwa ajili ya kutafuta makaazi ya muda.

Hata hivyo amesema kushikiliwa huko hakuhusiani kwa vyovyote vile na masuala ya kisiasa.