Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Lawrence Masira: Mvulana wa Kenya aliyetunukiwa na mchezaji wa Arsenal Mesut Ozil
Picha ya kijana mdogo akichunga ng'ombe akiwa amevaa jezi au fulana aliyoiandika jina la Mesut Ozil na chapa ya number ya mchezaji huyo imewavutia wengi katika mitandao ya kijamii akiwemo nyota mwenyewe wa soka.
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal Mesut Ozil amemnyooshea mkono mvulana mdogo kutoka nchini Kenya, Lawrence ambaye picha yake akiwa amevaa jezi bandia ilitumwa katika ujumbe wa twitter kwenye akaunti ya Ozil mwaka jana.
Tumemtafuta Lawrence, kujua zaidi kuhusu maisha yake
Video: Njoroge Muigai