Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 22.09.2019: Moura, Dier, Haaland, Pogba, Zidane, Tuchel, Malen

Lucas Moura, mchezaji wa kiungo cha mbele wa Tottenham

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lucas Moura, mchezaji wa kiungo cha mbele wa Tottenham

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Tottenham Lucas Moura, mwenye umri wa miaka 27, na mchezaji wa kiungo cha kati Eric Dier, aliye na miaka 25, wapo juu kwenye orodha ya Manchester United ya wachezaji wanaolengwa kwa uhamisho. (Star)

Inaarifiwa Manchester United ina hamu ya kumsajili meneja wa Paris St-Germain Thomas Tuchel kama anayewezekana kuichukua nafasi ya Ole Gunnar Solskjaer iwapo matokeo hayatoimarika (Mail)

Wakati huo huo, Manchester United ina hamu ya kujadili kuongezwa muda kwa mkataba wa mchezaji wa kiungo cha kati anayeichezea timu ya taifa ya Ufaransa pia Paul Pogba na wakala wa mchezaji huyo wa miaka 26, Mino Raiola katika wiki chache zijazo. (ESPN)

Hatahivyo Meneja Solskjaer ana hamu ya kutomuuza Pogba kwenda Real Madrid. (Mirror)

Meneja Solskjaer ana hamu ya kutomuuza Pogba kwenda Real Madrid.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Meneja Solskjaer hataki kuumuza Pogba kwenda Real Madrid.

Arsenal inatumai kumsajili upya mchezaji wa kiungo cha mbele wa Uholanzi Donyell Malen, baada ya kufunga mabao 10 katika mechi 13 msimu huu kwa timu ya PSV Eindhoven. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 aliyeuzwa na Gunners kwa £500,000 miaka miwili iliyopita analengwa pia na timu ya Liverpool. (Mirror)

Wakati huo huo , meneja wa Arsenal Unai Emery ametoa wito wa subra kwa mashabiki wakati akijitahdi kupata matokeo mazuri kutoka kwa mchezaji aliyemsajili winga wa Ivory Coast , Nicolas Pepe, mwenye umri wa miaka 24. (Express)

Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane anasema "hana wasiwasi" kuhusu uvumi kwamba aliyekuwa bosi wa Manchester United na Chelsea Jose Mourinho huenda akaichukua nafasi yake katika timu hiyo ya ligi ya Uhispania - La Liga. (Sun)

Maelezo ya video, Video: Kipa wa Ujerumani Muhammet Sozer afunga bao la ajabu dhidi ya Uingereza

Zidane pia amedai kwamba kushindwa kwa Real Madrid kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Tottenham Christian Eriksen, mwenye umri wa miaka 27, na mchezaji wa kiungo cha kati wa Ajax Donny van de Beek, aliye na umri wa miaka 22, msimu huu wa mjira wa joto ni uamuzi wa bodi na sio wake binfasi. (Sun)

Crystal Palace, Leicester City na Middlesbrough ni miongoni mwa timu zilizo na hamu ya kumsajili beki wa kati wa Wolves Cameron John, mwenye miaka 20, ambaye anacheza kwa mkopo huko Doncaster Rovers. (Mail)

Zidane

Chanzo cha picha, Reuters

Inaarifiwa Juventus imejiunga katika kinyanganyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Red Bull Salzburg Erling Braut Haaland, mwenye umri wa miaka 19. Manchester United na Manchester City pia wana hamu ya kumsajili mchezaji huyo aliyefunga hat-trick katika ushindi wa 6-2 wa timu yake katika mechi ya ligi ya mabingwa dhidi ya Genk mapema wiki hii. (Mirror)

Aston Vila ipo tayari kushindana na Leeds United kumsajili mlinzi wa Coventry City Sam McCallum, mwenye umri wa miaka 19. (Birmingham Mail)

Huku dirisha la uhamisho likiwa limefungwa, Mkuu wa Bristol City, Lee Johnson amesema anaweza kuangalia usajili wa maajenti walio huru kufuatia jeraha la muda mrefu la goti la mshambuliaji anayecheza kwa mkopo kutoka Stoke City striker Benik Afobe, mwenye umri wa miaka 26. (Bristol Post)

Tetesi za Jumamosi

Massimiliano Allegri

Liverpool inachunguza hali ya mchezaji mwenye umri wa miaka 20 raia wa Uholanzi Donyell Malen ambaye amefunga magoli 10 katika mechi 12 akiichezea PSV Eindhoven msimu huu (Calciomercato - in Italian)

Manchester United imeanzisha mazungumzo na kiungo wa kati wa England mwenye umri wa miaka 20 Angel Gomes kuhusu mkataba mpya katika uwanja wa Old Trafford. (Manchester Evening News)

Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy anasisitiza kwamba deni la £637m la ujenzi wa uwanja mpya halitakuwa na athari yoyote kuhusu dirisha la uhamisho la klabu hiyo... (Standard)

Rais wa Real Madrid Florentino Perez na Jose Mourinho kulia

Newcastle ina hamu ya mchezaji mwenza wa Paraguay Miguel Almirons katika klabu ya Atlanta raia wa Venezuela Josef Martinez, 26. (Newcastle Chronicle)

Beki wa Ubelgiji Thomas Meunier amekiri kwamba anahisi kukerwa katika timu yake kufuatia kukosa muda wa kucheza katika timu ya PAG.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alihusishwa na kujiunga na Arsenal na Man United msimu huu. (RMC

Thomas Meunier

Mkufunzi wa Everton Marco Silva anasema kwamba klabu hiyo inafikiria uwezo wa kumsaini beki wa kati katika dirisha la uhamisho la mwezi. (Liverpool Echo)

Mkufunzi wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger atachukua wadhfa wa kiufundi katika shirikisho la soka duniani Fifa katika kipindi cha wiki chache zijazo licha ya kuwa na hamu ya kuwa mkufunzi kwa mara nyengine.. (ESPN)

Aston Villa imetenga kitita cha £20m kununua mshambuliaji mpya mwezi Januari baada ya kuwakosa wachezaji iliokuwa ikiwalenga msimu. (Football Insider)

Mkufunzi wa zamani wa Real Madrid Santiago Solari anapigania kuwa mkufunzi wa kwanza wa klabu ya David Beckham Inter Miami. (BeINSports on Twitter)

Mkufunzi wa zamani wa Real Madrid Santiago Solari

Barcelona inahitaji kitita cha Yuro za au (£88m) baada ya mauzo ya wachezaji ili kuweka sawa matumizi ya kuafikia masharti ya Fifa ya fair Play. (Marca)

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anataraji naibu wake na mchezaji wa zamani wa Everton Mikel Arteta atamrithi atakapoondoka. (Evening Standard)

Winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha, 26, amewataka wachezaji wenzake kujiimarisha wakati ambapo klabu hiyo inaendelea kushuka kwa kiwango cha mchezo. (Sun)

Wilfried Zaha

Uwanja wa klabu ya Manchester City wa Etihad Stadium umeorodheshwa kuwa uwanja bora duniani na utafiti kuhusu timu zilizoshindia mataifa na maeneo yao, wakivishinda viwanja vya timu kama Barcelona- Nou Camp na Bayern Munich - Allianz Arena. (Mail)